Thursday, November 27, 2014

Waziri Prof Muhongo asema fedha za Escrow si mali ya umma, adai bado Serikali inadaiwa

                                        Prof. sospeter muhongo waziri wa nishati na madini
 Sakata la uchotwaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow linaendelea kuchukua sura mpya baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo kutoa ufafanuzi wa Serikali bungeni mjini Dodoma kuwa fedha hizo si za umma na kwamba bado Serikali ina mzigo wa madeni katika sakata hilo.
Kauli ya Prof Muhongo inakuja siku moja baada ya Kamati ya PAC kuwasilisha ripoti yake jana juu ya suala hilo ambapo pamoja na mambo mengine, Kamati ya PAC ilijiridhisha kuwa sehemu ya fedha hizo ni za Serikali.
Mwenyekiti wa hesabu za Serikali bungeni  PAC Zitto Kabwe










Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe akisoma taarifa ya kamati hiyo jana alisema Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Francis Mwakapalila, Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade wakithibitisha kuwa sehemu ya fedha zilizokuwamo kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow zilikuwa za Serikali.
Akiwasilisha maelezo ya Serikali leo, Prof Muhongo alipangua hoja moja baada ya nyingine zilizotolewa na Kamati ya PAC jana na kusisitiza kuwa fedha hizo si mali ya umma.

No comments:

Post a Comment