Friday, August 29, 2014

Zanzibar yapokea vifaa kuchunguza ebola

Watahalamu wa kupambana na ugonjwa hatari wa ebola

WIZARA ya Afya ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepokea vifaa mbalimbali vya kuchunguza wagonjwa watakaobainika kuambukizwa na ugonjwa hatari wa ebola huku ikiweka mikakati zaidi kudhibiti bandari bubu zinazotumiwa kuingiza wageni kinyume cha sheria.
Akikabidhi vifaa hivyo katika kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa cha Abeid Amaan Karume,
Uwanja ndege wa Abeid Amaan Karume Zanzibar





Ofisa wa kitengo cha kupambana na maradhi kutoka Wizara ya Afya, Salma Masauni alisema kifaa hicho kinachojulikana kwa jina la 'Thermos scan' kina uwezo wa kutambua kama mgonjwa ameambukizwa ugonjwa wa homa ya ebola kwa kiasi gani.
Dr. Salma Masauni Akizungumza na wahandishi wa habari
Alisema juhudi hizo zimechukuliwa kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo ambapo vitawekwa katika sehemu zote kuu za kupokea wageni ikiwamo Uwanja wa Ndege pamoja na Bandari Kuu.
Alibainisha kuwa kabla ya vifaa hivyo vya kubaini kiasi cha ugonjwa kwa aliyeathirika na ebola ambao ni tishio kwa baadhi ya nchi zikiwamo za Afrika ya Magharibi, Zanzibar ilikuwa haina vifaa vya kupambana na ugonjwa huo.

Emmanuel Okwi atua simba kwa mkataba wa miaka miwili, Asema Yanga waniacha

Emmanuel Okwi kusaini mkataba usiku huu mkataba wa miaka miwili Simba.

“Yanga wameniacha, nikachukua uamuzi wa kurudi Simba na kuomba kuichezea nao wamenikublia.

“Najua Yanga wamenishitaki TFF au Fifa, nitaendelea kulishughulikia suala hilo wakati nikiwa naitumikia Simba.

“Nashukuru kwa kuwa wamenipokea kwa mikono miwili,” alisema Okwi akionyesha kujiamini.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema wamemchukua Okwi baada ya kuandika barua kuomba arudi.

“Tumempokea baada kuipokea barua yake na kuijadili, kwa kuwa Yanga wamemuacha na hata FIfa inasisitiza wachezaji kupata nafasi ya kucheza ili kuepusha kuua vipaji vyao, tumeamua kuwa naye,” alisema Hans Poppe. 

Baada ya kumpokea kwa mikono miwili, Simba imeamua kumrudishia Emmanuel Okwi jezi yake namba 25.

Kabla ya kuondoka kwenda Etoile du Sahel alipouzwa 'bure' na Simba chini ya Ismail Aden Rage, Okwi alikuwa akitumia jezi hiyo

Yanga pia walimpa jezi hiyo, lakini leo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amethibitisha kuwa Simba imempa Okwi namna 25.

Baada ya kupokea namba hiyo, Okwi kesho anapaa Zanzibar kuungana na wenzake ambao wako kambini kujiandaa na Ligi Kuu Bara.

Saturday, August 23, 2014

Kesi yafunguliwa Bunge la Katiba, Kesi ya kuhoji uhalali wake yafunguliwa

Wajumbe Wa Bunge la Katiba
Dar es Salaam/Dodoma. Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma kwa sasa liko katika hatihati ya kuendelea baada ya kufunguliwa kesi ya kuhoji madaraka yake.
Kesi hiyo ilifunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana na Mwandishi wa Habari Saidi Kubenea, kupitia kwa wakili wake Peter Kibatala, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
Mahakama Kuu Kanda Ya Dar Es Salaam
Katika kesi hiyo iliyopewa usajili wa namba  28 ya mwaka 2014, Kubenea anaiomba mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya Mamlaka ya Bunge la Katiba. Kubenea amefungua kesi hiyo akiomba mahakama itoe tafsiri hiyo, chini ya  vifungu vya 25 (1) na 25 (2) vya Sheria ya Marekebisho ya Katiba namba Namba 83 ya mwaka  2011.
Sambamba na kesi hiyo ya kuomba tafsiri ya mamlaka ya Bunge  hilo, pia Kubenea amewasilisha maombi mahakamani hapo akiiomba mahakama itoe zuio la muda la kusimamisha Bunge hilo ili kusubiri uamuzi wa maombi ya tafsiri hiyo.
Maombi hayo ya kusimamisha Bunge hilo kwa muda yaliyopewa usajili wa namba 29 ya mwaka 2014, pamoja na maombi ya msingi ya tafsiri ya mamlaka ya Bunge yote yalifunguliwa mahakamani hapo jana chini ya Hati ya Dharura.
Rasim Ya Katiba
Katika kesi hiyo ya msingi anaiomba Mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya masharti ya vifungu hivyo vya sheria hiyo na pia itamke kama Bunge hilo lina mamlaka ya kubadilisha maudhui ya Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kwa kiwango gani.

