Wednesday, January 14, 2015

Mgomo wa wafanyakazi kufunga usafiri wa treni TAZARA

Treni ya abilia TAZARA
Njia kuu ya reli inayoiunganisha Zambia na Tanzania imefungwa, baada ya wafanyakazi wake kugoma wakidai malimbikizo ya mishahara ya miezi mitano ya nyuma. Kampuni inayosimamia njia hiyo TAZARA, ambayo anamilikiwa na serikali za Tanzania na Zambia, na imekuwa ikikabiliwa na uhaba wa fedha kwa zaidi ya muongo mmoja, ilisema treni zote zimesimamishwa kwa muda usiojulikana kuanzia siku ya Jumatatu. TAZARA ilisema katika taarifa kuwa kutokana na changamoto za muda mrefu za uendeshaji, hawana uwezo tena wa kukidhi gharama za uendeshaji, ambazo kwa sehemu kubwa zinahusisha manunuzi ya vipuri na ukarabati wa mabehewa na reli zake, mafuta na mishahara ya wafanyakazi. Reli ya TAZARA yenye urefu wa kilomita 1,860, ilijengwa na Wachina, ikianzia kwenye machimbo ya shaba katika eneo la Kapiri Mposhi nchini Zambia, hadi bandari ya Dar es Salaam nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment