![]() |
Rais J.Kikwete akisalimiana na Dr.aliye mapatia matibabu |
Rais Jakaya Kikwete awasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere akitokea nchini Marekani kwa matibabu. Apokelewa na wakazi wa DSM
Anaongea na waandishi wa habari pamoja na wananchi waliopo uwanjani
Rais kikwete :- Waambieni watanzania kuwa nimerudi na afya nzuri ingawa bado najiuguza sehemu niliyochanwa.
Rais kikwete :- Nimefanyiwa upasuaji wa tezi dume, Tezi ambayo wanayo wanaume pekee wanawake hawana,si Busha kwa inavyosemekana
Rais kikwete :- Ni kawaida yangu kufanya uchunguzi wa afya, hata mwaka 1984 nilipotoka China, nilifanya ukaguzi wa vyote
Rais kikwete :- Ni kawaida yangu kufanya uchunguzi wa afya, hata mwaka 1984 nilipotoka China, nilifanya ukagauzi wa vyote
Rais kikwete :- Wasukuma wanaamini kuwa ni ugonjwa ule wa kula madafu, siyo hivyo
Rais kikwete :- Tulishauriana na madaktari, tukakubaliana kufanya upasuaji katika hospitali ya Johns Hopkins ambao ni mabingwa
Rais kikwete :- Kwa upande wangu hali niliyokuwa nayo ni hatua ya Kwanza ya Saratani ambayo inatibika kwa upasuaji
Hata hivyo Rais ametoa wito kwa watanzania kufanya uchunguzi wa afya zao mara kwa mara magonjwa yote likiwemo maambukizi ya HIV
Rais ametoa shukrani kwa wananchi,viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa kwakuwa pamoja katika kipindi chote kigumu cha marazi na matibabu yake.
Vilevile alieleza kuhusu swala la sakata la IPTL la akouti ya tegeta-ESCROW kuwa hatoweza kulitolea maelezo kwavile alikuwa kwenye matubabu na hajapatiwa maelezo yoyote na kuhaidi litapatiwa majibu na Serikali.
![]() |
Rais J.Kikwete akiongea na wandishi wa habari baada ya kulejea kutoka kwenye matibabu Marekani |
No comments:
Post a Comment