Sunday, October 4, 2015

MWANASIASA MKONGWE KINGUNGE GOMBALI MWERU AACHANA NA CCM

kINGUNGE AKIZUNGUMZA  NA WAHANDISHI WA HABARI  NYUMBANI  KWAKE
 Kingunge amevua rasmi uanachama wa CCM na amesema sababu ya kujitoa CCM ni kutoridhishwa na mwenendo wa chama hicho kwasasa na hatojiunga na chama kingine ila yuko upande wa mabadiliko
Kingunge- "Kila unapopita vijana,kinamama, na watanzania wote wanataka mabadiliko na mimi niko upande wa mabadiliko na yaje haraka"
Kingunge- "Wanabadilisha kibwagizwo toka kidumu 'chama cha mapinduzi' hadi 'kidumu chama tawala', hapo ni kung'ang'ania madaraka"
Kingunge- "Baada ya kukaa madarakani muda mrefu chama cha CCM hakiwezi kufanya jipya, chama kikikaa nusu karne hakina jipya tena"
Kingunge- "Mabadiliko ni muhimu kweli kweli, upate watu wengine wenye pumzi mpya, mnataka mbakie nyinyi tu, nyie pumzi imekwisha"
Kingunge -" Sisemi chama hiki cha zamani kisifanye kazi, kiwekwe kando kwa muda, CCM imeacha kujadili issues sijui wanajadili nini"
Kingunge- "Wanaotaka tuondoke hapa twende mbele lazima watu wapya waongoze, lazima fikra mpya ziongoze".
Kingunge- "Tumefika mahali pagumu sana, nguvu ya kupinga mabadiliko ni kubwa ila kwa utafiti wangu nguvu ya wanaotaka mabadiliko ni kubwa zaidi hivyo msiogope" amemalizia kwa kusema hayo
KINGUNGI  AKISIKILIZA SWALI  KUTOKA KWA WANAHABARI

Wednesday, September 30, 2015

Dawa za kupunguza makali ya UKIMWI kuwa ghali zaidi Duniani

Dawa za kupunguza makali ya UKIMWI
Shirika la Afya duniani WHO limetoa muongozo mpya kuhusiana na matibabu ya watu walioambukizwa virusi vinavyosababisha UKIMWI.
Awali ilibidi walioambukizwa wasubiri hadi waanze kuwa wagonjwa kabisa kabla ya kuanza kutumia tembe za kupunguza makali ya ukimwi.
Hoja kuu ni kuwa bei ya dawa imeongezeka maradufu.
Je mataifa maskini ya Afrika yatamudu ongezeko la idadi ya watu ambao wanahitaji ya dawa za kupunguza makali ya Ukimwi ?

Tuesday, June 2, 2015

Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter atangaza kuwa atajiuzulu.

Rais wa FIFA Sepp Blatter
Akitangaza kujiuzulu,kwake Sepp Blatter mwenye umri wa miaka 79 ameitisha kikao cha dharura mara moja ili kumchagua rais mpya.
Blatter alichaguliwa tena wiki iliopita licha ya maafisa wake saba wakuu kukamatwa siku mbili kabla ya uchaguzi .
Lakini alisema kuwa mamlaka yake hayaungwi mkono na kila mtu.Shirikisho la FIFA lilikumbwa na mgogoro wa kukamatwa kwa maafisa wake kutokana na mashtaka ya ufisadi ikiwa ni miongoni mwa mashtaka yaliofunguliwa na marekani .
Uchunguzi mwengine unaofanywa na serikali ya Switzerland kuhusu vile michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2018 na 2022 ilitolewa pia unaendelea.''Nimehusika sana na FIFA na maslahi yake.Kilicho muhimu kwangu ni taasisi ya FIFA na Soka duniani''.

Friday, May 8, 2015

Miili ya wanajeshi liouwawaDRC yaludishwa nchini


Jeshi la umoja wa mataifa linalolianda amani kaskazini mashariki mwa nchi ya kongo DRC wameanza harakati za kusafirisha miili ya askari wawili wa kitanzania kuja kuzikwa nyumbani baada ya kuuwawa katika shambulio la kigaidi huko beni.


SHERIA YA MAKOSA YA MITANDAO TAYARI IMESAINIWA NA RAIS.

Rais wa Jamuhuri ya muungano Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete 

Rais Jakaya Kikwete tayari ameshasaini sheria yenye utata ya makosa ya mtandao na muda wowote kuanzia sasa itaanza kutumika rasmi.
Hivi ni baadhi ya vipengele vilivyozua utata katika sheria hiyo
1. Kifungu 7 (2b): Mpokeaji wa ujumbe (receiver) anaweza kushtakiwa kwa kosa la kupokea ujumbe ambao sheria imeufanya kuwa wa jinai. (Mfano: Mtu akikuforwadia ujumbe, ukiupokea na wewe umefanya kosa la jinai).
2. Kifungu 8: Itakuwa ni kosa la jinai kama mtu ataweka wazi nyaraka za siri za serikali hata kama ni nyaraka ya kusaidia nchi kwa ujumla (Mfano: Matumizi mabaya ya mali ya umma).
3. Kifungu 14: Picha yoyote yenye mwelekeo unaoweza kuonekana kama ‘mchafu kingono’ inaweza kupelekea mtu kufungwa hadi miaka 10 au kulipa milioni 30; Sasa kama mtu kaposti picha yake ambayo sio ya ponografia lakini ‘ikatafsiriwa’ hivyo. Sheria haijatafsiri ponografia!
4. Kifungu 23: Je, ulijua kuwa ‘kusababisha maudhi ya hisia’ kwa mtu mwingine ni unyanyasaji na unaweza kufungwa kifungo kisichopungua mwaka mmoja?
5. Rejea adhabu ya ibara mbalimbali: Sheria hii kila kosa linaweza fanya mtu afungwe kifungo hadi cha maisha na kulipa pesa hadi zisizohesabika kwani hakijawekwa kikomo cha juu cha adhabu bali kikomo cha chini tu kwa Kiingereza “not less than”
6. Sheria haijaeleza vizuri suala la kutumia jina lisilo lako kwenye mtandao na hivyo mtu anaweza kushitakiwa kama kuna mtu mwingine mwenye jina kama hilo katika maisha halisi.
7. Serikali kupitia waziri husika ndio ina mamlaka ya kusema jambo lililowekwa kwenye mtandao ni la kweli, uongo au la kupotosha. Kumbuka hata ESCROW, EPA walisema ni uwongo; ni wangapi katika mtandao wangeshtakiwa kiuonevu kwa hili?
8. Kifungu 22: Ukiweka ujumbe katika mtandao na ukaufuta au kuuboresha, kama ukishtakiwa kwa kuweka ujumbe huo unaweza kuhukumiwa pia kwa adhabu ya kuuboresha au kuufuta. Ni mara ngapi unafuta ‘status’ zako za WhatsApp? Unaweza shtakiwa kwa kuchelewesha ushahidi kisa tu ulifuta na hamna mtu anayeweza kujua ulifuta kwa kusudi au la.
9. Mkuu wa kituo cha Polisi chochote kile nchini anaweza kuagiza wewe umpatie simu/laptop yako au taarifa zako zote (kwenye email, chats) au hata vifaa vyako au ofisi yako kwa ajili ya upelelezi bila oda ya Mahakama.

Thursday, April 23, 2015

Wanajeshi wa Rwanda wadaiwa kuingia DRC

Jeshi la Rwanda likiwa kwenye moja ya onyesho lake
Msemaji wa Serikali ya DRC Lambert Mende anasema kuwa majeshi wanajeshi wa Rwanda wameonekana nchin humo katika hifadhi ya wanyama ya virunga,kilometa 120 kaskazini mwa Goma mji mkuu katika mkoa wa kivu kaskazini,hatahivyo majeshi ya DRC yalifyatua risasi za kutoa onyo, ambapo wanajeshi wa Rwanda nao walijibu kwa risasi na kumjeruhi mwanajeshi mmoja Mkongomani.
    hata hivyo kisa hicho kilikanushwa kupitia mtandao wa Twitter na naibu mwakilishi wa Rwanda katika Umoja wa Mataifa, aliyesema kuwa madai hayo ni upuzi mtupu.
    Rwanda imekosoa Serikali ya DRC na Ubalozi wa Umoja wa Mataifa nchini kwa kukosa kushughulikia kikamilfu maswala yanayohusu kundi la waasi la Democratic Forces for the Liberation of Rwanda, kundi la waasi kutoka Kabila la Wahutu ambalo limekuwa Congo kwa zaidi ya miaka 20.
  Mara kadhaa siku zilizopita Rwanda imewahi kuyatuma majeshi yake kukabiliana na waasi nchini DRC.

IGP apiga marufuku vikundi vya ulinzi vya vyama vya siasa


IGP Ernest Mangu
Mkuu wa jeshi la Polisi nchi IGP Ernest Mangu amepiga marufuku vikundi vya ulizi vya vyama vya siasa nchini ambavyo vina muonekano na muundo wa vyombo vya ulizi na usalama,

Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumalizaka kwa mkutano wa baraza la vyama vya siasa Jijini  Der es salaam jana,Ofisi ya vyama vya siasa na jeshi la polisi uliokuwa ukijadiliwa namna ya kuondoa vikundi hivyo au kuboresha shughuli za vikundi hivyo ambavyo vinamilikiwa na vyama vya siasa ambavyo ni CCM (Green Guard), CHADEMA (Red Brigade), CUF (Blue Guard), na ACT-WAZALENDO (Amani)

    IGP amesema wamejadiliana na vyama vyote vya siasa vinavyounda vikundi hivyo na Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchi iliyo chini ya Jaji Francis Mtungi itatoa muongozo ambao utatakiwa kufuatwa kwa utekelezaji ili waweze kufanya kazi zao kwa utaratibu unao takiwa bila kuathiri sheria ya nchi na katiba inayo ziwia kuundwa kwa vikundi vyovyote vya ulizi.