Mcheza
filamu Zohra Sehgal wa India, maarufu kama mkongwe wa Bollywood,
amefariki dunia mjini Delhi akiwa na umri wa miaka 102. Mkongwe huyo
alianza fani yake kama mcheza dansi na baadaye kuingia katika uigizaji
ambapo alijipatia tuzo kadhaa katika filamu za Bollywood. Katika miaka
ya 1960 alihamia London ambapo aliishi kwa miaka 30 kabla ya kurejea
India. Filamu ambazo ametajwa za Hollywood na za Uingereza ni: Never Say
Die, Bend It Like Beckham, The Jewel in the Crown, My Beautiful
Laundrette na Bhaji on the Beach.

No comments:
Post a Comment