Wednesday, September 17, 2014

Kazi kubwa ya wapinzani ni kutoa matusi’

Katibu wa itikadi CCM Nape Nauye
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema tofauti iliyopo kati ya CCM na vyama vingine ni kwamba chama hicho tawala, kinasikiliza changamoto zinazowakabili wananchi na kuzifanyia kazi huku wapinzani kazi yao kubwa, ikiwa ni kutoa lugha za matusi.
Nape alisema hayo wilayani Rufiji wakati wa mkutano wa hadhara, uliofanyika katika jimbo la Kibiti, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana.
Alisema hayo baada ya Kinana kuwaruhusu wananchi kuuliza maswali katika mkutano wa hadhara na kuwaita watendaji, ambao walitoa majibu yaliyowaridhisha wananchi hao.
Alisema CCM inashughulika na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi na sio kutukana katika majukwaa ya siasa.
Nape waliwataka kuwa makini na vyama vya upinzani, ambavyo vimeshinda kutekeleza majukumu yao na kuwaachia matatizo wananchi.
Alitoa mfano wa mji wa Arusha, ambao awali ulijulikana kama 'Geneva ya Afrika’, lakini kwa sasa umeharibika na hata idadi ya watalii imepungua, kutokana fujo za kisiasa za mara kwa mara.
Seleman Ndubugani ambaye amewahi kuwa mfuasi wa Chadema kabla ya kurejea CCM katika mkutano huo wa hadhara, alisema wamegundua kuwapo ubabaishaji ndani ya Chadema, ikiwa ni pamoja na ubaguzi.

No comments:

Post a Comment