Sakata la Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu kudaiwa kudanganya umri,
limeingia katika sura mpya baada ya Baraza la Sanaa Tanzania (Basata)
kueleza kuwa linasubiri uchunguzi ukamilike na litamvua taji hilo endapo
itabainika kweli alichakachua umri wake.
Kwa kumuangalia mrembo huyu, unahisi kweli atakuwa kadanganya umri wake?
Aliyekuwa
staa wa muziki kutoka kundi la TMK Wanaume Family, Yessaya Ambilikile
Mwakalekamo aka YP ameagwa jana katika viwanja vya TCC Chan’gombe na
kuzikwa makaburi ya Chang’ombe Dar es Salaam
Hizi ni picha mbalimbali wakiwemo na mastaa wa Bongo Fleva na Bongo Movie
Makasisi wanaoshiriki katika mkutano wa maaskofu wanaangazia masuala ya mafunzo ya kanisa katoliki kwa familia ,wametoa mwito kwa kanisa hilo duniani kuwachukulia watu wenye mapenzi ya jinsia moja kwa usawa
Kauli hii inakuja baada ya Maaskofu kuandika ripoti wakati wa mkutano wa synodi ukiendelea huko Vatican na kusema kuwa wapenzi wa jinsia moja wana zawadi na viwango vya kutoa kwenye jumuiya za kikristo hii ikiwa ni ripoti iliyotolewa mapema wiki hii.
Ripoti hiyo haitoi changamoto yoyote kwa msimamo wa muda mrefu wa kanisa hilo juu ya kupinga ndoa za jinsia moja,lakini baadhi ya vikundi vya kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja wanachukulia kauli hiyo kuwa ya mafanikio makubwa kwa jamii zao.
Na moja ya makundi yenye kushikilia msimamo mkali kikanisa wametupilia mbali ripoti hiyo na kuuita ya kisaliti.
Zaidi ya maaskofu 200 wa kanisa katoliki wanakutana kwenye mkutano wa synodi tangu mapema mwezi huu,katika mkutano huo ni papa Francis aliyetoa mwito wa kujadili masuala ya utoaji wa mimba,vidonge vya uzazi wa mpango,mapenzi ya jinsia moja na talaka.
Papa Francis amewataka viongozi wa juu wa kanisa hilo kuzingatia Zaidi suala la wapenzi wa jinsia moja chanya kuliko kuwa kinza na amefanikiwa kuwateka maaskofu wanaohudhuria mkutano huo wa sinodi.
Mwaka uliopita katika ripoti aliyo itoa papa Francis kuhusiana na mwenendo wa kanisa katoliki kuwa waumini walio wengi waliliacha mkono kanisa hilo kutokana na mafunzo yahusianayo na ngono na dawa za uzazi wa mpango.
Papa huyo anazichukulia ndoa hizo za jinsia moja kama zisizo na utaratibu akiinukuu ripoti ya kanisa katoliki iliyochapishwa mwaka 1986,wakati Papa Francis alipokua mshauri mkuu wa masuala ya teolojia ya kanisa katoliki wa hayati papa John Paul wa pili.
Nguvu kubwa ya vikundi vya kutetea haki za watu wenye mapenzi ya jinsia moja ni juu ya kauli ya papa Francia aliyoitoa mwishoni mwa mwaka wa jana alipokuwa kwenye kambi ya vijana wa kanisa hilo huko Rio de Jeneiro alitoa kauli kua kama mtu anamtafuta Mungu na ana nia njema ,yeye ni nani wa kuhoji?
Papa Francis anaingia katika historia ya kanisa katoliki ulimwenguni kutumia jina (hasha kum si matusi) WASENGE hadharani kuliko kutumia neno wapenzi wa jinsia moja.
Wazee wanaoishi katika kituo cha kulea wazee wasiojiweza cha Sarame wilayani Babati mkoani manyara wamelalamikia serikali kukosa mikakati madhubuti ya kuwahudumia hali inayochangia kituo hicho kukosa chakula na kulazimika kula mlo mmoja kwa siku,huku makazi hayo yakikabiliwa na wadudu aina ya Kunguni,Mende,na Mbu hali inayowanyima usingizi na kuchangia kudhoofika kwa afya Zao.
Licha ya baadhi ya wazee hao wachache kuonyesha hali ya kukata tamaa kutokana na maradhi yanayowasumbua yakiwemo ya kupooza kwa viungo huku wengine wakishindwa kutoka nje wamesema kwa takribani miezi sita sasa wamekosa chakula cha uhakika ama mlo wanaoupata hauna kitoweo ama mboga,huku wadudu hao pia wakiwanyima usingizi.
Kufuatia kuwepo kwa changamoto ya wazee hao ,Benki ya posta imekimbiza msaada wa haraka wa chakula na matunda pamoja na vifaa vya usafi,huku ,msimamizi wa kituo hicho cha Sarame Bw Samson munuo akikiri kuwepo kwa changamoto hizo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa wahudumu.
Akikabidhi msaada huo uliokwenda sambamba na sherehe za Eid el hadji,meneja wa benki ya Posta tawi la babati Bw Charles Woiso amesema baada ya kusikia uvumi wa changamoto hizo na kuwatembelea wazee hao benki hiyo imelazimika kusaidia msaada huo ili kupunguza makali ya njaa uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 1.5 pamoja na kufanya usafi katika eneo hilo.
Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ limelaani vikali askari wake kikosi cha kiteule cha nyandoto 27 KJ makoko ambaye anadaiwa kushindwa kutii maelekezo ya askari polisi wa Usalama Barabarani wilayani Tarime na kusabisha fujo na vurugu kubwa huku polisi wakitumia risasi za moto kudhibiti hali hiyo.
Akitoa tamko hilo jeshi la wananchi wa Tanzania mbele ya waandishi wa habari mjini Musoma, mkuu wa Brigedi 202 kundi la vikosi kanda ya magharibi Brigedia jenerali Mathiew Mayela sukambi amesema kwa niaba ya mkuu wa majeshi nchini, kitendo hicho cha aibu kimefanywa na askari binafsi na siyo Jeshi la wananchi na kwamba askari huyo amekiuka kiapo chake hivyo hastahili kuendelea kuitwa mwanajeshi wa Jeshi hilo.
kuhusu Migogoro ya mipaka kati ya wananchi na vikosi vya Jeshi,mkuu huyo wa Brigedi 202 kundi la vikosi kanda ya magharibi Brigedia jenerali sukambi,amewaonya baadhi ya watu wasipeonda kuheshimu mipaka ya vikosi vya jeshi.
Aidha kiongozi huyo wa Jeshi la wananchi wa tanzania kanda ya magharibi,ametumia nafasi hiyo kuwataka wanasiasa kuacha mara moja kuingiza masuala ya siasa ndani katika utendaji wa mambo ya kijeshi.
Katika tukio hilo ambalo lilitokea oktoba mosi mwaka huu majira ya saa kumi na moja jioni eneo la kituo cha mabasi mjini tarime, raia mmoja na askari kadhaa wa jeshi la polisi wakiongozwa na mkuu wa upelekezi wa makosa ya jinai (RCO) kanda maalum ya Tarime Rorya pamoja na askari wawili wa Jeshi la wananchi walijeruhiwa kwa risasri wakati wa kuzima vurugu hizo.