 |
Rais wa uganda Yoweri Museveni |
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ameyataka mataifa ya Afrika kujitoa katika mkataba unaounda mahakama ya kimataifa ya uhalifu – ICC, kwa kile anachodai kuwa taasisi hiyo ya kimataifa inawalenga waafrika isivyo haki.
 |
Jengo la mahakama ya kimataifa ICC |
Akiongea katika kilele cha maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa kenya zilziofanyika mjini Nairobi, Rais Museveni amesema atawasilisha mswaada katika kikao kijacho cha Umoja wa Afrika ili mataifa yote wanachama wa au yajiondoe katika mkataba huo wa ICC na kuwaachia magharibi wabakie humo.
 |
Nembo ya mahakama ya kimataifa ICC ikionyesha usawa |
Akizungumza kwa hamasa rais Museveni amesema awali alikuwa akiiunga mkono ICC kwa vile anaheshimu nidhamu na kutaka kila mmoja awajibishwe kwa makosa yake, lakini taasisi hiyo imegeuka ni chombo cha kuikandamiza afrika na kusema kwa maneno sitafanya kazi nao tena.
 |
Rais wa Kenya Uhuru Kenyata |
Waendesha mashtaka wa icc hivi karibuni walimfutia mashtaka Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta lakini naibu wake bado anaendelea kukabiliwa na mashtaka katika mahakama hiyo.
.jpg) |
Rais Kenyatta akiwa mahakama ya kimataifa ICC akifatilia kesi iliyokuwa inakabili |
No comments:
Post a Comment