Saturday, November 29, 2014

J.K arejea nchini na afya bora baada ya matibabu Mrekani



Rais J.Kikwete akisalimiana na Dr.aliye mapatia matibabu

Rais Jakaya Kikwete awasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere akitokea nchini Marekani kwa matibabu. Apokelewa na wakazi wa DSM
Anaongea na waandishi wa habari pamoja na wananchi waliopo uwanjani
Rais kikwete :-  Waambieni watanzania kuwa nimerudi na afya nzuri ingawa bado najiuguza sehemu niliyochanwa.
Rais kikwete :-  Nimefanyiwa upasuaji wa tezi dume, Tezi ambayo wanayo wanaume pekee wanawake hawana,si Busha kwa inavyosemekana
Rais kikwete :-  Ni kawaida yangu kufanya uchunguzi wa afya, hata mwaka 1984 nilipotoka China, nilifanya ukaguzi wa vyote
Rais kikwete :-  Ni kawaida yangu kufanya uchunguzi wa afya, hata mwaka 1984 nilipotoka China, nilifanya ukagauzi wa vyote
Rais kikwete :-  Wasukuma wanaamini kuwa ni ugonjwa ule wa kula madafu, siyo hivyo
Rais kikwete :-  Tulishauriana na madaktari, tukakubaliana kufanya upasuaji katika hospitali ya Johns Hopkins ambao ni mabingwa
Rais kikwete :-  Kwa upande wangu hali niliyokuwa nayo ni hatua ya Kwanza ya Saratani ambayo inatibika kwa upasuaji
Hata hivyo Rais ametoa wito kwa watanzania kufanya uchunguzi wa afya zao mara kwa mara magonjwa yote likiwemo maambukizi ya HIV
Rais ametoa shukrani kwa wananchi,viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa kwakuwa pamoja katika kipindi chote kigumu cha marazi na matibabu yake.
Vilevile alieleza kuhusu swala la sakata la IPTL la akouti ya tegeta-ESCROW kuwa hatoweza kulitolea maelezo kwavile alikuwa kwenye matubabu na hajapatiwa maelezo yoyote na kuhaidi litapatiwa majibu na Serikali.
Rais J.Kikwete akiongea na wandishi wa habari baada ya kulejea kutoka kwenye matibabu Marekani

Bunge limepitisha maazimio ya sakata la IPTL akauti ya Tegeta-ESCROW



Mwenyekiti wa hesabu za serikali Bungeni (PAC) Zitto Kabwe
Mwenyekiti wa PAC Zitto Kabwe amesoma maazimio mapya ya Bunge kwa mujibu wa kamati maalumu iliyoundwa leo na kuhusisha CCM, PAC na UKAWA
Azimio la bunge:-  Mamlaka ya uteuzi iwawajibishe na inashauriwa kutengua uteuzi wa Waziri wa Nyumba, ardhi na makazi Prof Tibaijuka, Waziri wa Nishati na Madini Prof Muhongo, Mwanasheria Mkuu wa serikali Jaji Werema, na Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Maswi
Azimio la bunge:-  Bunge liwawajibishe wabunge ambao ni sehemu ya bodi ya TANESCO na viongozi wa Kamati za Bunge
Azimio la bunge:-  Mamlaka husika ziitangaze Benki ya Stanbic, Mkombozi na benki yoyote nyingine itakayogundulika kuwa zinahusika na utakatishaji wa fedha haramu
Azimio la bunge:-  Kwa kuwa majaji walihusika, Rais aunde Tume ya kijaji ya uchunguzi na kuwasimamisha jaji Mujulusi na Prof Luhangisa
Azimio la bunge :-  Serikali ipitie upya mikataba ya Umeme na itoe taarifa kabla ya kumalizika kwa mkutano ujao wa bunge la Bajeti
Azimio la bunge :-  Serikali ichukue mitambo ya IPTL na iikabidhishe kwa TANESCO
Azimio la bunge:-  TAKUKURU na Polisi wamchukulie hatua bwana Sethi, na kumfungulia mashitaka akithibitika
Sethi muwekezaji wa IPTL anayetuhumiwa na sakata la akaunti ta Tegeta-ESCROW
Hata hivyo serikali kupitia kwa waziri Wasira alitoa msisitizo kwa kilicho pendekezwa: Tuamini kwamba haya yote ni kwa maslahi ya watanzania, CCM imeshirikiana na kambi ya upinzani kufanya maamuzi sahihi.

