Ukraine
imetuhumu waasi wanaoiunga mkono Urusi kwa kujaribu kuharibu ushahidi
wa "uhalifu wa kimataifa" katika eneo ndege ya Malaysia ilipoanguka.
Serikali imesema waasi wakiongozwa na Urusi wanazuia wawakikishi wa kimataifa na wataalam wake kuzuia uchunguzi.
Inaaminika ndege hiyo namba MH17 ilianguka baada ya kudunguliwa na
kombora, katika eneo linalodhibitiwa na waasi mashariki mwa Ukraine siku
ya Alhamisi.
Watu wote 298 waliokuwemo ndani walipoteza maisha.
Ndege hiyo aina ya Boeing 777 ilikuwa ikisafiri kutoka Amsterdam kwenda
Kuala Lumpur. Ilianguka kati ya Krasni Luch katika eneo la Lihansk na
Shakhtarsk karibu na Donetsk.
Katika taarifa yake, serikali ya
Ukraine imelalamika kwa kusema "magaidi" wamechukua miili 38 na
kuipeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti katika eneo linalodhibitiwa
na waasi katika jiji la Donetsk. Imesema pia waasi wanajaribu
kusafirisha mabaki ya ndege kwenda Urusi.
No comments:
Post a Comment