Mwenyekiti wa hesabu za serikali Bungeni (PAC) Zitto Kabwe |
Mwenyekiti wa PAC Zitto Kabwe amesoma maazimio mapya ya Bunge kwa mujibu wa kamati maalumu iliyoundwa leo na kuhusisha CCM, PAC na UKAWA
Azimio la bunge:- Mamlaka ya uteuzi iwawajibishe na inashauriwa kutengua uteuzi wa Waziri wa Nyumba, ardhi na makazi Prof Tibaijuka, Waziri wa Nishati na Madini Prof Muhongo, Mwanasheria Mkuu wa serikali Jaji Werema, na Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Maswi
Azimio la bunge:- Bunge liwawajibishe wabunge ambao ni sehemu ya bodi ya TANESCO na viongozi wa Kamati za Bunge
Azimio la bunge:- Mamlaka husika ziitangaze Benki ya Stanbic, Mkombozi na benki yoyote nyingine itakayogundulika kuwa zinahusika na utakatishaji wa fedha haramu
Azimio la bunge:- Kwa kuwa majaji walihusika, Rais aunde Tume ya kijaji ya uchunguzi na kuwasimamisha jaji Mujulusi na Prof Luhangisa
Azimio la bunge :- Serikali ipitie upya mikataba ya Umeme na itoe taarifa kabla ya kumalizika kwa mkutano ujao wa bunge la Bajeti
Azimio la bunge :- Serikali ichukue mitambo ya IPTL na iikabidhishe kwa TANESCO
Azimio la bunge:- TAKUKURU na Polisi wamchukulie hatua bwana Sethi, na kumfungulia mashitaka akithibitika
![]() |
Sethi muwekezaji wa IPTL anayetuhumiwa na sakata la akaunti ta Tegeta-ESCROW |
Hata hivyo serikali kupitia kwa waziri Wasira alitoa msisitizo kwa kilicho pendekezwa: Tuamini kwamba haya yote ni kwa maslahi ya watanzania, CCM imeshirikiana na kambi ya upinzani kufanya maamuzi sahihi.
No comments:
Post a Comment