Wednesday, January 14, 2015

Mgomo wa wafanyakazi kufunga usafiri wa treni TAZARA

Treni ya abilia TAZARA
Njia kuu ya reli inayoiunganisha Zambia na Tanzania imefungwa, baada ya wafanyakazi wake kugoma wakidai malimbikizo ya mishahara ya miezi mitano ya nyuma. Kampuni inayosimamia njia hiyo TAZARA, ambayo anamilikiwa na serikali za Tanzania na Zambia, na imekuwa ikikabiliwa na uhaba wa fedha kwa zaidi ya muongo mmoja, ilisema treni zote zimesimamishwa kwa muda usiojulikana kuanzia siku ya Jumatatu. TAZARA ilisema katika taarifa kuwa kutokana na changamoto za muda mrefu za uendeshaji, hawana uwezo tena wa kukidhi gharama za uendeshaji, ambazo kwa sehemu kubwa zinahusisha manunuzi ya vipuri na ukarabati wa mabehewa na reli zake, mafuta na mishahara ya wafanyakazi. Reli ya TAZARA yenye urefu wa kilomita 1,860, ilijengwa na Wachina, ikianzia kwenye machimbo ya shaba katika eneo la Kapiri Mposhi nchini Zambia, hadi bandari ya Dar es Salaam nchini Tanzania.

Thursday, January 8, 2015

KENGE WAKAMATWA UWANJA WA NDEGE WAKITOROSHWA KWENDA NJE YA NCHI


Kamanda wa Polisi wa JNIA, Khamis Suleiman ametaarifu kuwa Jeshi la Polisi linamshikilia raia wa Kuwait, Hussain Ahmed Ally Mansour (34) baada ya na viumbe hai aina ya Kenge 149 akiwa tayari kuwasafirisha kuelekea nchini Kuwait kupitia Dubai na Shirika la Ndege la Emirates.
Kamanda Selemani alisema Mansour alikamatwa na kenge hao akiwa amewaweka kwenye mifuko midogo midogo ilivyowekwa katika begi kubwa lenye rangi nyeusi.

Wednesday, January 7, 2015

Viongozi wa kisiasa wamta Rais Kikwete achukue hatua kwa waziri wa nishati Prf.Muhongo

Viongozi wa Umoja wa Ukawa
Viongozi wa vyama vya siasa nchini wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kutekeleza ahadi yake aliyoahidi wakati wa mkutano na wazee wa Dar es Salaam ya kufanya maamuzi ya kumwajibisha waziri wa nishati na madini ambaye alimweka kiporo na kudai kuwa atatoa maamuzi ndani ya siku mbili lakini hadi leo amekaa kimya.

Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Prof Iibrahim Lipumba amesema suala la viongozi wakiwemo mawaziri kuwajibika halikuanza leo hasa anaposhindwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kuisababishia serikali hasara au kushusha heshima ya taifa hivyo ni vyema uwajibikaji ukawa ni kwa kila mtumishi wa umma bila kubagua ili kuleta tija kwa taifa

Kwa upande wake mjumbe wa halmashauri kuu taifa ya chama cha mapinduzi CCM Bw Najim Msenga amesema niimani ya chama chake kuwa rais atafanya maamuzi sahihi kwa maslahi ya taifa kama alivyoahidi na kwamba suala hilo haliwezi kuathiri uhai wa CCM kwani bado iko imara baada ya baadhi ya watuhumiwa kuchukuliwa hatua.

Akizungumzia suala hilo katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Dk Willbroad Silaa amesema hata hao waliojiuzulu na kuenguliwa uteuzi wao maadam uchunguzi ulifanywa na vyombo sahihi hadi kufikia hatua ya kupelekwa bungeni na kujadiliwa na wao kutoa maazimio watuhumiwa wote hadi sasa walipaswa wawe wamefikishwa mahakamani.

Katika mkutano wake na wazee wa Dar es Salaam uliofanyika ukumbi wa Diamond Jublee desemba 22 mwaka jana Rais Kikwete alitengua uteuzi wa aliyekuwa waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh Anna Tibaijuka na kutangaza kumweka kiporo waziri wa nishati na madini Prof Muhongo

CHENGE AACHIA NAFASI YA UENYEKITI KAMATI YA BUNGE

Aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge la bajeti Andrew Chenge
Kufuatia azimio la kutaka viongozi wa Bunge waliotajwa kunufaika na fedha zilizochotwa kutoka kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge, ametangaza rasmi kuachia nafasi hiyo.
Taarifa zilizopatikana katika Ofisi ndogo ya Bunge ambako vikao vya Kamati mabalimbali za Bunge vinaendelea zimethibitisha kuwa Chenge alitangaza kujiuzulu nafasi yake baada ya kamati yake kukutana kwenye ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.
Chenge aliwaambia wabunge wenzake kuwa hataki malumbano na wabunge na wala hataki msuguano wowote. Kufuatia kujiuzulu kwake, nafasi yake kwa sasa inashikiliwa na Dk. Festus Limbu, ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa kamati.

Askari wa jeshi la polisi ajiua kwa kujipiga risasi ya Mdomoni Mkoani Mbeya.Kamanda wa

Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya
Askari wa jeshi lapolisi, Sajenti Patrick Kondwa amejiua kwa kujipiga risasi akiwa katika ofisi yake kwenye ghala lakuhifadhia silaha katika kituo cha polisi cha wilaya ya mbozi mkoani mbeya.
Akizungumza na ITV kwanjia ya simu, kamanda wa polisi mkoawambeya amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika na kwamba jeshi lapolisi linaendelea na uchunguzi wa tukiohilo.
 
Sajenti Patrick mwenye umri wamiaka 54 ,akiwa katika ofisi yake kwenye chumba cha kuhifadhia silaha katika kituo cha polisi cha wilaya ya mbozi amejipiga risasi mdomoni ambayo imetokea kisogoni na kuondoka na uhai wake, tukio ambalo limetokea majira ya saa tisa usiku na kuthibitishwa na kaimu mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo, ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya ileje, Rosemary Staki Senyamule.
 
Baadhi ya waombolezaji ambao wamezungumza na ITV  wamesema kuwa wamepokea msiba huo kwa masikitikomakubwa hasa kwa kuzingatia kuwa Sajenti Patrick alikuwani askari mwadilifu na anayeipenda kazi yake.

Tuesday, January 6, 2015

UAPISHAJI WA WENYEVITI SERIKALI ZA MITAA DAR VURUGU TUPU

Askari polisi wakijitawanya ili kudhibiti vurungu zilizo tokea wakati wa kuapishwa kwa viongozi wa mitaa
Polisi Jijini Dar es Salaam wamelazimika kufyatua risasi hewani na kufyatua mabomu ya machozi kufuatia kuibuka kwa vurugu katika hoteli ya Land Mark ambapo shughuli ya uapishaji wa wenyeviti wa serikali Mitaa zinafanyika.
Vurugu hizo, zimeibuliwa na kambi ya upinzani ambayo imelalamikia kuwa Mwenyekiti mmoja wa Chama tawala CCM aliyeapishwa hakuwa ameshinda katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uliofanyika mwaka jana

Saturday, January 3, 2015

RAIS ATEUA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI MPYA.

Mwanasheria mkuu wa Serikali Bw.George Mcheche Masaju
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Uteuzi wa Bwana Masaju ulianza jana, Ijumaa, Januari 2, 2015 na ataapishwa keshokutwa, Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bwana Masaju pia amepata kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

PANYA ROAD" 36 WATIWA MBARONI NA POLISI DAR

Msemaji wa jeshi la polisi SSP ADVERA BULIMBA
Jeshi la polisi nchini linawashikilia vijana 36 wa kundi maarufu Panya Road wanaodaiwa kufanya vurugu na kupora mali za watu na kusababisha taharuki katika jiji la Dar es salaam huku baadhi ya wananchi wakitoa maoni tofauti kuhusiana na tukio hilo.
Akitoa ufafanuzi wa taharuki hiyo msemaji wa jeshi la polisi SSP ADVERA BULIMBA ambaye mbali na kuwatoa hofu wananchi kuwa hali hiyo haitajitokeza tena amesema jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana na vikundi vyovyote vinavyotaka kuvuruga amani ya nchi.
Pia amesema kwamba endapo polisi wasingewadhibiti vijana hao mapema tangu wakiwa makaburini baada ya kumzika mwenzao aliyeuawa na wananchi baada ya kuiba hali ingekuwa mbaya zadi.
Kufuatia tukio hilo baadhi ya wananchi wa maeneo ya Magomeni ambako vurugu zilianzia wameelezea namna zilivyoanza hadi kusababisha watu kuanza kukimbia hovyo na wengine kuacha maduka yao wazi na taarifa kusambaa maeneo mengine.
Katika maeneo ya Mwananyamala na Ubungo baadhi ya waliozungumzia sakata hilo wameitaka serikali kuangalia makundi ya vijana na ikiwezekana wapatiwe elimu ya ujasiriamali bure ili waweze kuendesha maisha.
Wananchi wengine wameshauri vijana wasiokuwa na kazi mitaani wapelekwe jeshini wakafundishwe stadi za kazi pamoja na uzalendo ili kuepuka vitendo hivyo.
Taharuki hiyo ilitokea usiku wa tarehe 2 Januari, 2014 chanzo kikiwa ni kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la MOHAMED AYUB kuuawa na wananchi tarehe mosi mwaka huu katika maeneo ya Tandale kwa Mtogole kwa tuhuma za wizi ambapo tarehe 2 maziko yalifanyika na taarifa zilizolifikia jeshi la polisi zilidai kuwa baada ya maziko vijana wenzake walijipanga kufanya fujo ili kulipiza kisasi.