Friday, November 28, 2014

MAAZIMIO YA MAPENDEKEZO YA KAMATI YA ZITTO YALIVYOPITISHWA HADI 1 - 6!



1. Tunapendekeza kwamba vyombo vinavyohusika viendelee na uchunguzi kubaini jinai, ikithibitika achukuliwe hatua za kisheria...Azimio la kwanza limepita
2. Tundu Lissu: Vyombo viendelee kuchunguza pesa zilizogawiwa na Rugemalira na ikithibitika wachukuliwe hatua. Pendekezo la pili kuhusu Rugemalira, serikali imeweka marekebisho kuhusu uhalali wa pesa za Rugemalira alizogawa, Bunge limeazimia uchunguzi uendelee kufanyika
3. Azimio la 3 limerekebishwa kuwa waliopokea pesa wachunguzwe na kuchukuliwa hatua mahususi kwa mujibu wa sheria
4. Pendekezo la 4. Kamati inazitaka mamlaka kuzitangaza benki za Mkombozi na Stanbic kama asasi za utakatishaji fedha. Azimio la 4 limepita kwamba Kamati inazitaka mamlaka husika ikiwemo benki kuu kuchukua hatua dhidi ya benki zote zilizohusika
5. Azimio la 5:Serikali ipitie upya mikataba yote ya umeme na kutoa taarifa kabla ya kumalizika kwa Bunge la bajeti lijalo
6. Azimio la 6: Limepita kwamba mamlaka husika ziivunje bodi ya TANESCO na kuiunda upya kwa lengo la kuongeza ufanisi
Hata hivyo maazimio hayo yalishindwa kufikia muahafaka baada ya mapendekezo ya kupanguliwa kwa waziri wa nishati na madini profesa Sospeter Muhongo ayatolee Rais na sio bunge ndipo bahadhi ya wabunge walisimama na kushinikiza achie ngazi bila mafanikio,ndipo spika wa bunge Anne Makinda alifikia uhamuzi wa kuhailisha bunge hadi hapo itakapo tangazwa kwa mujibu wa spika wa bunge.

Mahakama yamtakasa Sheikh Issa Ponda

Sheikh Issa Ponda akiwa mahamani akisikiliza mashitaka yanayo mkabili
Dar es Salaam. Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemtakasa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda dhidi ya hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyomtia hatiani katika kesi ya jinai iliyotokana na mgogoro wa ardhi wa Chang’ombe Markazi.

Sheikh Issa Ponda akitoka mahama ya hakim mkazi kisutu akiwa chini ya ulizi mkali wa makachero
Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Agustine Shangwa baada ya kuridhika na hoja za rufani za Sheikh Ponda kupitia kwa Wakili wake, Juma Nassoro kupinga hukumu na hatia ya Mahakama ya Kisutu.

Mbali na kumfutia hatia hiyo, pia Jaji Shangwa alimshauri Sheikh Ponda kufungua kesi ya madai dhidi ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), pamoja na Kampuni ya Agritanza Ltd iliyonunua eneo la Chang’ombe Markazi.
Ponda alikata rufani mahakamani hapo akipinga hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyomtia hatiani katika kesi ya jinai namba 245 ya mwaka 2012, iliyokuwa ikimkabili yeye na wenzake 49.
Katika rufaa hiyo, Sheikh Ponda kupitia kwa wakili wake, Nassoro aliwasilisha jumla ya hoja sita za kupinga hukumu hiyo.
Hoja hizo zilikuwa ni pamoja na ya kudai kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikosea kumtia hatiani kwa kuwa hapakuwa na ushahidi wa kutosha kumtia hatiani kwa kosa hilo la kuingia kwa nguvu katika eneo hilo la mgogoro.

Thursday, November 27, 2014

Wakazi wa eneo la Sido jijini Mbeya wakifuatilia kwenye Tv wakati ripoti ya IPTL ilipokuwa ikawasilishwa bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Zitto Kabwe


Chenge, Tibaijuka, Kilaini walipuliwa mabilioni ya IPTL

Mwenyekiti wa hesabu za serikali bungeni PAC Zitto Kabwe

Dar es Salaam.
 Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imewataja vigogo wa serikali, wanasiasa na viongozi wa dini watatu walionufaika na uchotwaji wa Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow na jinsi baadhi walivyotumia mifuko ya plastiki kuzibeba.
Akisoma maoni ya kamati hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zitto Kabwe aliwataja waliochukua fedha hizo kutoka kwa mkurugenzi wa VIP, James Rugemalira na kiwango walichopokea katika mabano kuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti na Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge (Sh1.6 bilioni) na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka (Sh1.6 bilioni).
waziri wa ardhi,nyuma,makazi na maendeleo ya jamii Profesa Anna Tibaijuka
Wengine ni aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini ambaye pia ni mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (Sh40.4 milioni), aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona (Sh40.4 milioni), Mbunge mstaafu wa Sumbawanga (CCM), Paul Kimiti (Sh40.4 milioni), aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya Tanesco, Dk Enos Bukuku (Sh161.7 milioni).
Mwana sheria mstaafu wa Tanzania Andrew Chenge
Alisema majaji walioingiziwa fedha ni Jaji Profesa Eudes Ruhangisa (Sh404.25 milioni) na Jaji A.K Mujulizi (Sh40.4 milioni).

Kwa upande wa watumishi wa umma, Zitto alisema kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usajili wa Vizazi na Vifo (Rita), Philip Saliboko (Sh40.4 milioni), aliyekuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Emmanuel Daniel Ole Naiko (Sh40.4 milioni) na ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Lucy Appollo (Sh80.8 milioni).
Zitto alisema, “Kwa upande wa viongozi wa dini ambao waliingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni Askofu Methodius Kilaini (Sh80.9 milioni), Askofu Eusebius Nzigirwa (Sh40.4 milioni) na Padri Alphonce Twimannye Simon (Sh40.4 milioni).
Aliongeza, “Kamati ya PAC ilithibitishiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru kuwa baadhi ya watu walienda kugawana fedha kwenye benki tajwa (Mkombozi) wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi, maboksi, magunia na lumbesa.”
Mkurugenzi Rugemalira
Zitto alisema Mkurugenzi Mtendaji wa VIP Engeneering, James Rugemalira alipata mgawo wa Dola za Marekani Sh75 milioni kutoka katika fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow na kuzigawa kwa watu mbalimbali.

James Rugemalira
Rugemalira ambaye alikuwa na hisa 3 kati ya 10 za kampuni ya IPTL, alichukua kiasi hicho cha fedha na kukipeleka katika Benki ya Mkombozi inayomilikiwa na Kanisa Katoliki.
Zitto alisema Rugemalira alionekana kuhusika na IPTL pale alipofungua shauri mahakamani kuomba kuiondoa IPTL kwenye ufilisi na kisha kuuza hisa zake kwa kampuni ya PAP.
Alisema baada ya uamuzi wa Kahakama Kuu kutolewa Septemba 5, 2013, fedha za Escrow zilitolewa kwa haraka na kupelekwa katika benki hiyo baadaye kugawiwa kwa vigogo hao.
Kamati hiyo imekabidhiwa taarifa za Benki za Stanbic na Mkombozi ambazo zimeonyesha namna ambavyo fedha zilichukuliwa na watu na kampuni mbalimbali.
Ripoti hiyo ya PAC iliyosomwa jana ilikuwa na kurasa 116 na maneno 16,979.

Waziri Prof Muhongo asema fedha za Escrow si mali ya umma, adai bado Serikali inadaiwa

                                        Prof. sospeter muhongo waziri wa nishati na madini
 Sakata la uchotwaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow linaendelea kuchukua sura mpya baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo kutoa ufafanuzi wa Serikali bungeni mjini Dodoma kuwa fedha hizo si za umma na kwamba bado Serikali ina mzigo wa madeni katika sakata hilo.
Kauli ya Prof Muhongo inakuja siku moja baada ya Kamati ya PAC kuwasilisha ripoti yake jana juu ya suala hilo ambapo pamoja na mambo mengine, Kamati ya PAC ilijiridhisha kuwa sehemu ya fedha hizo ni za Serikali.
Mwenyekiti wa hesabu za Serikali bungeni  PAC Zitto Kabwe










Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe akisoma taarifa ya kamati hiyo jana alisema Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Francis Mwakapalila, Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade wakithibitisha kuwa sehemu ya fedha zilizokuwamo kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow zilikuwa za Serikali.
Akiwasilisha maelezo ya Serikali leo, Prof Muhongo alipangua hoja moja baada ya nyingine zilizotolewa na Kamati ya PAC jana na kusisitiza kuwa fedha hizo si mali ya umma.

Saturday, November 15, 2014

UTAFITI:Zaidi ya 9% ya watanzania wenye umri wa miaka 20 wanasumbuliwa na Maradhi ya Kisukari.

Utafiti uliofanywa na wizara ya afya nchni umebaini zaidi ya asilimia 9 ya watanzania wenye umri wa miaka 20 na kuendelea wanasumbuliwa na maradhi yasiyoambukiza ya kusukari.
Akifungua semina na upimaji wa sukari kwa wabunge na wafanyakazi wa ofisi ya Bunge,waziri wa afya na ustawi wa jamii Dokta Seif Rashid amesema mchango  wa magonjwa yasiyoambikiza katika magonjwa yote imeongezeka kutoka asilimia 10 hadi 30 mwaka huu na kuwaomba wabunge kufanya mazoezi mara kwa mara kuzingatia vyakula wanavyoshauriwa ili kukabiliana na tatizo hilo.
 
Awali wenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya huduma za jamii Mhe.Margaret Sitta amesema watanzania wanashtuka wanaposikia maradhi kama ukimwi na ebola kutokana na kutisha lakini wanasahau kuna maradhi mengine kama sukari,shinikizo la moyo,kansa yanaendelea kusababisha vifo vya watanzania wengi zaidi kila siku.
 
Novemba 14 ni siku ya maradhi ya sukari Duniani ambapo tafiti za ugonjwa huo zimeonyesha ifikapo mwaka 2035 kutakuwa na wagonjwa milioni 592 Duniani kote ambapo katika Bara la afrika kutakuwa na wagonjwa milioni 41.4 na nusu ya wagonjwa hao watakuwa hawajaanza matibabu,Ambapo kwa sasa asilimia 80 ya wagonjwa wa kisukari wanaishi katika nchni zinazoendelela ikiwemo tanzania.

