![]() |
Brigadia jenerali Methiew Mayela |
Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ limelaani vikali askari wake kikosi cha kiteule cha nyandoto 27 KJ makoko ambaye anadaiwa kushindwa kutii maelekezo ya askari polisi wa Usalama Barabarani wilayani Tarime na kusabisha fujo na vurugu kubwa huku polisi wakitumia risasi za moto kudhibiti hali hiyo.
Akitoa tamko hilo jeshi la wananchi wa Tanzania mbele ya waandishi wa habari mjini Musoma, mkuu wa Brigedi 202 kundi la vikosi kanda ya magharibi Brigedia jenerali Mathiew Mayela sukambi amesema kwa niaba ya mkuu wa majeshi nchini, kitendo hicho cha aibu kimefanywa na askari binafsi na siyo Jeshi la wananchi na kwamba askari huyo amekiuka kiapo chake hivyo hastahili kuendelea kuitwa mwanajeshi wa Jeshi hilo.
kuhusu Migogoro ya mipaka kati ya wananchi na vikosi vya Jeshi,mkuu huyo wa Brigedi 202 kundi la vikosi kanda ya magharibi Brigedia jenerali sukambi,amewaonya baadhi ya watu wasipeonda kuheshimu mipaka ya vikosi vya jeshi.
Aidha kiongozi huyo wa Jeshi la wananchi wa tanzania kanda ya magharibi,ametumia nafasi hiyo kuwataka wanasiasa kuacha mara moja kuingiza masuala ya siasa ndani katika utendaji wa mambo ya kijeshi.
No comments:
Post a Comment