![]() |
Balozi Ombeni Sefue |
Dar es Salaam. Serikali inapitia upya ulinzi wa viongozi wastaafu ili kuepuka fedheha iliyotokana na vurugu alizofanyiwa Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba hivi karibuni.
Mpango huo umeelezwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue mwishoni mwa wiki, akisema Serikali imekerwa na kufedheheshwa kutokana na tukio hilo lililotokea wakati wa mdahalo wa Katiba Inayopendekezwa katika Hoteli ya Blue Pearl, Dar es Salaam Novemba 2, mwaka huu.
“Kimsingi tutakachokifanya ni kupitia upya mpango wa ulinzi wa viongozi wote waliostaafu, japokuwa huwa tunafanya hivyo mara kwa mara, lakini kwa hili la Mzee Warioba tunaliangalia kwa umakini wake.
“Tumekerwa sana na tukio lile, halikutufurahisha hata kidogo kama Serikali kwa kuwa limemvunjia heshima Mzee Warioba, yule ni mzee wetu, anahitaji heshima, kwanza heshima yake na ulinzi.”
No comments:
Post a Comment