Wednesday, April 8, 2015

Kenya yaomba Msaada UN

Kutokana na mauajia Kenya imesema inahitaji msaada Nchi washirika wa Ulaya ili kuzuia mauaji ya halaiki nchini humo yanayofanywa na wapiganaji wa kikundi cha al-Shabaab.
hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Kenya Bi AMINA MOHAMED amesema nchi yake ilikuwa inahitaji msaada wa hatua za kiintel ejinsea na usalama kutoka kwa washirika wake.

Waziri wa mambo ya nje nchi Kenya Bi Amina Mohamed

Balozi Seif: Vijana someni.

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seif Ali Idd, amewataka vijana kusoma na kubadilika ili waweze kukabiliana na changamoto za ukosefu wa ajira kwa kuonyesha ubunifu wa akili na uwezo walionao.
Kauli hiyo imetolewa kwa niaba yake na mkuu wa mkoa kuskazinipemba Bw.Omar Khamis Othuman mara baada ya kukagua mabanda ya maonyesho ya kazi mbali mbali za vijana zikiwemo za ubunifu huko wesha katika wilaya chake chake.
Makamu wa Rais wa pili zanzibar Mh.Balozi Seif Ali Idd

Sunday, April 5, 2015

UGANDA YAANZA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA UGAIDI

Kufuatia mauaji yaliyotea katika chuo cha Garissa nchini Kenya polisi katika nchi jirani ya Uganda wamesema kuwa wamepokea habari kuwa shambulizi sawa na hilo linapangwa kufanywa nchini humo.
Mkuu wa polisi nchini Uganda Kale Kayihura amesema kuwa Al shabaab linapanga kushambulia taasisi ya elimu kwenye barabara inayounganisha mji ulio mashariki wa Jinja na mji mkuu Kampala.
"Hivyo basi vyombo vya ulinzi viko katika hali ya tahadhari kufuatia taarifa hizo," alisema Kayihura.
Mkuu wa jeshi la polisi Uganda Kale Kayihura

Kutoweka kwa amani wilayani mbinga


Msitu wa mbambi wilayani mbinga

Kumeibuka mgogoro mkubwa unaotishia amani wilayani Mbinga mkoani Ruvuma kati ya wananchi na uongozi wa halmashari ya wilaya ya Mbinga baada ya wananchi kuzuia mbao zilizokuwa zikivunwa na halmshauri hiyo kwenye msitu wa mbambi wakidai uongozi wa vijiji vinavyotunza msitu huo hauna taarifa na uvunaji huo.

Mbao zilizo ziwiwa na wananchi  wilayani mbinga

Saturday, April 4, 2015

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amemteua Rais Kikwete kuwa Mwenyekiti wa Jopo la majanga ya kiafya

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon, amemteua Rais Jakaya Kikwete kuwa Mwenyekiti wa Jopo la Ngazi ya Juu kuhusu Mwitikio wa Kimataifa wa Majanga ya Afya.

Kwa mujibu wa tangazo la uteuzi huo lililotolewa juzi, katika jukumu hilo la kimataifa, Rais Kikwete ataongoza wajumbe wengine akiwemo Delos Luiz Amorim wa Brazil, Micheline Calmy-Rey wa Switzerland, Marty Natalegawa wa Indonesia Joy Phumaphi wa Botswana na Rajiv Shah wa Marekani.

Jopo linatarajiwa kufanya kikao chake cha kwanza mapema Mei mwaka huu na linatarajiwa kuwasilisha taarifa yake kwa Katibu Mkuu wa UN mwishoni mwa Desemba, 2015.

Akizungumzia uteuzi huo, Rais Kikwete alisema amepokea kwa furaha na unyenyekevu.

“Ni majukumu makubwa na yenye changamoto nyingi, lakini dunia inahitaji tuwe na mikakati katika masuala haya ambayo ni muhimu kwa maisha ya binadamu. “Hatuna budi kufanya kazi hii na kutoa mchango wetu kwa ajili ya maisha ya wanadamu na dunia kwa ujumla,” alisema Rais Kikwete.

Rais wa Jamuri ya muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete

Mtanzania anaswa katika mauaji ya wanafunzi Kenya



Nairobi. Kenya Mtanzania mmoja ambaye hajafahamika amekamatwa kuhusiana na shambulio la kigaidi katika Chuo Kikuu cha Garissa, Kenya.
Taarifa zilizopatikana jana usiku na kutangazwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), zilieleza kuwa Mtanzania huyo anahojiwa kuwapo kwake katika eneo hilo hasa ikizingatiwa kwamba siyo mwanafunzi wala mtumishi katika chuo hicho.
Taarifa hizo zinasema kuwa Mtanzania huyo ni miongoni mwa watu wanne waliokuwa wamejificha na katika mabweni ya chuo hicho na kati yao, wawili walibainika kuwa ni wanafunzi.
Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba alipoulizwa jana kuhusu Mtanzania huyo, alisema atatoa taarifa rasmi kwa taratibu za jeshi hilo
Wauguzi wakimsaidia mmoja wa wahanga wa ugaidi wa Garissa

Mauaji Garissa:Simanzi yatanda Nairobi

Mjini Nairobi, biwi la simanzi lilitanda pale jamaa na marafiki wa wanafunzi waliouawa walipofika katika chumba cha kuhifadhia maiti kuwatambua wapendwa wao

Picha ya setlaiti ikionyesha ramani chuo cha Garissa