Ukawa: CCM wajiandae kwa anguko 2015

Viongozi wa Katiba ya wananchi (UKAWA)
Zanzibar. Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Zanzibar wameibeza ripoti iliyotolewa wiki hii na Taasisi ya Twaweza, wakisema haielezi hali halisi ilivyo.
Wamesema kwamba kutokana na ukweli huo, CCM iwe tayari kupokea matokeo magumu ya anguko katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani.
Tamko hilo limetolewa na viongozi wa vyama vinavyounda umoja huo, walipozungumza gazeti hili kwa nyakati tofauti, kufuatia ripoti ya utafiti ya Twaweza, inayoonyesha kuwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa anaongoza kati ya wagombea wanaotajwa kama uchaguzi ungefanyika sasa.
Makamu mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi Haji Ambari Khamis alisema kwamba muungano huo unakwenda na ajenda tatu katika kampeni za Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa na uchaguzi mkuu wa mwakani.
Alizitaja ajenda hizo kuwa ni pamoja na tatizo la umaskini, kudhrauriwa kwa Katiba ya wananchi, kuongezeka rushwa na ufisadi hali inayoathiri wananchi wa pande zote mbili za muungano.
“Kama mipango na mikakati itakwenda bila ya kujitokeza mabadiliko, CCM watakuwa na wakati mgumu kwa nafasi zote za wagombea ikiwemo urais wa Muungano na Zanzibar,” alisema Ambari ambaye pia aligombea urais wa Zanzibar mwaka 2010.
Upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Zanzibar (Chadema), Said Issa Mohamed alisema kuwa Ripoti ya Twaweza inapotosha ukweli dhidi ya nguvu za Ukawa katika kuelekea uchaguzi wa mwakani.

Monday, November 10, 2014

MFUKO WA KUPAMBANA NA EBOLA WAANZISHWA

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Dlamini Zuma
Viongozi wa juu wa maswala ya biashara barani Afrika wameanzisha mfuko wa kusaidia nchi zilizoathiriwa na ugonjwa wa Ebola.
Kiasi cha dola milioni 28.5 zilipatikana katika mkutano wa harambee mjini Addis Ababa nchini Ethiopia kwa ajili ya kuwapeleka wahudumu wa afya nchini Guinea, Sierra Leone na Liberia.
Wataalam wanasema kama wanataka kukabili ugonjwa huu kwa kasi hakuna budi kuanza na nchi hizo tatu.
Takriban watu 5000 kati ya 14,000 wamepoteza maisha kutokana na Virusi vya ugonjwa huu hasa nchini Liberia.
Akiongea baada ya mkutano wa Addis Ababa, mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Dlamini Zuma amesema rasilimali zilizokusanywa zitakua sehemu ya mchakato wa kupambana na ugonjwa huo siku za usoni.
mkutano wa Addis Ababa umefanyika wakati Liberia ilipotangazwa na Shirika la madaktari wasio na mipaka,MSF kuwa imefanikiwa kupunguza idadi ya maambukizo mapya.
Hata hivyo shirika hilo limesema bado Ebola iko kwa kiasi kikubwa nchini Guinea na Sierra Leone.

TAMKO: Ikulu: Tumefedheheshwa Jaji Warioba kushambuliwa

Balozi Ombeni Sefue
Dar es Salaam. Serikali inapitia upya ulinzi wa viongozi wastaafu ili kuepuka fedheha iliyotokana na vurugu alizofanyiwa Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba hivi karibuni.
Mpango huo umeelezwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue mwishoni mwa wiki, akisema Serikali imekerwa na kufedheheshwa kutokana na tukio hilo lililotokea wakati wa mdahalo wa Katiba Inayopendekezwa katika Hoteli ya Blue Pearl, Dar es Salaam Novemba 2, mwaka huu.
“Kimsingi tutakachokifanya ni kupitia upya mpango wa ulinzi wa viongozi wote waliostaafu, japokuwa huwa tunafanya hivyo mara kwa mara, lakini kwa hili la Mzee Warioba tunaliangalia kwa umakini wake.
“Tumekerwa sana na tukio lile, halikutufurahisha hata kidogo kama Serikali kwa kuwa limemvunjia heshima Mzee Warioba, yule ni mzee wetu, anahitaji heshima, kwanza heshima yake na ulinzi.”

