
Wanajeshi wa Sudan Kusini
Vita vikali vimezuka nchini
Sudan Kusini ,siku chache tu baada ya umoja wa mataifa kuonya kuwawekea
vikwazo viongozi wa pande husika kuhusu mzozo huo.
Mapigano hayo mapya yamesababisha zaidi ya raia
elfu arobaini pamoja na wafanyikazi wa misaada kukimbilia hifadhi katika
kambi moja ya umoja wa mataifa mjini bentiu.![]() | ||||||
Kambi ya umoja wa matifa Sudani kusini |
Ujumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa ambao ulikutana na rais Salva Kiir mbali na kuzungumza na kiongozi wa waasi Riek Machar ,umewataka viongozi hao kuweka kando tofauti zao kwa lengo la kuweka amani.
Zaidi ya watu millioni moja wameyatoroka makaazi yao tangu mwezi Disemba mwaka uliopita.
![]() |
Raia wa sudan kusini wakiyakimbia makazi yao |
No comments:
Post a Comment