Morogoro.
Gari la Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH), lililokuwa likisafirisha maiti 10 za watu kwenda
katika Hospitali ya Mtakatifu Francis Ifakara, wilayani Kilombero, limewagonga watu wawili waliofariki dunia papohapo, eneo la Mtego wa Simba, Mikese mkoani Morogoro.
Waliokufa katika ajali hiyo iliyotokea saa 5:25 asubuhi jana ni dereva na abiria wa bodaboda.
Maiti hizo zilizokuwa zimehifadhiwa katika mifuko
maalumu ya plastiki, zinaelezwa kuwa zilikuwa zikipelekwa katika
Hospitali ya Mtakatifu Francis, ili zitumike kwa mafunzo.
Akizungumzia ajali hiyo katika eneo la tukio, Mkuu
wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro, Boniface Mbao
alisema kuwa gari hilo lilikuwa likiendeshwa na Pankrasi Pascal, mkazi
wa Ifakara, wilayani Kilombero.
Mbao aliwataja waliokufa kuwa ni Shaaban Rajabu
na Ally Benulo, wakazi wa Kijiji cha Mikese, waliokuwa wamepakizana
kwenye pikipiki.
No comments:
Post a Comment