MBOWE ‘AMWAGA SUMU’ NYUMBANI KWA SITTA

Mwenyekiti wa CHADEMA freman Mbowe akiwasili Mjini urambo, Tabora.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amefanya mkutano mkubwa Urambo Mashariki na kumshutumu Mbunge wa jimbo hilo, Samuel Sitta kwa kuchakachua maoni ya wananchi katika mchakato wa Katiba Mpya.
Katika mkutano huo ulifanyika katika Uwanja wa Extended mjini hapa takriban mita 100 kutoka nyumbani kwa Sitta aliyeongoza Bunge la Katiba, Mbowe alisema historia ya nchi hii itamhukumu mbunge huyo kwa maovu hayo.
Alisema kutokana na uovu huo wa Sitta ambaye amekuwa akiisifia Katiba Inayopendekezwa kuwa itakuwa nzuri Afrika Mashariki na Kati, vyama vya upinzani vitaendelea kuidai katiba ya wananchi hata kwa miaka 100 ijayo.
Aprili mwaka huu, wabunge wa vyama vya upinzani chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), walisusia Bunge la Katiba mjini Dodoma wakilalamikia kuvunjwa kwa kanuni na kutofuatwa kwa mapendekezo ya wananchi yaliyotolewa katika Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.
Akihutubia mamia ya wafuasi wa chama hicho kwenye Operesheni Delete CCM, Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Ukawa, alisema ana uhakika Sitta ataipata hukumu hiyo ya historia kwa kile alichosema kudhulumu haki ya Watanzania milioni 45.
Mbowe anayetumia chopa katika ziara hiyo, alifika katika uwanja huo saa 11.45 na kuhutubia kwa dakika 30.
"Mzee Sitta najua upo nyumbani hapo na unanisikia, kama hunisikii basi mke wako Mama Margreth Sitta atakuwa ananisikia, lakini kama naye hayupo basi kutakuwa na wahudumu watanisikia na watakuja kukueleza," alisema huku akiwaonyesha wafuasi wa chama hicho nyumba ya Sitta iliyopo jirani na uwanja huo.
Alisema Sitta alipuuza maoni ya wananchi waliyotoa katika mchakato wa Katiba Mpya na ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba badala yake akaweka maoni ya chama chake cha CCM.
"Tunasema kwamba historia ya nchi hii itamhukumu kwa maovu aliyoyafanya kukataa maoni ya wananchi na kuweka maoni ya chama chake," alisema.
Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, alisema baada ya maoni ya wananchi kuchakachuliwa... "Sasa tutaidai Katiba Mpya hata kwa miaka 100 ijayo."
Alisema wabunge wa vyama vya upinzani walimwamini Sitta kwa kumpigia debe na baadaye walimpa kura iliyomfanya awe Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba kutokana na rekodi yake alipokuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Tulifanya hivyo kwa kumwamini kutokana na rekodi zake akiwa spika, tunajuta kumchagua hatukufahamu kwamba atatusaliti na kudhulumu haki za Watanzania," alisema Mbowe.
Chanzo:Mwananchi

Tuesday, November 4, 2014

NUSU YA WATANZANIA WAMESHUHUDIA UBAGUZI DHIDI YA WATU WENYE ULEMAVU KATIKA AJIRA

Bahadhi ya vifaa maalumu vya watu wenye ulemavu baiskeli na magongo
Nusu ya Watanzania wameshuhudia ubaguzi dhidi ya watu wenye ulemavu katika ajira
Watu binafsi na jamii kwa ujumla wanakiri kuwakosea
heshima watu wenye ulemavu
4 Novemba 2014, Dar es Salaam: Karibu nusu ya wananchi (46%) wameripoti kuwahi kushuhudia ubaguzi dhidi ya watu wenye ulemavu katika ajira. Wakati huo huo, ni wananchi wawili tu kati ya kumi (17%) waliokiri kufahamu asasi/mashirika yanayotoa upendeleo kwenye suala la kuwaajiri watu wenye ulemavu. Wananchi waliripoti kuwa miongoni mwa mashirika haya asilimia 38 ni taasisi za kiserikali. Vile vile wananchi waliripoti kuwafahamu watoto wenye umri wa kwenda shule ambao ni walemavu ila hawakuwa shuleni. Mwananchi mmoja kati ya watatu alisema anamfahamu mtoto mwenye umri wa kusoma shule ya msingi, na wawili kati ya kumi waliwajua watoto wenye umri wa kusoma shule ya sekondari lakini hawakuwa shule.
Matokeo haya yametolewa na Twaweza kwenye muhtasari wa utafiti wenye jina la Kulinda haki za kila mtu: Maoni ya wananchi juu ya ulemavu. Muhtasari huu umetokana na Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaofanyika mara kwa mara kupitia simu ya mkononi. Utafiti huu hukusanya taarifa kwenye kaya zote Tanzania Bara. Takwimu zilikusanywa mwezi Julai 2014.
Matokeo haya yameyotokana na mitazamo ya wananchi yanayoibua kwa undani ubaguzi dhidi ya watu wenye ulemavu ama moja kwa moja au kwa kupitia kukosekana kwa huduma na ajira.
Wananchi walikuwa na mtazamo ulioonesha kuwa wanawajali watu wenye ulemavu. Idadi kubwa ya wananchi (91%) waliripoti kuwa wanawaona watu wenye ulemavu kama watu wanaohitaji kutunzwa. Vile vile mwananchi mmoja kati ya watatu aliripoti kuwaona watu wenye ulemavu kama siyo watu kamili (33%) au kuwa ni watu ambao ni kikwazo kwao (32%). Karibu nusu ya wahojiwa (46%) wanawaona watu wenye ulemavu kama mzigo kiuchumi kwa familia zao na ni wananchi wanne kati ya kumi (39%) wanaowaona kama watu wenye uzalishaji mdogo kuliko watu wasio na ulemavu.
Licha ya maoni haya mkanganyiko, kuna idadi kubwa ya wananchi ambao wanawaona watu wenye ulemavu kama watu sawa na wengine (62%). Wananchi wameripoti kuwa watu wenye ulemavu wanaweza kushika nafasi za uongozi kwenye taasisi za dini (88%), biashara (87%) na jamii (85%). Aidha, wananchi sita kati ya kumi (58%) wanaamini kuwa watu wenye ulemavu wana fursa sawa na wengine.
Wananchi pia wanaunga mkono hatua zinazochukuliwa kuhakikisha fursa zinapatikana kwa watu wenye ulemavu. Walipoulizwa kuhusu viti vilivyotengwa Bungeni kwa ajili ya watu wenye ulemavu, karibu wananchi wote (97%) wanafikiri idadi iongezwe, wanaotaka viongezwe kama ilivyopendekezwa kwenye rasimu ya pili ya Katiba (29%), na wananchi (68%) wangependa viongezwe zaidi ya hapo.
Rakesh Rajani, Mkuu wa Twaweza, alibainisha: "Wananchi wengi wanawaona watu wenye ulemavu kama binadamu wasiokamilika wanaohitaji msaada. Hii haisaidii. Tunahitaji kuondokana na mtazamo huu wa kuwaona watu wenye ulemavu kama waathirika au mizigo na badala yake tuwaone kama watu wenye uwezo tofauti, wanaostahili heshima na haki ya kupata fursa sawa kama raia wengine. Hilo linahitaji hatua angalau kwenye mambo mawili: Moja, kuweka mfumo madhubuti wa kisheria ambao utaweka fursa sawa kwenye huduma zote za Serikali na biashara. Pili, kwa mashirika yanayotetea haki za watu wenye ulemavu, vyombo vya habari na wadau wengine kuwa wasisitize uwezo wa watu wenye ulemavu, na kuwapa nafasi ya kuonesha ni nini wanaweza kufanya na ni fursa zipi wanazostahili kupata ili waweze kufanya. Hii itasaidia sana, badala ya kuonesha mapungufu yao."