Clouds Yapewa Onyo na Kulipa Fiini Kwa Kukiuka Kanuni Za Utangazaji

Kituo Cha Clouds Fm Radio
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imetoa onyo pamoja na kutoza faini ya takribani Sh milioni 5 kwa kituo cha redio na televisheni cha Clouds, kwa kukiuka kanuni za utangazaji za mwaka 2005. 

Wakielezea uamuzi huo jana jijini Dar es Salaam, Kamati ya Maudhui ya mamlaka hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Margaret Munyagi ilisema kuwa ukiukwaji wa kanuni hizo ulifanywa kwa nyakati tofauti na vituo hivyo.
Kituo Cha Utangazaji Clouds Fm Radio

Alisema kwa upande wa kituo cha redio cha Clouds, kupitia kipindi chake cha ‘Njia Panda’ kilichorushwa hewani Juni 15 mwaka huu kati ya saa 8.00 mchana na saa 10.00 jioni kilikuwa na mada iliyohusu safari ya kuzimu ambapo maudhui yake yalijaa simulizi za kufikirika, za kishirikina na kichawi.

Aidha alisema kosa lingine kituo hicho hakikufuata kanuni za Utangazaji(maudhui) za mwaka 2005 zinazowataka kuwasilisha ratiba ya vipindi vyao kwa TCRA ili viidhinishwe na vilevile kuvichapisha katika gazeti kabla ya kurushwa hewani ambapo kipindi cha Njia Panda hakikuwasilishwa kwa ajili ya kuidhinishwa.
Majaji Wa Shindano La Bibi Bomba Clouds Televion

Wakati huo huo, kituo cha televisheni cha Clouds kilirusha kipindi cha ‘Bibi Bomba’ Mei 16 na Juni 6 mwaka huu kati ya saa 3.00 na saa 4.00 usiku ambacho kilikiuka kanuni za Utangazaji (maudhui) za mwaka 2005.
Rebo Ya Clouds TV

Alisema kipindi hicho kilidhalilisha mabibi hao walioshiriki pamoja na wanawake kwa ujumla kutokana na maswali ya aibu waliyokuwa wakiulizwa na waamuzi wa shindano hilo ambayo ni kinyume na kanuni hizo.
Washiriki Wa shindano La Bibi Bomba

Aidha alisema kituo hicho kinatozwa faini ya Sh milioni moja na kutakiwa kuwasilisha TCRA mwongozo wa kuchuja na kusimamia maudhui yasiyofaa kabla ya kutangazwa.

TCRA imesema kama Kanuni za Utangazaji zitaendelea kukiukwa hatua kali zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Diamond atangaza ndoa

Diamond na Wema wakiwa kwenye Pozi

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platinumz ametangaza ndoa na mchumba wake wa muda mrefu Wema Sepetu anayosema itafungwa hivi karibuni.
Msanii huyo ghali zaidi nchini kwa sasa, ametamka hayo alipozungumza na Mwanaspoti nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam juzi Jumatano. Alisema kuna mambo mengi yaliyomchelewesha kufikia hatua hiyo, ikiwamo maandalizi kwani amepanga mashabiki wake wahudhurie harusi hiyo.
Pete ya Uchumba

“Ndoa ni kitu cha heri na baraka, lakini kitu kinachofanya kidogo mambo yachelewe ni kwamba sisi au mimi ni mtu ninayefahamika, kwa hiyo hata ndoa yangu watu wengi wanatamani waihudhurie,” alisema Diamond.
Pia amesisitiza kwamba ndoa si jambo la masihara kwani ni tendo la kiimani na ndio maana amekuwa makini katika mipango yake.
Wema Akionyesha Pete Ya Uchumba Aliyevishwa na Diamond

“Nataka kila kitu kishuhudiwe na mashabiki, ninaweza hata kuifanyia Uwanja wa Taifa,” aliongeza.
“Unajua nilishindwa kufanya mambo haya haraka kwa sababu wengi nadhani wangeamini kwamba ninafanya hivyo ili kutafuta umaarufu zaidi, tunataka tufanye kiusahihi yasije tokea mambo kama ya Instagram tunataka tuje kuwa mfano wa kuigwa.”
Pete Ya Uchumba Na Ndoa

Alipoulizwa tarehe ya ndoa hiyo Diamond alisema: “Nilishasema ni hivi karibuni, unajua siku zote vitu vya kheri waswahili wanasema lazima uvifiche, hata Mwenyezi Mungu naye anasema anampenda mtu aliye na siri, lazima vitu vingine uvifiche ili vipate kufanikiwa.
Wakati mwingine kunakuwa na husda, hasidi kwa hiyo ukiviweka wazi sana vinaweza kutofanikiwa.”
Taarifa kwamba Diamond hataoa zilisambaa na kudaiwa kumchefua mchumba wake Wema Sepetu ambapo katika mahojiano mkali huyo wa wimbo ‘Mdogo Mdogo’
Moja ya Sehemu ya kumbi za Harusi

Friday, August 22, 2014

Rais Kikwete asafiri kwa treni kwa mara ya Kwanza

Rais Kikwete akiwa kwenye behewa maalum la Tazara

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, jana, Alhamisi, Agosti 21, 2014, ameweka historia nyingine katika ziara yake ya Mkoa wa Morogoro wakati aliposafiri kwa treni ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), ikiwa ni mara yake ya kwanza kutumia usafiri huo katika kipindi chake cha Urais.
Rais Kikwete, akifuatana na Mama Salma Kikwete, amesafiri kilomita 143 ndani ya Behewa la Kirais (Presidential Coach) la T-One kwa kiasi cha saa tatu na dakika 25 akitokea stesheni ya Ifakara katika Wilaya ya Kilombero kwenda Stesheni ya Kisaki, Wilaya ya Morogoro.
Rais Kikwete akiwapungia mkono wananchi wa Ifakara

Rais Kikwete akiandamana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mheshimiwa Joel Bendera na Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa John Pombe Magufuli, amepanda treni hiyo kiasi cha saa 4:45 asubuhi Ifakara na kushuka 8:10 mchana wakati alipowasili Kisaki. Kwa muda mwingi alikuwa katika Chumba cha Mikutano (Conference Room) cha Behewa la Kirais hilo ambalo pia lina huduma nyingine nyingi za Kirais.
Rais kikwete akiwa na viongozi mbalimbali ndani ya treni





Rais Kikwete anakuwa Rais wa tatu wa Tanzania kutumia Behewa hilo na kusafiri ndani ya treni ya TAZARA. Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambaye TAZARA ilibuniwa na kujengwa chini ya uongozi wake, alitumia Behewa hilo na treni hiyo mara mbili, mara ya kwanza ikiwa mwaka 1976 aliposafiri na mgeni wake, aliyekuwa Rais wa Sierra Leone, Mheshimiwa Siaka Stevens.
Rais wa Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi pia alitumia Behewa hilo na usafiri wa TAZARA mara mbili wakati Rais wa Tatu, Mheshimiwa William Mkapa hakupata kutumia Behewa hilo wala usafiri wa TAZARA.
Hiyo ilikuwa mara ya pili kwa Rais Kikwete kuweka historia katika ziara yake ya siku saba katika Mkoa wa Morogoro iliyoanza jana, Jumatano, Agosti 20, 2014.
Rais Kikwete akiwajulia hari wagonjwa hospitari ya wilaya kilombero









