Watu
wengi wanahofiwa kufa baada ya watu wanaodhaniwa kuwa wanamgambo wa
Boko Haram kushambulia mji wa Damboa, kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Watu walioshuhudia wameiambia BBC kuwa nusu ya mji huo umeteketezwa kwa
moto, likiwemo soko kuu. Mkazi mmoja amesema mashambulio hayo yalifanywa
siku ya Alhamis usiku na kuendelea hadi saa za alfajiri. Mji wa Damboa
uliopo kilomita 85 kutoka mji mkuu wa jimbo la Borno, Maiduguri sasa
hauna watu kutokana na wenyeji kukimbia
ghasia hizo. Boko Haram ilishambulia kambi za jeshi mjini humo wiki
mbili zilizopita na kuua wanajeshi kadhaa. Wizara ya ulinzi ya Nigeria
imesema jeshi lilizuia shambulio hilo na kuua wanamgambo 50. Hata hivyo
wakazi wanasema mji huo sasa unalindwa na makundi ya sungusungu.
Boko Haram wakati mwingine wameonekana kuwa na silaha nzito kuliko hata majeshi ya serikali.
No comments:
Post a Comment