Tuesday, July 29, 2014

Ajira Uhamiaji zapigwa ‘stop

AJIRA za washindi 200, walioitwa kufanya usaili wa nafasi za ajira za Konstebo na Koplo wa Uhamiaji, zimesitishwa kupisha uchunguzi wa utaratibu wa uteuzi wa washindi hao.
Hatua hiyo imekuja katika siku chache, tangu kulipoibuka utata, uliotokana na kuitwa kwa watu zaidi ya 10,000 wenye shahada za kwanza, kufanya usaili wa nafasi 70 tu za Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, zilizokuwa wazi katika Idara hiyo.
Taarifa ya Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga, kwa vyombo vya habari jana, ilieleza kuwa hatua hiyo ya kusitisha ajira hizo, imechukuliwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil.
Kwa mujibu wa Nantanga, hatua hiyo imechukuliwa baada ya kuibuka tuhuma kuwa kati ya washindi hao 200, ambao walishatangazwa na kutakiwa kuanza kazi Jumatano ya wiki ijayo, sehemu kubwa ni ndugu na jamaa za wafanyakazi wa Uhamiaji.
“Kutokana na kusitishwa kwa ajira hizi, waombaji wote walioitwa na kutakiwa kuripoti Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji tarehe 6, Agosti 2014, sasa wanatakiwa kusubiri hadi hapo watakapotangaziwa tena baada ya uchunguzi huu kukamilika na uamuzi kufanyika,” alieleza Nantanga katika taarifa yake.
Tayari Katibu Mkuu, Abdulwakil, ameshaunda Kamati Ndogo ya Uchunguzi wa suala hilo. Taarifa zilizofikia gazeti hili jana, zilieleza kuwa kuna uwezekano muda wa uchunguzi huo na hadidu za rejea, vitajulikana leo.
Sifa za wasailiwa
Sifa za wasailiwa 100 katika nafasi ya Koplo wa Uhamiaji, zilikuwa awe amehitimu Kidato cha Sita na kufaulu, bila kutaja kiwango cha ufaulu ; na ya pili ni umri usiozidi miaka 30.
Kwa nafasi 100 za Konstebo wa Uhamiaji, sifa zilikuwa awe amehitimu Kidato cha Nne na kufaulu, bila kutaja kiwango cha ufaulu, na awe na umri usiozidi miaka 25.
Majukumu na kazi zao, zilikuwa kufungua, kupanga na kutunza majalada ya huduma mbalimbali za Uhamiaji, kuandika hati mbalimbali za Uhamiaji, kufanya doria sehemu za mipakani, bandarini, vituo vya mabasi, treni na sehemu zenye vipenyo vya kuingia na kutoka nchini, vikiwemo vya majini.
Nyingine ni kusindikiza watuhumiwa wa kesi za Uhamiaji mahakamani pamoja na wageni wanaofukuzwa nchini, kufanya ukaguzi kwenye mahoteli, nyumba za kulala wageni na sehemu za biashara, kuchapa au kuandika kwa kompyuta barua au nyaraka mbalimbali zinazohusu kazi za kila siku za Uhamiaji, kufanya matengenezo/ ukarabati wa mitambo na vitendea kazi vya Uhamiaji na kuandaa na kutunza takwimu za huduma mbalimbali za uhamiaji.
Tuhuma Tuhuma hizo zilizosambaa katika mitandao ya jamii, zilidai kuwa matokeo ya usaili wa nafasi za kazi Uhamiaji, yaliyotolewa katika magazeti, yameonesha kuwa katika Idara hiyo Watanzania wengine, mbali ya watoto au ndugu wa wafanyakazi wa Idara hiyo, hawawezi kupata ajira ndani ya Idara hiyo ya Serikali kirahisi.
“Majina ya wengi walioitwa kazini ni watoto au ndugu wa wafanyakazi wa idara hiyo,” ilieleza taarifa hiyo, iliyosambazwa katika mitandao na kutaja majina ya wanaodaiwa kuwa ni washindi wa usaili huo na uhusiano wao na maofisa wa Uhamiaji. “Hii ni sampuli tu, ila zaidi ya asilimia tisini ni watoto na ndugu wa maofisa Uhamiaji. Nadhani ingekuwa vyema wasingekuwa wanatangaza nafasi hizi, bali wawe wanagawiana ndani kwa ndani. Alamsiki,” ilieleza taarifa hiyo.
Utata usaili Hivi karibuni Idara ya Uhamiaji ilipotangaza majina ya wasailiwa zaidi ya 10,000, waliotakiwa kushindania nafasi 70 za Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji. Hatua hiyo ilisababisha utata, kutokana na uchache wa nafasi, ikilinganishwa na wasailiwa walioitwa.
Utata huo ulisababisha kuibuka kwa hisia za usaili huo, kugubikwa na rushwa, kiasi kwamba Nantanga alilazimika kutoa taarifa, kukanusha kuwepo kwa tuhuma hizo.
“Tuhuma za rushwa zinazoambatanishwa na kazi hii, ni hisia tu za wahusika, kwani kwanza hazina ushahidi, na pia usaili ulifanywa kufuatana na kanuni na sheria zinazosimamia ajira za watumishi wa umma,” ilieleza taarifa hiyo ya Nantanga, kuhusu usaili wa watu zaidi ya 10,000.

Saturday, July 26, 2014

Mchakato wa ujenzi ‘flyover’ Tazara waanza


Dar es Salaam. Tatizo la foleni katika jiji la Dar es Salaam, limeanza kupatiwa dawa baada ya Serikali ya Tanzania na Japan kutiliana saini mkataba wa ujenzi wa barabara za juu (flyover) katika makutano ya Barabara ya Mandela na Nyerere.
Akizungumza baada ya kutiliana saini, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk Servacius Likwelile alisema Japan imeiongezea Tanzania Sh5.64 bilioni, baada ya kiasi cha Sh52.55 bilioni kilichotolewa Juni 18, 2013 kutofikia kiwango kinachotakiwa na makandarasi kwa ajili ya ujenzi wa njia hiyo ya juu.
Sambamba na mradi huo, pia nchi hizo zimetiliana saini mkataba mwingine wa kuboresha usambazaji wa umeme katika jiji la Dar es Salaam kwa kujenga vituo vidogo katika maeneo ya Mwananyamala, Muhimbili na Jangwani Beach.
Miradi hiyo itakayogharimu jumla ya Sh77.5 bilioni na inafadhiliwa na Serikali ya Japan, chini ya Shirika la Maendeleo la Japan (Jica).
“Kama mnavyojua, barabara na nishati ndiyo nguzo katika ukuaji wa uchumi. Msaada huu utatuwezesha kuongeza kasi katika kuimarisha uwekezaji katika sekta ya hizi. Pia, zitachochea maendeleo katika maeneo mengine,” alisema na kuongeza kuwa kiasi kingine cha Sh71.9 bilioni kimetolewa kwa ajili ya kusaidia usambazaji wa umeme jijini Dar es Salaam ili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza na kukwamisha shughuli mbalimbali za uzalishaji.
Kuhusu barabara hiyo, Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada alisema Serikali yake imeongeza fedha ili kukabiliana na upungufu wa bajeti uliosababishwa na kushuka kwa thamani ya fedha pamoja na ongezeko la bei ya vifaa vya ujenzi.
Alisema mkataba na mkandarasi unatazamiwa kutiwa saini Septemba mwaka huu na ujenzi wa barabara hiyo utaanza muda mfupi baadaye.
Mwakilishi Jica nchini, Yasunori Onishi alisema sekta ya usafirishaji ni moja ya shughuli kubwa wanazozifanya nchini ili kuleta maendeleo.
Alisema shirika lake limekuwa likitekeleza miradi mbalimbali ya kupunguza msongamano katika Jiji la Dar es Salaam kwa miaka 30 sasa, ikiwamo ujenzi wa Daraja la Salenda ulioanza mwaka 1980. “Jica pia tulisaidia kuundwa kwa mpango mkuu wa sera na mfumo wa usafirishaji katika jiji la Dar es Salaam mwaka 2007 na 2008. Hata hivyo, katika utafiti wetu, tulipendekeza kipaumbele kielekezwe katika makutano ya Tazara,” alisema Onishi.
Alisema mradi wa ujenzi wa barabara ya juu eneo hilo la Tazara, unatarajiwa kuwanufaisha zaidi ya watu milioni mbili wanaofanya safari zao kila siku kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwenda katikati ya jiji. Pia alisema barabara hiyo itapunguza kwa asilimia 30, muda unaotumika kusafiri katika umbali huo kutoka dakika 37 hadi dakika 25.
“Tumejipanga kikamilifu kutekeleza maazimio tuliyosaini leo. Naiomba Serikali pia itimize wajibu wake katika kuhakikisha kuwa fedha zilizotolewa zinatumika katika mambo yaliyokusudiwa,” alisema.
Onishi alisema Jica ina dhamira ya dhati kuisaidia Serikali ikiwamo upanuzi wa Barabara ya Bagamoyo (Mwenge - Tegeta) ambayo ujenzi wake utakamilika mwisho wa mwezi huu.lisema kipande kingine cha Morocco – Mwenge bado kinafanyiwa usanifu na ujenzi wake utafanyika katika awamu ya pili inayotarajiwa kuanza Septemba mwaka huu

