![]() |
Mwenyekiti wa petroli Tanzania(TPDC),Michael Mwenda na James Andilile wakipandishwa gari ya polisi |
![]() |
Mwenye kiti wa (PAC) Zitto Kabwe |
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Michael Mwanda na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, James Andilile jana walikamatwa na polisi kwa agizo la na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), inayoongozwa na Zitto Kabwe kwa kushindwa kuwasilisha mikataba 26 ya gesi na mapitio yake mbele kamati hiyo tangu mwaka 2012.
Baada ya kukamatwa, Mwanda na Andilile walipandishwa katika gari dogo la wazi (pick-up) la polisi na kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi ambako taarifa iliyotolewa baadaye jioni na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ilisema viongozi hao wameachiwa huru kusubiri sheria na taratibu za Bunge.
Kamanda Kova alisema baada ya kuwakamata ilibainika kwamba katika Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya 296 Kifungu cha 12 (3) kinamtaka Mwenyekiti wa PAC kupendekeza kwa Spika wa Bunge kwanza kuhusu jambo lolote aliloliona kama ni kosa.
“Spika akisharidhika kuhusu tuhuma zozote zilizoletwa mezani kwake ndipo anamwandikia Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili suala hilo lipate ufafanuzi wa kisheria ikiwa ni pamoja na hatua za kisheria zinazostahili kuchukuliwa.
No comments:
Post a Comment