Monday, September 1, 2014

Naibu Waziri wa Elimu Jenist Mhagama ahangiza kuundwa kwa madawati ya walim Nchini

Naibu waziri wa elimu Jenist Mhagama akizunguma Jambo

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenista Mhagama ameagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinatenga madawati maalumu ya kushughulikia kero za walimu ikiwamo ucheleweshaji wa mishahara.
Mhagama alitoa agizo hilo kwa nyakati tofauti mwishoni mwa wiki wakati alipofanya ziara katika Wilaya za Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani.

Naibu Wazili wa elimu Jenist Mhagama akiojiwa na Wandishi wa habari

Alikwenda kutembelea baadhi ya shule na kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo ya elimu pamoja na ujenzi unaofanyika baada ya Serikali kutoa fedha za kujenga madarasa na maabara katika shule hizo.
Mhagama alisema yako malalamiko mengi ya walimu kutotendewa vizuri wanapokwenda katika ofisi za halmashauri kufuatilia madai yao na kusema umefika wakati walimu watengewe madawati ya kushughulikia shida zao.

No comments:

Post a Comment