Serikali yaifunga Hospitali ya IMTU


Dar es Salaam. Serikali imeifungia Hospitali ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU), baada ya kuifanyia ukaguzi na kubaini kasoro kadhaa za uendeshaji wake.
Ukaguzi huo ulifanywa jana na jopo la wataalamu kutoka Manispaa ya Kinondoni, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, baada ya IMTU kukumbwa na kashfa ya utupaji wa mabaki ya viungo vya binadamu katika Bonde la Mto Mpiji, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Ukaguzi huo ulifanywa jana na jopo la wataalamu kutoka Manispaa ya Kinondoni, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, baada ya IMTU kukumbwa na kashfa ya utupaji wa mabaki ya viungo vya binadamu katika Bonde la Mto Mpiji, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Hospitali hiyo imefungiwa wakati Kamati ya Watu 15, iliyoundwa na Serikali ikiendelea kuchunguza kashfa hiyo.
Hata hivyo, wakati taarifa za kufungiwa zikitolewa habari za ndani zinaonyesha kuwa hapakuwa na mgonjwa yeyote hospitalini hapo, ikielezwa kuwa wagonjwa wote waliondoka baada ya kuibuka kwa kashfa ya viungo IMTU ikihusishwa.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dk Bunini Kamba alisema kuwa wameamua kuifungia hospitali hiyo kwa muda usiojulikana, baada ya kukuta upungufu mbalimbali katika maeneo ya kutolea huduma, jambo linalohatarisha usalama wa wagonjwa.
“Maabara tumekuta dawa ambazo muda wake wa kutumika umepita na hazikuwa katika mpangilio maalumu. Wodini hakuna usimamizi maalumu, hasa kwa wagonjwa wenye majeraha,” alisema Dk Bunini.
Aliongeza: “Hakuna wauguzi wa kutosha na mashine ya kuchoma taka ngumu haifanyi kazi vilivyo. Tumeona kuwa hospitali hii haistahili kuendelea kutoa huduma kwa jamii.”
Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Profesa Yasin Mgonda alisema: “Tumesikia uamuzi huo uliotolewa baada ya kufanyika ukaguzi. Tutajirekebisha na tutakapokamilisha tutawaita kuja kutukagua tena.”
Alisema kuwa pamoja na sababu nyingine, hospitali yake imefungiwa baada ya kubainika kuwa bomba la maabara limeharibika na halitoi maji.
Nyingine ni kutojaza vitabu vya wagonjwa kwa mujibu wa taratibu za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, pia duka lake la dawa kuwa halijasajiliwa lakini akasema sababu hiyo imewashangaza kwani wanachojua wao duka hilo limesajiliwa.
Kwa upande wake, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Primus Saidia aliliambia gazeti hili kwamba anaipongeza Serikali kwa uamuzi huo akisema utanusuru maisha ya wananchi waliokuwa wakipata huduma hospitalini hapo.
“Tunaipongeza Serikali, ila tunaiomba iwatafutie wanafunzi wa chuo hicho maeneo mengine ya kujifunzia,” alisema Dk Saidia.
Juzi, Dk Saidia alisema kuwa wote waliohusika na kashfa ya utupaji mabaki ya viungo vya binadamu wanastahili kuchukuliwa hatua kali kwa sababu kitendo hicho kimekiuka sheria, taratibu, haki za binadamu, maadili ya ufundishaji na taaluma ya udaktari.
“Kama ni taasisi ya utafiti imepoteza sifa ya kufanya utafiti na kama ni ya mafunzo basi imepoteza sifa ya kutoa mafunzo ya tiba. Kama ni hospitali itakuwa imepoteza sifa za kutoa tiba kwa binadamu,” alisema Dk Saidia.
Naye spika wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho (IMTUSO), William Mapunga alisema kuwa kufungiwa kwa hospitali hiyo kutawaathiri, kwani watakosa sehemu ya kwenda kufanya mafunzo kwa vitendo, akiiomba Serikali kuliangalia suala hilo kwa mapana.

Thursday, July 24, 2014

MAKALA: Tiba, kinga ya Ukimwi vyanukia

Watafiti katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Temple, Marekani wamegundua dawa ya kuangamiza Virusi Vya Ukimwi (VVU) ambayo ni ya uhakika zaidi ukilinganisha na zilizowahi kupatikana katika tafiti za awali duniani.
Dawa yao inaweza kutumika kwa tiba ya wanaoishi na VVU na kinga kwa wale ambao bado hawajaambukizwa.
Mmoja wa watafiti hao, Dk Kamel Khalili aliwaambia waandishi wa habari juzi mjini Philadelphia, Marekani kuwa tofauti na utafiti mwingine, wao wamegundua namna ya kukiondoa kirusi kilichoingia kwenye kinasaba (DNA) ndani ya CD4 na kukitoa nje na hatimaye kukiua.
Alisema dawa hiyo inafanya kazi hiyo bila kuathiri seli za mwili wa binadamu.
Dk Khalili alisema ugunduzi wao ni wa hali ya juu zaidi kwa sababu teknolojia ya kutengeneza dawa hiyo ni tofauti na nyingine zilizokwisha kugunduliwa ambazo hazina uwezo wa kupenya ndani ya seli za binadamu, bali kuathiri tu VVU vilivyopo nje yake, ndani ya mfumo wa damu.
“Dawa yetu inakivuta kirusi nje ya seli (CD4) bila kuiathiri seli yenyewe na kukiua. Hivyo dawa hii itatumika kwa muda fulani na kuua virusi vyote mwilini na hakuna haja ya kuitumia wakati wote kama ilivyo dawa ya kufubaza VVU (ARV).”
ARV huangamiza VVU vilivyopo kwenye damu na kuendelea kuviacha hai vile ambavyo tayari vimeingia ndani ya CD4, hivyo kufanya virusi kuzuka upya pindi mwathirika anapoacha kutumia dawa.
Mmoja wa wataalamu katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Kituo cha Mbeya (NIMR-MMRC), Clifford Majani ameuelezea utafiti huo kama mwanga mpya katika teknolojia ya kukabili VVU.
“Kama imepatikana teknolojia ya kukiondoa kirusi ndani ya seli ni hatua nzuri ya kukabili VVU. Hili lilionekana kuwa gumu mwanzoni,” alisema Majani.
Alisema imekuwa vigumu kuua kirusi kikiwa ndani ya seli na hata baadhi ya wanasayansi wamejaribu kutengeneza dawa itakayotambua seli zilizoathirika ili ziuawe lakini hilo likawa gumu.
“Inaweza ikapatikana dawa ya namna hiyo (inayoua seli zilizoathirika) lakini ikawa inaathiri vitu vingine ndani ya mwili. Hilo halikubaliki. Kikubwa katika ugunduzi huo ni dawa kuweza kukifuata kirusi kinakojificha na kukiondoa, jambo ambalo dawa nyingi zimeshindwa zikiwamo ARV,” alisema.
Hata hivyo, Majani alisema changamoto ambayo inaweza kujitokeza katika majaribio ya dawa hiyo ni usalama wakati wa matumizi.
“Lazima dawa hiyo ichunguzwe isije ikawa inaathiri viungo vingine pamoja na utendaji wa mwili kwa ujumla. Maana hapo ndipo dawa nyingi zinaposhindwa… Tusubiri tuone hii inaweza kuwa na matumaini zaidi,” alisema Majani.
Mkutano wa Ukimwi
Ugunduzi huo umekuja wakati wanasayansi, waunda sera na wadau wa mapambano ya VVU wakiwa wanatoa kauli za kukata tamaa kwenye mkutano wa Ukimwi unaomalizika kesho huko Melbourne, Australia.
Wanasayansi kadhaa wanaotoka kwenye taasisi kubwa za utafiti za VVU wameweka wazi kuwa tafiti nyingi zilizokuwa na matumaini zimeshindwa kufanya kazi kwa asilimia 100 baada ya dawa zake kufanyiwa majaribio kwa sababu dawa zake zinapotumika, vipimo huonyesha wamepona lakini baada ya muda VVU hurejea upya.
“Kinachoonekana ni kwamba virusi hivi hujificha sehemu fulani ya mwili ili visiathirike na kusubiri mtu aache dawa ili virejee upya kushambulia CD4,” alisema Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya wa Magonjwa ya Kuambukiza na Kinga ya Peter Doherty ya Australia, Profesa Sharon Lewin.
Dawa mpya inavyofanya kazi
Dk Khalili alisema wametengeneza dawa yao kwa protini maalumu ambayo inakata sehemu ya seli iliyoshambuliwa na kirusi cha Ukimwi na kukivuta nje.
Baada ya kukivuta, dawa huachana na seli hiyo na kuiacha ikijitibu yenyewe na kupona kabisa kiasi cha kuendelea na kazi zake za kinga mwilini mwa binadamu bila tatizo.
VVU kwa kawaida hushambulia seli kinga aina ya CD4 na kuzifanya kama kiwanda cha kuzalishia virusi vingine.
Kwa kawaida seli ikishaingiliwa na kirusi, huacha kazi yake ya kinga ya mwili na badala yake kuchukua jukumu la kutengeneza VVU.
“Dawa yetu inafanya kazi kwa haraka, kwa makini na bila kuathiri seli,” alijigamba Dk Khalili.
Alisema tayari imefanyiwa majaribio maabara na kuonekana inafanya kazi vizuri na sasa wamehamishia majaribio kwa wanyama.Sha

Katika maabara, alisema dawa hiyo ilifanyiwa majaribio kwa damu ya binadamu na ikaonyesha kufanya kazi kwa asilimia 100.
Dk Khalili anaamini kwamba majaribio hayo yatawachukua miaka michache... “Lakini tunaamini ni mfumo ambao utaweza kufanya kazi vizuri kwa binadamu.”
Alisema wanachofanya sasa ni kuangalia mfumo ambao utakuwa mzuri zaidi kwa ajili ya tiba ya binadamu.
Kwa namna teknolojia ya dawa hiyo ilivyo, alisema wanaweza kuitumia kwa ajili ya kuwatibu wale ambao tayari wameambukizwa na hata kuwakinga wale ambao siyo waathirika.
Uzuri wa dawa hiyo, pia alisema inaweza kutumiwa na mtu ambaye anatumia ARV pasipo kuingiliana kiutendaji.
Ugunduzi wao ulichapishwa kwenye Jarida la Taifa la Elimu ya Sayansi la National Academy of Science la Marekani na kuonekana kuvuta hisia za wengi.
Hali ya Ukimwi duniani
Akizungumza kwenye mkutano wa Melbourne, Profesa Lewin alisema tafiti za sasa zinaonyesha kuwa karibu watu milioni 14 duniani wanaishi na VVU.
Alisema mamilioni ya watu hao wamekuwa wakisaidiwa kwa kutumia ARV, wakati huu ambao bado hakuna kinga wala tiba, inayoaminika.
Alisema ingawa tafiti nyingi hazijaonyesha matumaini waliotarajia ya kupata kinga na chanjo, bado juhudi zinaendelea ili kuhakikisha wanafikia mahali HIV inakuwa haina nafasi katika mwili wa mwanadamu.
Alisema pamoja na matokeo hasi ambayo yamejitokeza kwenye tafiti nyingi, bado anaamini kwamba ipo siku chanjo na tiba vitapatikana.
Wanasayansi waliohudhuria mkutano huo waliitaka dunia isiogope kutokana na kushindwa kwa baadhi ya tafiti kama ilivyokuwa kwa mtoto wa Jimbo la Mississippi, nchini Marekani ambaye alitangazwa amepona na baadaye virusi vikaibuka upya.
Ndege ya shirika la Algeria iliyokuwa imebeba abiria 116 ambayo awali iliripotiwa kuwa imepoteza mawasiliano kwa zaidi ya dakika 50 imethibitishwa kuwa imeanguka.

Kwa mujibu wa Aljazeera, maafisa wa Algeria wamethibitisha kuwa ndege hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka Burkina Faso kwenda katika mji mkuu wa Algeria, Algiers imeanguka Kusini mwa Mali.

Maafisa wa serikali ya Ufaransa wameeleza kuwa ndege hiyo AH5017 ilipotea kwenye radar katika eneo la Mali baada ya mvua kubwa kunyesha na inaelezwa kuwa vipande vya ndege hiyo vimeanza kuonekana baharini.

Ndege hiyo inayomilikiwa na kampuni binafsi ya Hispania inayofahamika kama Swiftair ilikuwa imebeba abiria 110 na wafanyakazi sita.

Wednesday, July 23, 2014

KIJANA "ANG'OLEWA" MENO 232

Salim Kikeke's photo.

Madaktari nchini India wametoa meno 232 kutoka katika mdomo wa kijana mwenye umri wa miaka 17, katika upasuaji uliochukua saa saba.
Kijana huyo Ashik Gavai alifikishwa hospitali akiwa amevimba na maumivu kwenye taya na shavu lake la upande wa kulia, amesema Dokta Sunada Dhiware, mkuu wa idara ya meno katika hospitali ya JJ jijini Mumbai.
Kijana huyo amekuwa akisumbuliwa kwa miezi 18, na alilazimika kusafiri kwenda mjini, baada ya madaktari katika kijiji chake kushindwa kufahamu chanzo cha tatizo.
Madaktari wameelezea hali hiyo kuwa "ni haba sana" kutokea na ni jambo ambalo "limevunja rekodi ya dunia".
Upasuaji huo uliofanyika siku ya Jumatatu, ulihusisha madaktari wawili na wasaidizi wawili.
Ashik sasa ana meno 28.
"Ashik aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa aina yake ambao ufizi mmoja huunda meno mengi. Ni kama aina ya uvimbe wa saratani," amesema Dokta Dhiware.
"Mwanzoni, hatukuweza kukata fizi, kwa hiyo tulilazimika kutumia nyundo na tindo kufanikisha.
"Tulivyopasua tu, meno madogo madogo yakaanza kutoka, moja baada ya jingine, na tulipoyahesabu, yalifika meno 232." Amesema daktari huyo.


Tuesday, July 22, 2014

MAKALA; Teknolojia Jinsi waongoza ndege wanavyopatikana

Wiki iliyopita Mkufunzi Mwandamizi wa usimamizi wa ndege kutoka Chuo cha Mafunzo ya Usafiri wa Anga (CATC), Shadrack Kalinga alifafanua namna ndege inavyoongozwa kuanzia kupaa mpaka kutua katika kiwanja kingine.
Leo atafafanua jinsi mchakato wa kuwapata waongoza ndege na mafunzo wanayopitia mpaka kufuzu kuifanya kazi hiyo.
Kama zilivyo kada nyingine za sayansi, waongoza ndege wanapitia mafunzo ya kina ya nadharia na vitendo katika vyuo vya usafiri wa anga.
“Kwa kawaida mafunzo ya uongozaji ndege huchukua wiki 20: kumi ni mafunzo ya nadharia na 10 nyingine katika vitendo kupitia mashine maalumu (simulators).
“Hata hivyo, hapa nchini mara nyingi wiki hizo huwa zinazidi kwa sababu kuna miezi mitatu katikati ya kwenda kwenye mafunzo ya vitendo katika viwanja vikuu vya ndege nchini,” anasema Kalinga.
Kuhusu kiwango cha ufaulu kinachotakiwa, Mkuu wa Chuo hicho Margareth Kyarwenda anasema unahitajika ufaulu wa hali ya juu wa mosomo ya sayansi na hesabu.
“Ili uweze kusoma kozi za usafiri wa anga unatakiwa uwe umafaulu vizuri sana masomo sayansi na hesabu hali kadhalika Kiingereza na Jiografia kidato cha nne na cha sita. Pia kama umemaliza shahada basi uwe umesoma masomo ya uhandisi na kufaulu vizuri,” anaeleza Kyarwenda.
Anabainisha kuwa mwanafunzi anapoanza masomo hayo huanza upya na shahada yake ya awali haichukuliwi kama mwendelezo wa masomo--uzamili au Stashahada.
Mashine maalumu za kufundishia uongozaji ndege
Katika kujifunza uongozaji ndege, wanafunzi wanahitaji wapitie nadharia pamoja na vitendo.
Katika vitendo hupewa mazoezi namna ya kuziongoza ndege kupitia mitambo ya ‘simulator’ yenye uwezo wa kutengeneza hali za hewa za namna mbalimbali.
Mitambo hii inajumuisha mfumo wa skrini zilizofungwa kwa kubananishwa kwa muundo wa duara ili kutoa muono endelevu kutoka ya kwanza hadi ya mwisho. Mfumo huo wa duara hupimwa kwa kipimo cha nyuzi kati ya 280 au zozote ndani ya 360.
Mitambo huongozwa na mfumo wa kompyuta (operating system) na kuunganishwa mashine za kuongezea ambazo huwekwa kutokana na idadi watu wanaohitajika katika chumba husika.
Mwanafunzi aliyepo kwenye zamu ya mafunzo hayo hukaa katikati na wengine kumsaidia kwenye mitambo mingine ya mbele.
“Humu ndani kuna programu ambazo zinaweza kutengeneza uwanja wa ndege. ghushi wa mahali popote ulimwenguni na pia kuweka hali za hewa kama mawingu, mvua, jua kali, ukungu na mengine mengi,” anasema Kalinga.
Kwa mujibu wa Kyarwenda mtambo mpya waliofunga katika chuo hicho cha CATC kinachomilikiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) unagharimu takriban Sh1.5 bilioni na ni wa kisasa zaidi.
Kalinga pia naongeza kuwa chumba cha ‘simulator’ katika chuo chao kinabeba wanafunzi wanane na kila mmoja anatakiwa afanye mafunzo kwa vitendo kwa jumla ya saa nane—saa moja kila siku.
Anabainisha baada ya kumaliza mafunzo hayo mwanafunzi huyo anaenda kufanya tena mazoezi kwa vitendo miezi mitatu kwa kuongoza ndege moja kwa moja.
“Baada ya hapo wanamfanyia tathmini na akifaulu anapelekwa katika bodi ya uamuzi ya (TCAA) ambapo anafanyiwa usaili kwa mahojiano.
“Ukipita hapo sasa ndiyo unapewa leseni na kwenda kuanza kuongoza ndege huku ukisimamiwa,” anasema Kalinga.
Mkufunzi huyo anasema baada ya kuangaliwa kwa muda, mwanafunzi huyo anajaza ‘log book’ ambayo itamfanya awe amehitimu na kuanza kazi kama mwongozaji.

SHAMBULIO KATIKA KIKOSI CHA RAIS DRC

Shambulio katika kambi ya jeshi ya kikosi cha kumlinda rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo limezuiwa, kwa mujibu wa maafisa wa serikali.
Hali imerejea kuwa ya utulivu na kundi dogo la "waliojipenyeza" limezidiwa nguvu, imesema serikali ya Kinshasa.
Milio mizito ya bunduki ilisikika katika kambi ya Tshatshi, kwa karibu dakika 30.
Mamlaka hazijasema nani amehusika na shambulio hilo.
Wakazi wa eneo hilo walihamishwa, na uwanja wa ndege wa kimataifa kufungwa.
Mlinzi mmoja wa kikosi cha rais ameliambia shirika la habari la AFP kuwa watu 20 waliokuwa na mavazi ya kiraia wamezidiwa nguvu.
Mwanajeshi mwingine ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa washambuliaji wanne wameuawa.
Shambulio katika kambi ya Tshatshi mwezi Disemba mwaka jana pia lilidhibitiwa.

Wakuu wa mikoa tanzania wapashwa

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, amewataka Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala nchini, kuheshimiana.
Pia, amewataka watambue kuwa wote ni wateule wa Rais, hivyo wanatakiwa wawe na uhusiano na mawasiliano mazuri ili kuwatumikia kwa ufanisi wananchi.
Balozi Iddi alisema hayo Dar es Salaam jana wakati akifungua mkutano wa mafunzo ya siku tatu ya uongozi kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa.
Mafunzo hayo yameandaliwa na kufadhiliwa na Taasisi ya Uongozi. Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, alisema kumekuwa na changamoto ya uhusiano na muingiliano wa kiutendaji miongoni mwa wakuu hao wa mikoa na makatibu tawala.
Alisema hali hiyo imesababisha baadhi yao, kuamua vile wanavyoona na wengine kuwasilisha malalamiko kwa viongozi wakuu.
“Nyinyi ni viongozi mliokabidhiwa dhamana kubwa katika mikoa yenu, lakini pia nyie ndio wawakilishi wa Mheshimiwa Rais katika hiyo mikoa yenu, uwajibikaji na mshikamano ndio sababu pekee itakayowezesha watanzania kutimiza wajibu wao wa kuboresha maisha yao,” alisisitiza.
Alisema maendeleo katika mikoa hiyo, kamwe haitawezekana endapo viongozi hao wa juu wa mikoa, hawatakuwa wawazi katika mawasiliano baina yao, uhusiano wao kikazi ukiwa mbaya na kukiwa na kutokuelewana.
“Mawasiliano ya katibu tawala kwenda kwa mkuu wa mkoa ni ushauri, maelezo, ufafanuzi na taarifa muhimu, wakati mawasiliano ya mkuu wa mkoa kwenda kwa katibu tawala zaidi ni maelekezo ya kisera na uwajibikaji,” alisema.
Alisema kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003, katibu tawala wa mkoa husaini na mkuu wa mkoa mkataba wa utendaji kazi, ambapo katika tathmini ya mwaka, suala la uhusiano wao ni miongoni mwa vipimo vilivyomo kwenye tathmini hiyo.
Aliwataka viongozi hao, kuepuka misuguano baina yao, ambayo huenda ikaigwa na ngazi za chini na kusababisha utendaji katika mkoa mzima kuwa mbaya na hivyo kuurudisha nyuma mkoa husika.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia, alisema Serikali siku zote imekuwa ikisisitizia viongozi wake kuthamini na kuheshimiana, lakini kubwa zaidi kuhakikisha kuwa hawaingiliani katika utendaji wao.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Joseph Semboja, alisema mafunzo hayo yamelenga katika kuwakumbusha viongozi hao juu ya umuhimu wa kuzingatia suala la mawasiliano, kuepuka kuingiliana katika utendaji na kuwa na uhusiano mzuri baina yao katika kuwatumikia wananchi.
“Tumeanza na wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa wa Tanzania Bara, tutafanya pia mafunzo kwa viongozi kama hao Zanzibar na kushuka hadi ngazi za chini kuanzia wakuu wa wilaya na watendaji, lengo ni kuimarisha mazingira mazuri ya utendaji baina yao,” alisema.

Bei ya mafuta kushuka

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeanza mchakato wa kutafuta namna ya kupunguza gharama za uingizaji wa mafuta nchini. Hatua hiyo itawezesha pia bei ya nishati hiyo nchini kushuka.
Chini ya mchakato huo, Ewura inataka kushusha gharama za uagizaji wa mafuta, kwa kuchagiza ushindani wa upatikanaji wa mitaji ya fedha za uagizaji nishati hiyo.
Inataka katika ushindanishaji wa watoaji wa fedha ambao ni benki, hatimaye kuwe na ulinganifu wa upatikanaji fedha hizo miongoni mwa kampuni za mafuta.
Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi alisema jijini Dar es Salaam jana, baada ya kufanikiwa katika utaratibu wa uingizaji mafuta wa pamoja, sasa wameamua kukutana na wadau kujadili namna ya kushusha zaidi gharama za nishati hiyo muhimu.
Mkutano huo wa wadau ulikutanisha washiriki mbalimbali, ikiwemo Benki Kuu (BoT), kampuni za mafuta, benki za biashara.
Ngamlagosi alisema uingizaji wa pamoja wa mafuta, umesaidia kuokoa muda na gharama kubwa za fedha zilizokuwa zikilipwa kutokana na meli kukaa muda mrefu. Mjadala huo umelenga mambo mawili makuu, yatakayowezesha kushuka kwa nishati hiyo.
Ushindani wa benki
Mkurugenzi huyo mkuu wa Ewura alisema kwanza wanaangalia namna ya kuweka ushindani wa benki katika ulipaji wa huduma za mikopo ya kampuni, ambazo zinaingia mkataba kwa ajili ya ununuzi wa mafuta.
“Kwa mfano, kwa sasa ni asilimia moja ambayo inalipwa na mlaji, lakini bado tunataka tuangalie iweze kushuka zaidi ya hapa. Kwa mfano nchi ya Msumbiji, kampuni zinalipa kati ya asilimia 0.3 mpaka 0.4 kwa hiyo na sisi tufike huko,” alisema Ngamlagosi.
Alisema jambo lingine ni kurekebisha barua za benki kwa ajili ya kuruhusu upakuaji wa mafuta. Alisema katika uagizaji wa pamoja wa mafuta, meli moja inakuwa na mafuta ya kampuni nne au tano na ikitokea mmoja akashindwa kuwasilisha barua husika, hukwamisha ushushaji wa mafuta.
“Hapa ikitokea mmoja akashindwa kuleta ‘letter of credit’ (barua) kutokana na kushindwa kuelewana na benki, anakwamisha mzigo wa watu wote, kwa hiyo hata hii tutaangalia namna ya kurekebisha,” alisema.
Mafuta bei chini
Kwa mujibu wake, kwa sasa suala hili wamelileta kwa ajili ya majadiliano na kupata mawazo ya wadau wa sekta hiyo. Mpango huo utakapofanikiwa, utatoa unafuu kwa mtumiaji wa mwisho ambaye ni mlaji.
Aidha, utaratibu wa uingizaji wa mafuta kwa pamoja umebainika kupunguza gharama kubwa na hivyo kuwa nafuu kwa walaji na uchumi wa nchi. Taarifa ya mamlaka inasema utaratibu huo umeokoa takribani Sh bilioni 126 ambazo hutumika.
“Hata gharama zimepungua sana. Zamani meli moja ilikuwa inakaa karibu siku 40 hadi 60 na kwa siku zinakaa meli tano mpaka sita, ambazo zote ilikuwa lazima uzilipie dola za Marekani 20,000 kwa hiyo ilikuwa gharama kubwa sana,” alisema.
Utafiti UDSM
Alisema manufaa hayo yaligunduliwa baada ya utafiti ulioafanywa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Idara ya Uchumi. Alisisitiza kwamba utaratibu huo umekuwa na manufaa.
Alisema ni muhimu kuangalia njia nyingine za kushusha gharama zaidi. Kampuni zakubali Mmoja wa wadau aliyehudhuria mkutano huo kutoka Kampuni ya Petroleum Importation Coordinator Ltd, Raymond Lusekelo, alisema mipango hiyo ya kushusha gharama zaidi ni mizuri, ikiwa itatekelezwa ipasavyo.
Lusekelo, ambaye ni Meneja Mipango wa kampuni hiyo, alisema anaamini hata wafanyabiashara wengine wa nishati hiyo, hawana tatizo na mpango huo, ambao unaonekana utaleta nafuu zaidi kwa watumiaji wa mwisho wa mafuta.
Mkurugenzi Mkuu wa Ewura alisema Agosti 4 mwaka huu, itakuwa mwisho wa kupokea maoni kutoka kwa wadau, kueleza ni kwa namna gharama zishuke.
Baada ya kufunga mchakato wa kupokea maoni, watapanga tena siku ya kukutana na wadau wa karibu hususani kampuni za mafuta. Baada ya hapo, Ewura itaeleza mapendekezo juu ya maoni yaliyokusanywa.


Saturday, July 19, 2014

WAASI WATUHUMIWA "KUHARUBU USHAHIDI"

Ukraine imetuhumu waasi wanaoiunga mkono Urusi kwa kujaribu kuharibu ushahidi wa "uhalifu wa kimataifa" katika eneo ndege ya Malaysia ilipoanguka.
Serikali imesema waasi wakiongozwa na Urusi wanazuia wawakikishi wa kimataifa na wataalam wake kuzuia uchunguzi.
Inaaminika ndege hiyo namba MH17 ilianguka baada ya kudunguliwa na kombora, katika eneo linalodhibitiwa na waasi mashariki mwa Ukraine siku ya Alhamisi.
Watu wote 298 waliokuwemo ndani walipoteza maisha.
Ndege hiyo aina ya Boeing 777 ilikuwa ikisafiri kutoka Amsterdam kwenda Kuala Lumpur. Ilianguka kati ya Krasni Luch katika eneo la Lihansk na Shakhtarsk karibu na Donetsk.
Katika taarifa yake, serikali ya Ukraine imelalamika kwa kusema "magaidi" wamechukua miili 38 na kuipeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti katika eneo linalodhibitiwa na waasi katika jiji la Donetsk. Imesema pia waasi wanajaribu kusafirisha mabaki ya ndege kwenda Urusi.


Salim Kikeke's photo.Salim Kikeke's photo.

Alshabaab lashambulia tena eneo la lamu huko kenya.


Friday, July 18, 2014

MAMIA WAHOFIWA KUFA DAMBOA- NIGERIA

MAMIA WAHOFIWA KUFA DAMBOA- NIGERIA
Watu wengi wanahofiwa kufa baada ya watu wanaodhaniwa kuwa wanamgambo wa Boko Haram kushambulia mji wa Damboa, kaskazini mashariki mwa Nigeria. Watu walioshuhudia wameiambia BBC kuwa nusu ya mji huo umeteketezwa kwa moto, likiwemo soko kuu. Mkazi mmoja amesema mashambulio hayo yalifanywa siku ya Alhamis usiku na kuendelea hadi saa za alfajiri. Mji wa Damboa uliopo kilomita 85 kutoka mji mkuu wa jimbo la Borno, Maiduguri sasa hauna watu kutokana na wenyeji kukimbia ghasia hizo. Boko Haram ilishambulia kambi za jeshi mjini humo wiki mbili zilizopita na kuua wanajeshi kadhaa. Wizara ya ulinzi ya Nigeria imesema jeshi lilizuia shambulio hilo na kuua wanamgambo 50. Hata hivyo wakazi wanasema mji huo sasa unalindwa na makundi ya sungusungu.
Boko Haram wakati mwingine wameonekana kuwa na silaha nzito kuliko hata majeshi ya serikali.
Watu wengi wanahofiwa kufa baada ya watu wanaodhaniwa kuwa wanamgambo wa Boko Haram kushambulia mji wa Damboa, kaskazini mashariki mwa Nigeria. Watu walioshuhudia wameiambia BBC kuwa nusu ya mji huo umeteketezwa kwa moto, likiwemo soko kuu. Mkazi mmoja amesema mashambulio hayo yalifanywa siku ya Alhamis usiku na kuendelea hadi saa za alfajiri. Mji wa Damboa uliopo kilomita 85 kutoka mji mkuu wa jimbo la Borno, Maiduguri sasa hauna watu kutokana na wenyeji kukimbia ghasia hizo. Boko Haram ilishambulia kambi za jeshi mjini humo wiki mbili zilizopita na kuua wanajeshi kadhaa. Wizara ya ulinzi ya Nigeria imesema jeshi lilizuia shambulio hilo na kuua wanamgambo 50. Hata hivyo wakazi wanasema mji huo sasa unalindwa na makundi ya sungusungu.
Boko Haram wakati mwingine wameonekana kuwa na silaha nzito kuliko hata majeshi ya serikali.


Ndege yatua barabarani Uganda

  Ndege hiyo N604AR, iliyokuwa imewabeba wanajeshi wa Marekani, ilitua katika eneo la Kiwawu umbali wa kilomita 22 kutoka wilaya ya Mityana.
 Ndege hii ilikuwa inaelekea mjini Juba Sudan Kusini
Shughuli ziliathirika leo wilayani Mityana baada ya ndege kutua kwa dharura katika barabara ya magari ya Mityana.
Kwa mujibu wa mtandao wa Nation, kamishna wa wilaya Joel Walusimbi, alithibitisha tukio hilo akisema rubani wa ndege hiyo alilazimika kutua katikati ya barabara
Polisi walisema kuwa ndege hiyo ilikuwa inaelekea mjini Juba Sudan Kusini kutoka uwanja wa ndege wa Entebbe.

17 mahakani kwa ugaid


Watumiwa wa ugaid wakiwa jini ya ulizi mkali wa askiri wakifiksha mahamani
WATU 17 wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka ya kujihusisha na vitendo vya ugaidi.
Washitakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo jana saa 7:30 mchana wakiwa chini ya ulinzi mkali.
Kulikuwa na magari mawili ya jeshi la Magereza, magari mawili yaliyokuwa na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na manne yaliyokuwa na askari zaidi ya 15 wenye silaha waliovaa nguo za kiraia.
Walisomewa mashitaka na Mawakili wa Serikali, Prosper Mwangamila, Mwanaamina Kombakono, George Barasa na Brenda Nicky mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa.
Wakili Barasa alidai katika tarehe tofauti nchini kati ya Januari mwaka jana na Juni mwaka huu, washitakiwa 16 walipanga njama za kutenda kosa la kuingiza watu nchini kwa ajili ya kufanya vitendo vya ugaidi.
Alidai katika kipindi hicho, washitakiwa walikubali kuwaingiza nchini Sadick Absaloum na Farah Omary kwa ajili ya kujihusisha na vitendo vya ugaidi.
Katika mashitaka yanayomkabili mkazi wa Kitunda, Jihad Swalehe, Wakili Nicky alidai kati ya Machi 21 mwaka jana na Juni 2 mwaka huu, Dar es Salaam, pamoja na wenzake ambao hawajafikishwa mahakamani, walipanga njama za kuwaingiza watu kwa ajili ya kufanya vitendo vya kigaidi.
Kwa mujibu wa Wakili Nicky, katika kipindi hicho, Dar es Salaam, kwa kutumia mawasiliano ya mtandao wa kijamii wa facebook, Swalehe aliwasiliana na Nero Saraiva na watu wengine akiomba malighafi, fedha na ujuzi kwa ajili ya kuweka mabomu.
Ilidaiwa aliomba ujuzi huo ili aweke mabomu nchini Kenya kwa lengo la kusababisha hofu, majeraha na vifo kwa wananchi wa nchi hiyo.
Mbali na Swalehe, washitakiwa wengine ambao ni wakazi wa Zanzibar na Dar es Salaam ni Nassoro Abdallah, Hassan Suleiman, Anthari Ahmed, Mohamed Yusuph, Abdallah Hassan, Hussein Ally, Juma Juma, Said Ally, Hamis Salum, Said Salum, Abubakari Mngodo, Salum Salum, Salum Amour, Alawi Amir, Rashid Nyange na Amir Juma.
Washitakiwa hao hawakuruhusiwa kujibu mashitaka kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu.
Wakili Mwangamila alidai upelelezi wa kesi hizo haujakamilika na kuomba kesi inayowakabili watu 16 itajwe Julai 23 mwaka huu kwa kuwa wanatarajia kuwasilisha ombi maalumu.
Hakimu Riwa aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 23 mwaka huu itakapotajwa. Kwa upande wa kesi inayomkabili Swalehe, itatajwa Julai 31 mwaka huu. Washitakiwa wote walirudishwa rumande kwa kuwa mashitaka yanayowakabili hayana dhamana.
Taarifa za siri
Awali katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba alisema taarifa za siri kutoka kwa raia wema zimefanikisha kukamata watu 16 wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vinavyoashiria ugaidi ikiwemo, umwagiaji watu tindikali katika maeneo mbalimbali nchini.
Alisema watuhumiwa wanadaiwa kujihusisha na uandaaji wa vijana na kuwawezesha katika nyanja mbalimbali ikiwemo kifedha, wafanye vitendo vya uhalifu wa kitaifa na kimataifa.
Kwa mujibu wa msemaji huyo wa polisi, watu hao walikamatwa katika maeneo mbalimbali ya Tanzania Zanzibar na Bara.
“Katika jitihada za kuhakikisha kwamba nchi inaendelea kuwa ya amani na utulivu na wananchi wanaendelea kufanya kazi zao za kimaendeleo bila hofu ya kufanyiwa uhalifu, tumeendelea kukamata wahalifu wa aina mbalimbali maeneo tofauti,” alisema.
Jeshi hilo kupitia kwa msemaji wake Bulimba, limeshukuru wananchi na kuomba waendelee kutoa taarifa za siri zisaidie kukamata watu wanaotuhumiwa kufanya uhalifu.
Hata hivyo, alipoulizwa kama watuhumiwa hao wana uhusiano wowote na matukio ya milipuko ya mabomu ya Arusha na Zanzibar, Bulimba hakuweka bayana zaidi ya kusema maeneo hayo ni sehemu ya Tanzania na watuhumiwa hao wamekamatwa maeneo tofauti nchini.
Pia alipoulizwa endapo watuhumiwa hao wana uhusiano wowote na vikundi vya nje vya uhalifu, bila kufafanua zaidi alisema, “naomba muelewe kwamba watuhumiwa hao wanaandaliwa kufanya uhalifu wa kitaifa na kimataifa”.

Wednesday, July 16, 2014

VAN GAAL AANZA KAZI OLD TRAFFORD



Louis van Gaal ameanza kazi rasmi Old Trafford siku ya Jumatano kwa kwenda kwenye uwanja wa mazoezi.
Kocha huyo Mholanzi aliteuliwa mwezi Mei, lakini amekuwa na timu ya taifa ya Uholanzi nchini Brazil, ambapo ilimaliza katika nafasi ya tatu.
Wachezaji wa Manchester United walirejea mazoezini Julai 4 chini ya kocha msaidizi Ryan Giggs.
Van Gaal atazungumza na waandishi wa habari kesho.



REAL MADRID TIMU "TAJIRI" DUNIANI - FORBES


Klabu ya kandanda ya Real Madrid ya Spain imeongoza katika orodha ya Forbes ya timu zenye thamani zaidi duniani.
Real Madrid, walioshinda Champions League mwezi Mei, ina thamani ya takriban dola BILIONI 3.44, kwa mujibu wa Forbes.
Forbes imesema tatu bora zote ni timu za soka. Barcelona imeshika nafasi ya pili, ikiwa na thamani ya dola bilioni 3.2 na Manchester United ni ya tatu ikiwa na thamani ya dola bilioni 2.81.
Forbes imetathmini thamani ya timu hizo kwa kutazama thamani ya hisa, madeni na mikataba ya viwanja vyao.
Timu ya New York Yankees ya baseball ya Marekani imeshika nafasi ya nne ikiwa na thamani ya dola bilioni 2.5. Nafasi ya tano inashikiliwa na Dallas Cowboys ya mchezo wa American Football ambayo ina thamani ya dola bilioni 2.3.

Tuesday, July 15, 2014

Ridhiwani Ataja 11 Wanaotosha Kugombea Urais 2015

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete ametaja majina 11 ya wanachama wa CCM wanaofaa kuwania urais kurithi kiti cha baba yake, Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda wake mwakani.

Ridhiwani (35), ambaye alishinda kiti cha ubunge wa Jimbo la Chalinze Aprili mwaka huu, alitaja majina hayo katika mahojiano maalumu na gazeti hili yaliyofanyika mjini Dodoma hivi karibuni.

Miongoni mwa aliowataja kuwa wana sifa ni makada watano walio chini ya uangalizi wa CCM wa mwaka mmoja baada ya kubainika kuanza kampeni za urais mapema, mawaziri wawili waliopoteza nyadhifa zao katika kashfa ya Operesheni Tokomeza, mwanamke mmoja na Rais wa Zanzibar.

“Kutaja majina tu, naweza kuorodhesha wengi tu. Naweza kuorodhesha hata watu 500, kwa sababu tunaona wengi sana,” alisema mtoto huyo wa Rais Kikwete ambaye amekuwa ndani ya CCM kwa muda mrefu akitokea umoja wa vijana wa chama hicho, UVCCM. “Kwa mfano, kwa upande wa Bara tunao Emmanuel Nchimbi, William Ngeleja, January Makamba, Bernard Membe, Steven Wassira, Edward Lowassa na Asha-Rose Migiro,” alisema.

Aliongeza: “Hawa ni kwa uchache zaidi… ni baadhi ya watu ambao wanatajwa kwa upande wa Bara, lakini jambo la msingi ni nani mwenye sifa za kuwa rais.”

Alisema pamoja na kwamba wanasiasa hao wote wanazo sifa za kuiwania nafasi hiyo ya juu, vikao vya chama ndivyo vitakuwa na nafasi ya kuwachuja ili kupata wanaotosha. “Kama wanatosha au la, vikao vya chama vitakaa kuamua licha ya kuwa hao wote niliowataja, kwa sifa za kugombea urais wote wanajitosheleza. Wana sifa, wana uwezo wa kugombea na wana uwezo wa kushinda, hao ni kwa upande wa Bara,” alisema.

Alipoulizwa hali ikoje kwa upande wa Zanzibar, Ridhiwani alisema, “Sisi chama chetu kina utajiri wa watu kwa upande wa Zanzibar kuna Shamsi Vuai Nahodha, Hussein Ali Mwinyi, Dk Seif Ally Iddi (Makamu wa pili wa Rais Zanzibar) na Dk Mohammed Ali Shein, Rais wa Zanzibar. Hawa ni watu ambao wana uwezo na hata wakipewa jukumu la kuongoza nchi hii wanaweza. Tunao wengi sana.”

Membe, Wassira, Lowassa, Ngeleja na Makamba walipewa adhabu na Kamati ya Maadili ya CCM ya kutogombea nafasi yoyote ndani ya chama wala kufanya kampeni baada ya kudaiwa kukiuka taratibu za chama hicho, wakati Nchimbi na Nahodha walilazimika kujiuzulu nyadhifa zao za uwaziri kutokana na kashfa ya Operesheni Tokomeza ambayo ililenga kushughulikia majangili, lakini ikahusishwa na vitendo vya ukiukaji haki za binadamu.

Ridhiwani hakumtaja Waziri Mkuu wa zamani, Fredrick Sumaye ambaye pia anatumikia adhabu hiyo ya Kamati ya Maadili ya CCM.

Sunday, July 13, 2014

Hatimaye timu ya Ulaya imefanikiwa kushinda Kombe la Dunia katika ardhi ya Amerika Kusini

Manuel Neuer kipa bora, Lionel Messi mchezaji bora







UJERUMANI MABINGWA WA KOMBE LA DUNIA 2014!!!!!!


Goli la Gotze

Goli la Gotze

Half time ya extra time Argentina 0-0 Ujerumani

Photo: Half time ya extra time
Argentina 0-0 Ujerumani

Gonzalo Higuain alitikisa nyavu- mwamuzi wa pembeni akayoosha kibendera- off side

Salim Kikeke's photo.

UKATILI: Mtoto Afichwa Uvunguni kwa Miaka 6 Huko Morogoro

Wakati jamii ikiwa bado haijasahau mateso aliyoyapata mtoto Nasra Mvungi na kusababisha  kifo chake, tukio lingine la aina hiyo limetokea katika Kijiji cha Matongola, Tarafa ya Magole Wilaya ya Kilosa, baada ya kubainika mtoto wa miaka sita akiwa amefichwa uvunguni mwa kitanda na kufanyiwa vitendo vya kikatili na mama yake mzazi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonald Paulo alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa taarifa za mateso ya mtoto huyo zilifikishwa Kituo cha Polisi wilayani Kilosa  saa za mchana jana, baada ya uongozi wa  kijiji na kata kutoa taarifa na tayari mwanamke huyo amekamatwa kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Mama aliyefanya ukatili huo anafahamika kwa jina la Sala Mazengo ambaye alimficha ndani mtoto wake aliyefahamika kwa jina la Devota Malole na kumfanyia vitendo vya kikatili ikiwa pamoja na kutompa chakula, wala kumfanyia usafi.

Baada ya kufichuliwa kutoka alipofichwa, mtoto huyo alionekana kuwa dhaifu kiafya kutokana na kukosa lishe pamoja na mazingira aliyokuwa akiishi kutoridhisha, jambo ambalo ni kosa kisheria, pia ukiukwaji wa haki za watoto.

Inadaiwa kuwa tangu mwaka 2009 Sala amekuwa akimficha mtoto wake huyo ambaye sasa amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa kwa ajili ya kupatiwa vipimo na matibabu.

Hata hivyo, mwanamke huyo alipoulizwa alidai kuwa afya ya mtoto wake ilikuwa mbaya tangu alipozaliwa kutokana na magonjwa ya mara kwa mara, pia hali ngumu ya maisha ilichangia kudhoofisha afya ya mtoto huyo.

Alidai kuwa ana watoto sita, pia alikiri kumlaza chini mtoto huyo kutokana na kuwa na kitanda kimoja, ambacho hakiwatoshi watoto hao.

Aliongeza kuwa hata chakula amekuwa akikipata kwa shida kutokana na kushindwa kufanya kazi kwa kuwa ana mtoto mwingine mdogo.

Kamanda Paulo alisema kuwa  mwili wa mtoto huyo umedhoofu kutokana na kufichwa ndani kwa muda mrefu na bado mwanamke huyo hajaeleza sababu za kufanya vitendo vya ukatili dhidi ya mtoto huyo.

“Siwezi kutoa taarifa ya kidaktari, lakini kutokana na afya ya mtoto yule na mazingira tuliyomkuta ni dhahiri alikuwa akipata mateso na kufanyiwa vitendo vya ukatili. Hata hivyo, uchunguzi zaidi tunaufanya na kwamba taratibu za kumfikisha mtuhumiwa huyo Kituo Kikuu cha Polisi mkoani hapa zinaendelea,” alisema Kamanda Paulo.

Alisema kuwa mpaka sasa bado haijafahamika kama mtoto Davota ni mlemavu au la na kwamba taarifa za afya ya mtoto huyo zitatolewa baada ya madaktari kumfanyia uchunguzi wa kina.

REFA WA FAINALI ATAJWA


Nicola Rizzoli amechaguliwa na Fifa kuwa mwamuzi katika mchezo wa fainali - Kombe la Dunia Brazil 2014 kati ya Ujerumani na Argentina.
Howard Webb kutoka England, aliyechezesha fainali ya Kombe la Dunia 2010 Afrika Kusini, aliorodheshwa lakini hakuchaguliwa.
Ujerumani itapambana na Argentina kwenye dimba la Maracanã, jijini Rio De Janeiro, siku ya Jumapili Julai 13.
Rizzoli ni msanifu majengo kutoka Bologna, na tayari amechezesha mechi tatu katika michuano ya Kombe la Dunia Brazil.
Mwamuzi huyo mwenye umri wa miaka 42 alichezesha mechi kati ya Spain dhidi ya Uholanzi, Nigeria na Argentina na Argentina ilipocheza na Ubelgiji.
Rizzoli pia alichezesha mchezo wa fainali ya Ligi ya Europa kati ya Atlètico Madrid dhidi ya Fulham mwaka 2010, na pia mchezo wa fainali ya Uefa Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2013 kati ya Bayern Munich na Borussia Dortmund.
Rizzoli atasaidiwa na waamuzi wa pembeni Renato Faverani na Andrea Stefani, na mwamuzi wa nne atakuwa Carlos Vera kutoka Ecuador.
Rizzoli atakuwa mwamuzi wa tatu kutoka Italy kuchezesha fainali, baada ya Sergio Ginella mwaka 1978 na Pierluigi Collina mwaka 2002.
Photo: REFA WA FAINALI ATAJWA
Nicola Rizzoli amechaguliwa na Fifa kuwa mwamuzi katika mchezo wa fainali - Kombe la Dunia Brazil 2014 kati ya Ujerumani na Argentina. 
Howard Webb kutoka England, aliyechezesha fainali ya Kombe la Dunia 2010 Afrika Kusini, aliorodheshwa lakini hakuchaguliwa. 
Ujerumani itapambana na Argentina kwenye dimba la Maracanã, jijini Rio De Janeiro, siku ya Jumapili Julai 13. 
Rizzoli ni msanifu majengo kutoka Bologna, na tayari amechezesha mechi tatu katika michuano ya Kombe la Dunia Brazil.
Mwamuzi huyo mwenye umri wa miaka 42 alichezesha mechi kati ya Spain dhidi ya Uholanzi, Nigeria na Argentina na Argentina ilipocheza na Ubelgiji. 
Rizzoli pia alichezesha mchezo wa fainali ya Ligi ya Europa kati ya Atlètico Madrid dhidi ya Fulham mwaka 2010, na pia mchezo wa fainali ya Uefa Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2013 kati ya Bayern Munich na Borussia Dortmund. 
Rizzoli atasaidiwa na waamuzi wa pembeni Renato Faverani na Andrea Stefani, na mwamuzi wa nne atakuwa Carlos Vera kutoka Ecuador. 
Rizzoli atakuwa mwamuzi wa tatu kutoka Italy kuchezesha fainali, baada ya Sergio Ginella mwaka 1978 na Pierluigi Collina mwaka 2002.

Saturday, July 12, 2014

Ukweli Kuhusu Kuzikwa Kwa Balali 'Kabari Lake Laonekana'

Mkazi wa Kijiji la Luganga, Wilaya ya Mufindi, Iringa, alikozaliwa Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daudi Ballali analazimika kutumia saa 32 kufika katika kaburi la kiongozi huyo lililopo eneo la Silver Spring, Maryland nchini Marekani.

Ndugu wa Ballali (pichani) wanaweza kutaka kwenda kuona kaburi la ndugu yao, kutokana na ukweli kwamba wengi wao hawakuwahi kupata fursa ya kumzika Gavana huyo ambaye alikuwa kiongozi wa juu kabisa wa taasisi kubwa inayosimamia masuala ya fedha na uchumi wa nchi.

Mwandishi wa gazeti hili alisafiri kwa saa 24 kutoka Dar es Salaam hadi Washington, Marekani ambako alithibitisha pasi na shaka kwamba Ballali alizikwa Mei 21, 2008 katika makaburi ya Gate of Heaven, baada ya kufariki dunia akiwa nyumbani kwake Maryland, Mei 16, mwaka huo.

Safari hiyo ya siku kumi, ilianza Alhamisi Juni 26, 2014 hadi Jumapili, Julai 6. Mwandishi wa habari hizi aliligundua kaburi hilo baada ya kwenda makaburi ya Gate of Heaven kwa siku tatu mfululizo.

Siku ya kwanza, mwenyeji wa mwandishi ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sasa alimfikisha katika makaburi hayo, lakini kaburi la Ballali halikuonekana na hata mwandishi alipokwenda siku ya pili peke yake, kaburi hilo pia halikuonekana kwa kutokana na ukubwa wa eneo hilo.

Siku ya tatu, Mwandishi wa Mwananchi alilazimika kuomba msaada wa Ofisi ya Makaburi ya Gate of Heaven, ambayo ilimsadia kuonyesha eneo lilipo kaburi hilo, hivyo kuwezesha kupata picha zake.

Kaburi lake liko katika msitari wa mwisho kabisa na Ukanda wa Kijani wa miti iliyozunguka makaburi ya Gate of Heaven, likiwa limeandikwa jina la kiongozi huyo, pamoja na maneno ya Kiingereza yanayosomeka “When the heart weep for what it has lost, the soul rejoices for what it has found”.

Maana ya maneno hayo ni kwamba “wakati moyo ukiomboleza kwa kile kilichopotea, roho hufurahi kwa kile kilichopatikana”. Kaburi hili limezungukwa na makaburi mengine kadhaa ambayo si ya Watanzania, kwani kwa haraka kutokana na mazingira yalivyokuwa, Mwandishi wa Mwananchi hakuweza kuona kaburi jingine lenye majina yenye asili au kuwa na mwelekeo wa asili ya Tanzania.

Uthibitisho huu ni tofauti na hekaya za miaka nenda rudi zilizogubika kifo cha kiongozi huyo, ambaye tangu alipoondoka nchini kwenda Marekani Agosti 2007, hakuwahi kurejea na badala yake zilisikika taarifa za kuugua kwake, kifo chake na baadaye mazishi yake yaliyokuwa ya siri kubwa yakiwahusisha ndugu wa karibu pekee.

Kutokana na mazingira hayo, kumekuwapo na uvumi kwamba Ballali hakufa na pengine amefichwa kusikojulikana, madai yanayochagizwa na mtu aliyejitokeza katika mitandao wa kijamii ya Twitter na facebook, akidai kwamba yeye ni Ballali na kwamba hajafa, huku akisisitiza kuwa wakati ukiwadia ukweli utafahamika.

Mtu huyo asiyefahamika hadi sasa alianza kujitokeza Twitter, Oktoba Mosi, 2012 pale aliposema “Nitakutana na Rais Kikwete (Jakaya) na ujumbe wake wiki hii hapa Marekani”. Mtu huyo alidai kwamba alikuja nchini Tanzania na kukaa karibu na Hoteli ya Hyatt Kempinski Kilimanjaro na baadaye kuondoka ghafla kwa kile alichokiita sababu za kiusalama.

Novemba 13 mwaka huo alituma ujumbe akisema:“In Dar es Salaam, Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kempinski Kilimanjaro Hotel. Feels good to be close to my former office, BoT,” akimaanisha kwamba niko Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, najisikia vizuri kuwa karibu na ofisi yangu ya zamani BoT.

Mtu huyo ambaye sasa tunaweza kuthibitisha kuwa ni feki amekuwa akiendelea kutuma ujumbe akijitambulisha kwa jina hilo la Ballali.

