Saturday, April 4, 2015

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amemteua Rais Kikwete kuwa Mwenyekiti wa Jopo la majanga ya kiafya

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon, amemteua Rais Jakaya Kikwete kuwa Mwenyekiti wa Jopo la Ngazi ya Juu kuhusu Mwitikio wa Kimataifa wa Majanga ya Afya.

Kwa mujibu wa tangazo la uteuzi huo lililotolewa juzi, katika jukumu hilo la kimataifa, Rais Kikwete ataongoza wajumbe wengine akiwemo Delos Luiz Amorim wa Brazil, Micheline Calmy-Rey wa Switzerland, Marty Natalegawa wa Indonesia Joy Phumaphi wa Botswana na Rajiv Shah wa Marekani.

Jopo linatarajiwa kufanya kikao chake cha kwanza mapema Mei mwaka huu na linatarajiwa kuwasilisha taarifa yake kwa Katibu Mkuu wa UN mwishoni mwa Desemba, 2015.

Akizungumzia uteuzi huo, Rais Kikwete alisema amepokea kwa furaha na unyenyekevu.

“Ni majukumu makubwa na yenye changamoto nyingi, lakini dunia inahitaji tuwe na mikakati katika masuala haya ambayo ni muhimu kwa maisha ya binadamu. “Hatuna budi kufanya kazi hii na kutoa mchango wetu kwa ajili ya maisha ya wanadamu na dunia kwa ujumla,” alisema Rais Kikwete.

Rais wa Jamuri ya muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete

No comments:

Post a Comment