Monday, September 1, 2014

Mwafaka Katiba mpya waja

Rais Dr. Jakaya M. Kikwete Akiwa na viongozi wa vyama ya siasa nchini
MKUTANO wa Rais Jakaya Kikwete na viongozi wa juu wa vyama vya siasa uliofanyika jana mjini Dodoma umetajwa kuwa na dalili nzuri zinazoashiria mwafaka utapatikana juu ya mchakato wa utengenezaji Katiba mpya. Kikwete alikutana jana na vyama hivyo kupitia Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kinachoongozwa na Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo kukiwa na ajenda mbili mojawapo ikihusu mchakato unaoendelea wa kutengeneza Katiba mpya.
TCD inaundwa na vyama vyenye uwakilishi bungeni, ambavyo ni CCM, CUF, CHADEMA, TLP, NCCR-Mageuzi na UDP. Ingawa yaliyojiri ndani ya mkutano huo unaotajwa ulijaa amani na ucheshi hayakuwekwa wazi, Cheyo ambaye ni Mwenyekiti wa TCD alisema ajenda nyingine ilihusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015

No comments:

Post a Comment