Ballali alifariki dunia kama ilivyotagazwa, lakini ilikuwaje akaenda safarini Washington, ugonjwa wake na hata kifo chake kilikuwaje? Je ndugu zake wanasemaje, safari

Friday, July 11, 2014

WAZIRI wa Ujenzi, Dk John Magufuli amesisitiza Serikali haitaweka matuta ya vizuizi vya kupunguza ajali katika barabara zote zilizoko nchini.
Alisema hayo juzi katika Kijiji cha Igogo wilayani Igunga Mkoa wa Tabora, baada ya wananchi kulalamika juu ya ajali zinazotokea katika eneo lao kutokana na mwendo kasi wa magari.
Magufuli alisema, kwa sasa serikali haiwezi kuweka matuta katikati ya barabara kwani ikiweka matuta itakuwa imevunja Sheria za Usalama Barabarani Namba 32 ya mwaka 1973.
Alisema alama zitakazowekwa ni za pundamilia. Waziri huyo ambaye alionya juu ya vitendo vya wananchi, kung’oa alama zinazowekwa barabarani, alihimiza wazitunze.
Awali, zilisikika sauti kutoka kwa wananchi zikieleza furaha ya ujio wa Waziri Magufuli, huku wakimwomba wawekewe matuta katika eneo hilo, kutokana na ajali zinazotokea mara kwa mara.
“Ujio wako leo kwetu ni furaha kubwa kwa sisi wakazi wa kijiji cha Igogo, hivyo tunakuomba sana utuwekee matuta eneo hili kwani zaidi ya watu wanne wamepoteza maisha kwa kugongwa na gari,” alisikika mmoja wananchi hao.
Wakati huo huo, Waziri alitembelea daraja la mto wa Mbutu na kukagua ujenzi unaoendelea.
Pia, alizungumza na wananchi wa kata ya Mbutu katika eneo hilo la daraja, linalotarajia kukamilika mwezi ujao. Magufuli alisema serikali inatambua kudaiwa fedha na wakandarasi, wanaojenga barabara za lami sehemu mbalimbali nchini.
Alisema wakati jiwe la msingi la ujenzi wa lami lilipowekwa, wapo baadhi ya watu walisema haitajengwa Mkoa wa Tabora “Lakini kwa sasa wamejionea wenyewe kwa macho yao lami iliyojengwa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi,” alisema.
Hata hivyo, alisema gharama za ujenzi wa barabara ya lami mkoani Tabora ni zaidi ya Sh bilioni 500, ambazo hakuna fedha zilizotolewa na wafadhili, bali yote ni ya serikali.
Alisisitiza, serikali chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete ni tajiri, ikizingatiwa kwamba wakoloni waliacha kilometa 1,300 za barabara za lami, lakini, sasa serikali ya Kikwete imejenga kilometa 11,154 za lami na kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tano Afrika, zinazotumia fedha zake za ndani.
Kuhusu madeni ya kampuni za ukandarasi mkoani Tabora, alisema ni Sh bilioni 111. Kati ya hizo, kampuni sita za China zinadai Sh bilioni 105 huku kampuni za Tanzania zikidai Sh bilioni sita.
Kwa upande wa nchi nzima, Magufuli alisema serikali inadaiwa zaidi ya Sh bilioni 600. Hata aliwahakikishia wakandarasi watalipwa fedha zote.
 

Thursday, July 10, 2014

Zohra Sehgal wa Bollywood Afariki Dunia;

Mcheza filamu Zohra Sehgal wa India, maarufu kama mkongwe wa Bollywood, amefariki dunia mjini Delhi akiwa na umri wa miaka 102. Mkongwe huyo alianza fani yake kama mcheza dansi na baadaye kuingia katika uigizaji ambapo alijipatia tuzo kadhaa katika filamu za Bollywood. Katika miaka ya 1960 alihamia London ambapo aliishi kwa miaka 30 kabla ya kurejea India. Filamu ambazo ametajwa za Hollywood na za Uingereza ni: Never Say Die, Bend It Like Beckham, The Jewel in the Crown, My Beautiful Laundrette na Bhaji on the Beach.
Mcheza filamu Zohra Sehgal wa India, maarufu kama mkongwe wa Bollywood, amefariki dunia mjini Delhi akiwa na umri wa miaka 102. Mkongwe huyo alianza fani yake kama mcheza dansi na baadaye kuingia katika uigizaji ambapo alijipatia tuzo kadhaa katika filamu za Bollywood. Katika miaka ya 1960 alihamia London ambapo aliishi kwa miaka 30 kabla ya kurejea India. Filamu ambazo ametajwa za Hollywood na za Uingereza ni: Never Say Die, Bend It Like Beckham, The Jewel in the Crown, My Beautiful Laundrette na Bhaji on the Beach.


Wednesday, July 9, 2014

Formation Hapa kweli pagum wewe je upo wapi?

Salim Kikeke's photo.Salim Kikeke's photo.

  Hii ndoo mechi kail kutoke wengi walidhani kuwa haya yangifanywa na wenyeji Bra71L

Kura yako inakwenda kwa nani? UHOLANZI au ARGENTINA?

                       
Uholanzi   na  Argentina

               


Monday, July 7, 2014

ASHLEY COLE ASAINI ROMA

Beki wa zamani wa Chelsea Ashley Cole amejiunga na klabu ya Roma ya Italia kwa mkataba ya miaka miwili.
Roma ime 'tweet' picha ya Cole na kuthibitisha kupitia tovuti yao kuwa mchezaji huyo amesaini mkataba hadi mwaka 2016.
Ashley Cole ameichezea Chelsea kwa miaka minane, akishinda ligi kuu mwaka 2010 na Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2012.
Pia alishinda vikombe vinne vya FA na Chelsea, kuongeza vitatu alivyoshinda akiwa na Arsenal ambayo alishinda nayo makombe mawili ya ligi pia.

Wednesday, July 2, 2014

SHEHE Mkuu Amcharukia Jackline Wolpe

TABIA ya staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper kubadilibadili dini mara kwa mara imeonekana kuwakera watu mbalimbali akiwemo Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum ambaye amemcharukia vikali.

Wolper kiimani ni Mkristo lakini hivi karibuni alibadili na kuwa Muislam kabla ya kurejea tena kwenye imani yake ya awali ya ukristo.

Sababu ya Wolper kubadili dini ilikuwa ni kufunga ndoa na aliyekuwa mchumba wake Abdallah Mtoro ‘Dalas’, walipoachana akaamua kurudi kwenye ukristo.

Akizungumza na Risasi Jumamosi juzikati, Shehe Salum, alisema Wolper anapaswa kujichunguza na kubadilika haraka kwani kitendo anachofanya ni kinyume na taratibu za dini.
“Siyo vizuri hata kidogo na hata dini zote zinakemea kitendo cha kuchezeachezea dini kwani ni chukizo kwa Mungu.

“Kwa upande wa Dini ya Kiislamu, kuna sheria kali zaidi kwa mtu akionekana na tabia hiyo, anaweza hata kuuawa hivyo wanaofanya mchezo huo waache kwani siyo vizuri. Huko ni kumfanyia Mungu dhihaka,” alisema Shehe Salum na kuongeza:

“Unajua suala la imani ni kitu kinachomhusu mtu binafsi, ni vyema kufanya uamuzi wa hakika na kushika njia moja na siyo kufanya dhihaka na dini ya Mwenyezi Mungu. Ni kitu kibaya sana.”
Naye Juma Suleiman, mkazi wa Ilala, jijini Dar es Salaam alimwambia mwandishi wetu kuwa, katika imani ya kiislam kunakatazwa watu kucheza na dini huku akisisitiza anayefanya hivyo anaweza kulaaniwa.

Dini siyo kitu cha kuchezea, ni daraja la kumfikisha mtu kwenye haki, si mahala pa kuingia na kutoka, kuingia na kutoka. Huko ni kucheza na Mungu. Namshauri huyo mtoto (akimaanisha Wolper) abadilike. Asifanye mchezo na imani, Mungu anaweza kumlaani kwa kumchezea,” alisema Suleiman

Serikali yathibitisha kifo cha balozi wa Libya

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Asa Mwambene. Mwambene amesema mpaka sasa chanzo cha kifo cha balozi huyo hakijajulikana.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Assa Mwambene. Mwambene amesema mpaka 
sasa chanzo cha kifo cha balozi huyo hakijajulikana.
Msemaji wa serikali hapa nchini Assa Mwambene amekiri kutokea kwa kifo cha Balozi Msaidizi wa Libya nchini bwana Ismail Nwairat kwa kujipiga risasi mwenyewe majira ya saa saba usiku katika chumba cha ofisi za ubalozi huo.
Mwambene alisema kuwa mpaka sasa haijafahamika kifo cha balozi huyo kimetokana na nini, ila wafanyakazi wa karibu katika ubalozi huo wamesema kuwa walisikia mlio wa risasi chumbani kwake, na walipojaribu kufungua mlango ulikuwa umefungwa na wakatumia nguvu ya kuvunja mlango huo na kufanikiwa kumkuta balozi yupo katika hali ya mbaya.
Aidha walimuwahisha katika hospital ya Ami iliyopo Oysterbay na baada ya nusu saa madaktari walithibitisha kuwa amefarika dunia.
Serikali imesikitishwa na kifo hicho na wanafanya utaratibu wote wa kuusafirisha mwili wa marehemu kuupeleka nchini kwao kwa ajili ya mazishi.

DIAMOND KATIKA RED CARPET YA TUZO ZA BET

Photo: DIAMOND KATIKA RED CARPET YA TUZO ZA BET
Picha kutoka Michuzi Matukio
http://michuzi-matukio.blogspot.co.uk/2014/07/diamond-platnumz-bet-red-carpet-and.html#more 
DIAMOND NDANI YA BET