Wednesday, January 7, 2015

CHENGE AACHIA NAFASI YA UENYEKITI KAMATI YA BUNGE

Aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge la bajeti Andrew Chenge
Kufuatia azimio la kutaka viongozi wa Bunge waliotajwa kunufaika na fedha zilizochotwa kutoka kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge, ametangaza rasmi kuachia nafasi hiyo.
Taarifa zilizopatikana katika Ofisi ndogo ya Bunge ambako vikao vya Kamati mabalimbali za Bunge vinaendelea zimethibitisha kuwa Chenge alitangaza kujiuzulu nafasi yake baada ya kamati yake kukutana kwenye ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.
Chenge aliwaambia wabunge wenzake kuwa hataki malumbano na wabunge na wala hataki msuguano wowote. Kufuatia kujiuzulu kwake, nafasi yake kwa sasa inashikiliwa na Dk. Festus Limbu, ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa kamati.

No comments:

Post a Comment