Ndege ya Malaysia Flight MH 370
iliyopotea miezi mitano iliyopita imerudi tena kwenye vichwa vya habari
ikiwa na ripoti za kushangaza.
Ripoiti ya benki ya Kuala Lumpur,
Malaysia inaoensha kuwa akaunti za abiria wanne wa ndege hiyo
zimechukuliwa pesa July 18 mwaka huu fedha ambazo zitajwa kuwa zaidi ya
£20,000.
Msaidizi wa mkuu wa upelelezi wa makosa
ya jinai Malaysia, Izany Abdul Ghany ameiambia Mirror kuwa wanaendelea
kufanya uchunguzi kufahamu jinsi ambavyo pesa hizo zilivyopotea.
“We are investigating the case as
unauthorised access with intent to commit an offence,We are getting CCTV
footage from the bank to identify the suspects involved.”
Ameeleza kuwa pesa hizo zilitolewa
katika akaunti ya abiria watatu na kuwekwa katika akauti ya abiria wanne
kabla ya kutolewa kabisa.
Ndege ya Malaysia ilipotea March 8, 2014
ikiwa imebeba wafanyakazi 12 na abiria 227 kutoka katika mataifa
mbalimbali na bado haijapatikana huku maafisa wakitangaza kuwa watu wote
waliokuwa kwenye ndege hiyo wamepoteza maisha
No comments:
Post a Comment