Katika siku yake ya kwanza jana, msafara wa Rais Kikwete, uliweka historia kwa kuwa magari ya kwanza kuvuka Mto Kilombero kwa kutumia daraja, ukiwa unatokea Wilaya ya Ulanga kuingia Wilaya ya Kilombero ambako Rais aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja kamili kwenye Mto huo.
Msafara huo, ulivuka Mto huo kwa kutumia daraja jembamba la chuma ambalo linatumiwa kama daraja la muda na mafundi wa Kampuni ya Kichina ambayo inajenga daraja kubwa  kwenye Mto huo linalogharimu Sh. bilioni 56 zinazotolewa na Serikali ya Tanzania.
Kutokana na adha ya karne na karne ambayo wananchi wa wilaya hizo mbili wamekuwa wanaipata kuvuka Mto Kilombero kwa kivuko na hata mitumbwi, wananchi wa maeneo hayo wamelipachika Daraja hilo jina la Daraja la Ukombozi.
Daraja la Mto Kilombero ni moja ya madaraja makubwa matatu ambayo Rais Kikwete, katika kampeni yake ya Urais ya mwaka 2005, aliahidi kuyajenga na ambayo yaliwekwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Madaraja mengine ni lile la Kigamboni, Dar Es Salaam, ambalo ujenzi wake unaendelea na Daraja la Mto Malagarasi Mkoani Kigoma ambalo ujenzi wake umekamilika.
Madaraja hayo matatu, na mengine mawili, ya Kirumi kwenye Mto Mara na la Rufiji ni madaraja ambalo yalikuwa yamepangwa kujengwa katika Mpango wa Kwanza wa Taifa wa Maendeleo. Daraja la Kirumi lilijengwa wakati wa uongozi wa Mwalimu Nyerere na lile la Rufiji lilijengwa wakati wa uongozi wa Mzee Mkapa. Matatu yaliyobakiwa yamejengwa wakati wa Uongozi wa Rais Kikwete.

Rais kikwete na Mama Salma wakiwasili katika kituo cha tazara Kisaki

Wednesday, August 20, 2014

Ukawa gumzo Kamati Kuu CCM

Mwenyekiti wa CCM Rais J.K. Kikwete
Dodoma. Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), jana ulikuwa gumzo katika kikao cha Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mjini hapa.
Mjadala katika kikao hicho ulijikita kusaka mwafaka na moja ya maazimio yake, ni kuendelea majadiliano ya kusaka maridhiano baina ya chama hicho na vyama vinavyounda Ukawa ili kukwamua mchakato wa Katiba Mpya.
Rasimu ya Katiba
Kamati hiyo ilitoa maelekezo hayo baada ya kupokea na kujadili taarifa kuhusu mchakato wa Katiba Mpya pamoja na taarifa za mazungumzo ya kusaka maridhiano yaliyofanyika katika ngazi tofauti na kwa nyakati tofauti.
Habari kutoka ndani ya CC iliyofanyika chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete ziliyataja mazungumzo hayo kuwa ni yale yaliyowahusisha makatibu wakuu wa vyama, yale yaliyofanyika chini ya uratibu wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na yaliyoratibiwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi.
“Kamati Kuu imemwagiza Katibu Mkuu (Abdulrahman Kinana)
Katibu Abdulheman Kinana
kuendelea na jitihada za mazungumzo tena kwa uzito zaidi, maana sisi (CCM) hatujawahi kukataa mazungumzo na tumeona baadhi ya mapendekezo yao yana maana sana na yana nafasi yake katika mchakato huu,” kilisema chanzo chetu kutoka ndani ya kikao hicho.
Wenyeviti wa umoja wa Ukawa
Chanzo chetu kilimnukuu Rais Kikwete akisema kwa kuzingatia mchakato wa Katiba ulivyo, si vyema kupuuza kila kinachosemwa na wapinzani kwani baadhi ya mawazo yao yanaweza kuongeza thamani katika mchakato huo.

Habari zinasema maelekezo ya kuwashawishi Ukawa ili warejee katika meza ya mazungumzo na baadaye bungeni, ni matokeo ya mjadala ulioonyesha kutokuwapo kwa uwezekano wa kupatikana kwa theluthi mbili ya kura kutoka Tanzania Zanzibar wakati wa kupitisha Rasimu ya Katiba katika Bunge Maalumu.
“Baada ya hesabu kupigwa ilionekana kwamba tunahitaji kura 141 kutoka Zanzibar na kwa hesabu za pale kikaoni ilisemekana kwamba tayari tuna kura za uhakika 135, kwa hiyo zinazotafutwa ni kura sita tu,” kilisema chanzo kingine na kuongeza:

Tuesday, August 19, 2014

Jaji Lewis Makame afariki dunia

Jaji Lewis makame anzi ya uhai wake
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Lewis Makame, amefariki dunia katika Hospitali ya Ami Trauma Centre iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa kwa maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.
Jaji Makame alifariki jana mchana katika hospitali hiyo, alikokuwa amelazwa ambapo pia Rais Jakaya Kikwete, alimtembelea kumjulia hali.
Rais Jakaya  Kikwete akimjulia hali Jaji Lewis Makame
Taratibu za mazishi zilikuwa zikiendelea jana nyumbani kwake Masaki.
Historia fupi iliyopatikana, inaonesha kuwa Jaji Makame alikuwa na Shahada ya Kwanza ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha London nchini Uingereza, ambapo baada ya kufanya mazoezi na kufanya kazi nchini humo, alirejea nchini Tanzania miaka ya 1960 na kutumikia Taifa mpaka alipofikia cheo cha Jaji wa Mahakama ya Rufaa.
Jaji Lewis Makame akilitumikia Taifa
Mbali na cheo hicho, Jaji Makame pia alitumikia Taifa katika nafasi ya Mwenyekiti wa NEC na Mwenyekiti wa Jukwaa la Tume za Uchaguzi za Nchi Wanachama wa Jumuiya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-ECF).

Maandamano ya albino yasambaratishwa Dar

Walemavu wa ngozi wakiandamana kituo cha polisi buguruni
MAANDAMANO ya walemavu wa ngozi kwenda Kituo cha Polisi Buguruni jijini Dar es Salaam jana, yalisambaratishwa kwa mabomu ya machozi na askari Polisi, baada ya waandamanaji hao kuzingira kituo hicho na kukaidi amri ya kutawanyika.
Kituo cha Polisi Buguruni
Waandamanaji hao walitokea Mahakama ya Mwanzo Buguruni kwenda katika kituo hicho, kulalamikia uamuzi wa Mahakama hiyo kutoa dhamana kwa mshitakiwa, Ombeni Swai, mkazi wa Tabata Matumbi, anayedaiwa kutishia kumuua mwenzao.
Kabla ya maandamano hayo, Swai alifikishwa mahakamani hapo, mbele ya Hakimu Mfawidhi, Benjamini Mwakasona na kushitakiwa kwa kosa la kutishia kumuua mlemavu wa ngozi, Mwinyisi Issa.
Karani wa mahakama hiyo, Edwin Mwandawanda alidai mahakamani hapo kwamba Swai alitishia kwa maneno kumuua Issa Agosti 16 mwaka huu, saa 7 mchana katika eneo la Buguruni Wilaya ya Ilala.

Sunday, August 17, 2014

Waliokimbia zahanati ya ebola watafutwa


Ebola  Liberia
Kituo kilichotengwa na kuwekewa karantini kwa sababu ya ebola, kimeshambuliwa na zana kuporwa katika mji mkuu wa Liberia, Monrovia.
Watu kama 20 hadi 30 waliowekwa hapo kuangaliwa kama wana dalili za ebola walitoroka baada ya kituo hicho kuporwa Jumamosi usiku.
Kituo cha wagonjwa wa Ebola
Kituo kiko kwenye mtaa wa West Point, wenye wakaazi wengi.
Washambuliaji walipora magodoro na vitu vyengine.
Mwandishi  anasema pengine washambuliaji walikerwa kuwa kituo hicho kimewekwa katika mtaa wao.
Wakuu wa Liberia wanajaribu kuwatafuta wagonjwa waliotoroka ili kuwarejesha tena kwenye kituo hicho.
Watu zaidi ya 400 wamekufa kwa sababu ya ebola nchini Liberia kati ya zaidi ya 1,000 katika kanda ya Afrika Magharibi.

Kitaifa Gari lililobeba maiti kumi laua wawili Mikese

Morogoro.
Gari la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), lililokuwa likisafirisha maiti 10  za watu kwenda katika Hospitali ya Mtakatifu Francis Ifakara,
wilayani Kilombero, limewagonga watu wawili waliofariki dunia papohapo, eneo la Mtego wa Simba, Mikese mkoani Morogoro.
Waliokufa katika ajali hiyo iliyotokea saa 5:25 asubuhi jana ni dereva na abiria wa bodaboda.
Maiti hizo zilizokuwa zimehifadhiwa katika mifuko maalumu ya plastiki, zinaelezwa kuwa zilikuwa zikipelekwa katika Hospitali ya Mtakatifu Francis, ili zitumike kwa mafunzo.
Akizungumzia ajali hiyo katika eneo la tukio, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro, Boniface Mbao alisema kuwa gari hilo lilikuwa likiendeshwa na Pankrasi Pascal, mkazi wa Ifakara, wilayani Kilombero.
 Mbao  aliwataja waliokufa kuwa ni Shaaban Rajabu na Ally Benulo, wakazi wa Kijiji cha Mikese, waliokuwa wamepakizana kwenye pikipiki.

