Ndege ya shirika la Algeria iliyokuwa
imebeba abiria 116 ambayo awali iliripotiwa kuwa imepoteza mawasiliano
kwa zaidi ya dakika 50 imethibitishwa kuwa imeanguka.
Kwa mujibu wa Aljazeera, maafisa wa
Algeria wamethibitisha kuwa ndege hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka
Burkina Faso kwenda katika mji mkuu wa Algeria, Algiers imeanguka Kusini
mwa Mali.
Maafisa wa serikali ya Ufaransa
wameeleza kuwa ndege hiyo AH5017 ilipotea kwenye radar katika eneo la
Mali baada ya mvua kubwa kunyesha na inaelezwa kuwa vipande vya ndege
hiyo vimeanza kuonekana baharini.
Ndege hiyo inayomilikiwa na kampuni
binafsi ya Hispania inayofahamika kama Swiftair ilikuwa imebeba abiria
110 na wafanyakazi sita.
No comments:
Post a Comment