![]() |
Wazee wasio jiweza wa mkoani manyara |
Wazee wanaoishi katika kituo cha kulea wazee wasiojiweza cha Sarame wilayani Babati mkoani manyara wamelalamikia serikali kukosa mikakati madhubuti ya kuwahudumia hali inayochangia kituo hicho kukosa chakula na kulazimika kula mlo mmoja kwa siku,huku makazi hayo yakikabiliwa na wadudu aina ya Kunguni,Mende,na Mbu hali inayowanyima usingizi na kuchangia kudhoofika kwa afya Zao.
Licha ya baadhi ya wazee hao wachache kuonyesha hali ya kukata tamaa kutokana na maradhi yanayowasumbua yakiwemo ya kupooza kwa viungo huku wengine wakishindwa kutoka nje wamesema kwa takribani miezi sita sasa wamekosa chakula cha uhakika ama mlo wanaoupata hauna kitoweo ama mboga,huku wadudu hao pia wakiwanyima usingizi.
Kufuatia kuwepo kwa changamoto ya wazee hao ,Benki ya posta imekimbiza msaada wa haraka wa chakula na matunda pamoja na vifaa vya usafi,huku ,msimamizi wa kituo hicho cha Sarame Bw Samson munuo akikiri kuwepo kwa changamoto hizo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa wahudumu.
Akikabidhi msaada huo uliokwenda sambamba na sherehe za Eid el hadji,meneja wa benki ya Posta tawi la babati Bw Charles Woiso amesema baada ya kusikia uvumi wa changamoto hizo na kuwatembelea wazee hao benki hiyo imelazimika kusaidia msaada huo ili kupunguza makali ya njaa uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 1.5 pamoja na kufanya usafi katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment