Sunday, December 14, 2014

Serikali ya awamu ya nne kumaliza vibaya’


Rais wa Tanzania awamu ya nne Dr. Jakaya Mrisho Kikwete
Dar es Salaam. Wakati Serikali ya Awamu ya Nne imebakiza takriban mwaka mmoja kuondoka madarakani, sifa ya Tanzania kwenye jumuiya ya kimataifa imeendelea kutiwa doa kutokana na kuhusishwa na ongezeko la ufisadi wa mabilioni ya fedha za umma na ujangili.
Kutokana na hali hiyo, huenda uongozi wa awamu hiyo iliyo chini ya Rais Jakaya Kikwete ikaiacha nchi vibaya na historia ya pekee ya kuwapo kwa ‘mikwaruzano’ kati yake na wafadhili mbalimbali wanaoelezwa kutoridhishwa na namna fedha za umma zinavyochotwa na wajanja wachache wakiwamo viongozi wa umma.

Marekani
Juzi, Balozi wa Marekani nchini, Mark Childressi alieleza kuwa nchi yake haitatoa fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Milenia (MMC) kwa Serikali ya Tanzania, hadi itekeleze maagizo ya Bunge kuhusu uchotwaji wa fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow. Kauli ya kiongozi huyo imedhihirisha ukubwa wa tatizo hilo, ingawa Ikulu imeshasema haitekelezi maagizo kwa shinikizo la misaada.

Museveni ayataka mataifa ya Afrika yajitoe ICC




Rais wa uganda Yoweri Museveni
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ameyataka mataifa ya Afrika kujitoa katika mkataba unaounda mahakama ya kimataifa ya uhalifu – ICC, kwa kile anachodai kuwa taasisi hiyo ya kimataifa inawalenga waafrika isivyo haki.
Jengo la mahakama ya kimataifa ICC
Akiongea katika kilele cha maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa kenya zilziofanyika mjini Nairobi, Rais Museveni amesema atawasilisha mswaada katika kikao kijacho cha Umoja wa Afrika  ili mataifa yote wanachama wa au  yajiondoe katika mkataba huo wa ICC na kuwaachia magharibi  wabakie humo.
Nembo ya mahakama ya kimataifa ICC ikionyesha usawa
Akizungumza kwa hamasa rais Museveni amesema awali alikuwa akiiunga mkono ICC kwa vile anaheshimu nidhamu na kutaka kila mmoja awajibishwe kwa makosa yake, lakini taasisi hiyo imegeuka ni chombo cha kuikandamiza afrika  na kusema kwa maneno sitafanya kazi nao tena.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyata
Waendesha mashtaka wa icc hivi karibuni walimfutia mashtaka Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta lakini naibu wake bado anaendelea kukabiliwa na mashtaka katika mahakama hiyo.
Rais Kenyatta akiwa mahakama ya kimataifa ICC akifatilia kesi iliyokuwa inakabili

Wednesday, December 3, 2014

Wanafunzi 826 na walimu wao wakimbia vita Kiteto

Mkoa wa Manyara na wilaya zake
Siku kadhaa zimepita tangu kutokea kwa mapigano mapya kati ya wakulima na wafugaji katika Wilaya ya Kiteto, mkoani Manyara.
Ni Alhamisi mchana, siku ambayo kwa kawaida ni ya masomo, lakini kimya kimetawala katika kijiji kizima cha Chekanao na Ilera huku sauti za ndege zikishamiri.
Makundi ya vijana na wakulima yanaonekana yakijadiliana na mbali yalipo makundi haya, vijana wa Kimasai nao wanaonekana wakiwa wametulia na fimbo zao.
Katika shule iliyopo kijijini hapo, polisi wametanda na silaha zao wakizungukazunguka. Anajitokeza mwalimu anayejitambulisha kwa jina la Paulo Sulle.
Akiwa bado na hofu anajitambulisha kuwa yeye ndiye mwalimu mkuu msaidizi wa Shule ya Msingi Chekanao.
Namuuliza kwa nini Alhamisi ambayo ni siku ya masomo, hakuna hata mwanafunzi mmoja darasani? Anajibu shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 526,lakini wote wamekimbia mapigano ya kugombea ardhi kati ya wakulima na wafugaji.

CAG Mpya Profesa Mussa Assad uwakondesha waliohusika na ESCROW asema moto ni uleule

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof.Mussa Assad
Dar es Salaam. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mpya, Profesa Mussa Assad amesema ataanza kazi kwa moto uleule ulioachwa na mtangulizi wake, Ludovick Utouh aliyestaafu.
Akizungumza jana mara baada ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete Ikulu, Profesa Assad aliyeteuliwa Novemba 5 kushika wadhifa huo alisema: “Ninasubiri niingie ofisini nianze kazi… nitaendeleza yote yaliyoachwa na mwenzangu, sitatoka nje ya mstari.”
Profesa Assad alisema yuko tayari kusimamia utendaji kazi wa kisasa kwa kusimamia misingi ya ofisi yake, ili kulinda hadhi na heshima aliyopewa na Rais katika uteuzi huo.
Kuhusu Ripoti ya Akaunti ya Escrow, Profesa Asaad alisema anasubiri kukabidhiwa rasmi taarifa hiyo na maagizo yote yaliyotolewa na Bunge kwa ajili ya kutekeleza yale yaliyopo chini ya ofisi yake na kuendeleza yale ambayo yalishaanza kutekelezwa.