Saturday, August 16, 2014

Vita vipya vyazuka nchini Sudan Kusini

Wanajeshi wa Sudan Kusini


Vita vikali vimezuka nchini Sudan Kusini ,siku chache tu baada ya umoja wa mataifa kuonya kuwawekea vikwazo viongozi wa pande husika kuhusu mzozo huo.
Mapigano hayo mapya yamesababisha zaidi ya raia elfu arobaini pamoja na wafanyikazi wa misaada kukimbilia hifadhi katika kambi moja ya umoja wa mataifa mjini bentiu.

Kambi ya umoja wa matifa Sudani kusini





Idadi ya watu nchini Sudan Kusini tayari inatishiwa kuangamizwa na uhaba wa chakula kutokana na mzozo huo.
Ujumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa ambao ulikutana na rais Salva Kiir mbali na kuzungumza na kiongozi wa waasi Riek Machar ,umewataka viongozi hao kuweka kando tofauti zao kwa lengo la kuweka amani.
Zaidi ya watu millioni moja wameyatoroka makaazi yao tangu mwezi Disemba mwaka uliopita.
Raia wa sudan kusini wakiyakimbia makazi yao

Mjadala mkali wabunge kuteuliwa kuwa mawaziri

Wajumbe wa bunge la katiba wakiwakwenye kikao Dodoma
SUALA la mawaziri kuwa wabunge au hapana, limezua mjadala mkali katika vikao vya kamati mbalimbali za Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea mjini hapa. Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Makamu Mwenyekiti wa Kamati Namba 10, Salmin Awadhi Salmin, alisema katika kamati yake mjadala kuhusu Rasimu ya Katiba ni mzuri na wajumbe wamekuwa wakitoa hoja mbalimbali za kuiboresha.
"Yapo mambo mengi yamejitokeza katika majadiliano ya ibara za sura mbalimbali tulizojadili kwa wiki hii, ambazo ni Sura ya 7,8, 11, 14 na 15, lakini mjadala mkubwa ulikuwa kwenye suala la mawaziri wawe wabunge au vipi.
Baraza jipya la mawaziri
"Kama mnavyojua Rasimu ya Tume ya Jaji Joseph Warioba imependekeza mawaziri wasitokane na wabunge ili kuweka mgawanyo mzuri wa madaraka," alisema Mwenyekiti huyo.
Alifafanua kuwa wajumbe wanaounga mkono ibara hiyo, licha ya suala la mgawanyo wa madaraka, lakini pia wanajenga hoja kuwa lazima mihimili hiyo ijitegemee kwa maana ya Bunge na Serikali.
"Wanasema mawaziri wakiwa wabunge kama ilivyo sasa, wakiwa kwenye vikao vya bunge wanatetea msimamo wa serikali zaidi, pia mgawanyo wa madaraka unakua haupo.
"Wanaotaka mawaziri waendelee kuwa wabunge, wanasema ukiwatoa nje ya Bunge inakuwa ngumu hasa unapotaka ufafanuzi wa mambo mbalimbali yanayofanywa na serikali, kwa vile waziri anaweza kupanga safari yoyote kwani hahusiki na Bunge," alisema Salmin.

Hoja mpya zalichanganya Bunge Maalumu

Dodoma. Mapendekezo mapya yanayopelekwa kwenye Kamati za Bunge Maalumu kwa ajili ya kurekebisha baadhi ya Ibara za Rasimu ya Katiba, yamezua mivutano mikali kiasi cha baadhi ya sura kuwekwa kiporo au kurukwa na kamati husika.
Habari,zinasema mapendekezo hayo ni yale yanayozigusa taasisi kubwa za nchi, zikiwamo Bunge la Jamhuri ya Muungano na Mahakama, pamoja na nafasi za Makamu wa Rais.
Katika baadhi ya kamati yamepelekwa mapendekezo ambayo yanataka Bunge liwe na sehemu tatu ili kutoa fursa kwa mambo ya Tanzania Bara kujadiliwa bila wabunge kutoka Zanzibar kuwapo.
“Mapendekezo yaliyopo ni kwamba wanataka Bunge liwe na sehemu tatu ambazo ni Bunge la Muungano kwa masuala ya muungano na humohumo linakuwa na sehemu mbili ambazo ni wabunge wa Zanzibar kwa ajili ya masuala ya Wazanzibari na sehemu ya Tanganyika kwa ajili ya mambo ya bara,” kilisema chanzo chetu kutoka katika kamati moja ya Bunge hilo.

Ndege ya Malaysia Iliyopotea,Ripoti ya Benki Zinaonyesha Abiria Wanaeendelea Kuchukua Pesa.

Ndege ya Malaysia Flight MH 370 iliyopotea miezi mitano iliyopita imerudi tena kwenye vichwa vya habari ikiwa na ripoti za kushangaza.

Ripoiti ya benki ya Kuala Lumpur, Malaysia inaoensha kuwa akaunti za abiria wanne wa ndege hiyo zimechukuliwa pesa July 18 mwaka huu fedha ambazo zitajwa kuwa zaidi ya £20,000.

Msaidizi wa mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Malaysia, Izany Abdul Ghany ameiambia Mirror kuwa wanaendelea kufanya uchunguzi kufahamu jinsi ambavyo pesa hizo zilivyopotea.

 “We are investigating the case as unauthorised access with intent to commit an offence,We are getting CCTV footage from the bank to identify the suspects involved.”

Ameeleza kuwa pesa hizo zilitolewa katika akaunti ya abiria watatu na kuwekwa katika akauti ya abiria wanne kabla ya kutolewa kabisa.

Ndege ya Malaysia ilipotea March 8, 2014 ikiwa imebeba wafanyakazi 12 na abiria 227 kutoka katika mataifa mbalimbali na bado haijapatikana huku maafisa wakitangaza kuwa watu wote waliokuwa kwenye ndege hiyo wamepoteza maisha

Friday, August 15, 2014

J.K Kikwete Asema Urais Pacha Kwa Sasa Ni Ndoto

Dar/Dodoma. Rais Jakaya Kikwete amesema suala la uraia wa nchi mbili linaonekana kutokuwa na nguvu kwa sasa kutokana na kutojitokeza katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba, hivyo kutoingia katika Rasimu ya Katiba inayojadiliwa sasa bungeni.

Kauli ya Rais Kikwete imekuja wakati suala hilo likionekana kuwagawa wajumbe katika Kamati za Bunge Maalumu, kutokana na kuwapo kwa mapendekezo kwamba suala uraia pacha liingizwe kwenye rasimu hata kama halikuwekwa na Tume.

Juzi, suala hilo liliwagawa wajumbe wa Kamati Namba mbili inayoongozwa na Waziri Kiongozi mstaafu wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha na kusababisha ibara hiyo kukosa theluthi mbili ya kura kutoka pande zote za muungano.

Akizungumza katika kongamano maalumu linalowakutanisha Watanzania waishio nje ya nchi Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alisema suala hilo limekosa wasemaji wanaoguswa moja kwa moja ambao wangeweza kulitetea, hivyo kutokuwa miongoni mwa vipaumbele katika rasimu hiyo.

“Msijipe matumaini kwa sababu kwa namna ilivyoandikwa kwenye Rasimu ya Katiba, haiwezi kuzaa uraia wa nchi mbili, bali inaweza kutoa stahiki ya fursa wanazoweza kupata Watanzania waishio nje ya nchi, kupitia sheria,” alisema.

Kongamano hilo la kwanza la siku mbili linawakutanisha Watanzania waishio katika nchi 17 duniani, lililoandaliwa na Asasi ya Tanzania Diaspora Initiative (TDI).

Rais Kikwete alisema Serikali yake inafahamu umuhimu wa kupatikana kwa uraia pacha kwa watu wake lakini suala la uraia ni la kikatiba na siyo la Rais kwa kuwa Katiba ndiyo inayoamua.

Alisema hata chama chake (CCM), kilipojaribu kuliingiza lilionekana kutokuwa na nguvu ya kutosha kwa kuwa hakuna ambaye lilikuwa likimgusa moja kwa moja.

Aliwashauri kuwatumia wajumbe katika Bunge linaloendelea mjini Dodoma ili wapaze sauti zao na ikiwezekana watumie fursa zote za mawasiliano kufikisha ujumbe wao.

“Sisi upande wa Serikali tunaliona ni suala jema, ila halina nguvu kwa sababu wabunge wengi haliwagusi moja kwa moja, hivyo si rahisi kulipigania. Mbona nchi nyingine watu wao wananufaika na hili! Kwa nini hapa kwetu lishindikane?” alihoji.

Ndani ya kamati

Habari kutoka ndani ya kamati zinasema wajumbe wamegawanyika kuhusu suala hilo na wengine wameshindwa kufikia mwafaka kama ilivyotokea katika Kamati namba 11 inayoongozwa na Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela.

Mwandishi wetu alidokezwa kuwa kulikuwa na mvutano mkali kuhusu pendekezo la kuanzishwa kwa uraia pacha na hadi sasa uamuzi wa kura bado haujafanyika kuhusu suala hilo na wajumbe wa Kamati namba tano inayoongozwa na Hamad Rashid Mohamed walikubaliana kwa kauli moja kuongeza ibara inayoruhusu kuanzishwa kwa uraia pacha.

Itakumbukwa kuwa suala hilo ndilo lilizua mvutano mkali baina ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsi na Watoto, Sophia Simba kiasi cha kutoleana maneno makali wakati wakilijadili kwenye Kamati namba 6 inayoongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wasira.

Ugonjwa wa Ebola Wahofiwa kufika Nchi

Ugonjwa Hatari wa Ebola umeingia nchini kufuatia watu wawili wanaodhaniwa kuwa na maambukizi yake kuwasili nchini.
Wagonjwa hao wamepelekwa katika kituo maalumu kwa ajili ya wagonjwa wa ugonjwa huo kilichopo Temeke jiji Dar es salaam.

Watu hao wawili walipatikana katika uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Baada ya Kuwasili kutoka sehemu tofauti , mmoja ni raia wa Benin na Mwingine ni Mtanzania.

Wednesday, August 13, 2014

Ukawa wamtaka Rais Jakaya Kikwete kusitisha bunge maalumu.


Tanzania kuongoza Afrika wataalamu wa gesi

Waziri wa nishati na madini Mh. Prof. Sospeter Muhongo
UTEKELEZAJI wa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete, ya kumwachia mrithi wake mazingira ya kuongoza nchi tajiri, umeanza kutoa mwanga, ambapo Tanzania sasa inajiandaa kuongoza Afrika kwa kuwa na wataalamu wazawa wa mafuta na gesi.
Jana Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alitangaza kuwa katika miaka mitano ijayo, Tanzania itakuwa na wataalamu zaidi ya 300, watakaokuwa wamebobea katika masuala hayo kutoka katika vyuo mbalimbali vya kimataifa.
Aidha, wakati Serikali ikitarajia kuwa na wataalamu hao miaka mitano ijayo, yaani 2020, ni wakati huo huo Tanzania itakuwa ikianza kupokea mapato yake ya kwanza kutokana na rasilimali hiyo.

Hospital za wagonjwa wa ebola zatajwa

PAMOJA na kuwa mpaka sasa hakuna mgonjwa mwenye virusi vya homa hatari ya ebola, wala anayehisiwa kuwa na ugonjwa huo nchini, Serikali imeshajiandaa kukabiliana na ugonjwa huo, ambao umeshaua zaidi ya watu 1,000 katika nchi za Afrika Magharibi.


Katika maandalizi hayo, Serikali imeagiza vituo kadhaa katika mikoa yote, kuwa tayari kutoa huduma endapo atatokea mgonjwa aliyepata maambukizi ya ugonjwa huo nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu hatua hizo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid alisema katika vituo hivyo vifaa kinga pamoja na dawa vimeshaandaliwa.
“Katika Mkoa wa Dar es Salaam, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Temeke Isolation Unit, yametengwa maeneo ya kuhudumia wagonjwa wa ebola endapo watatambuliwa. Eneo la Temeke bado linaendelea kuboreshwa kwa kuzingatia vigezo maalumu ili likidhi mahitaji ya matibabu ya ugonjwa huu,” alisema Dk Rashid.