Polisi nchini Uganda wanawafanyia uchunguzi
nguruwe wawili kuhusiana na "ugaidi" baada ya wanyama hao kuingia katika
eneo la bunge.
Taarifa zinasema nguruwe hao watoto walikuwa wamepakwa rangi za chama tawala na kubebeshwa mabango yanayowatuhumu wabunge kwa ufisadi.
Watu wawili wanaoshukiwa kutekeleza tukio hilo wanashikiliwa na polisi wakisubiri kuburuzwa mahakamani mjini Kampala.
Askari polisi kadhaa wamesimamishwa kazi kufuatia tukio hilo na
wanakabiliwa na mashtaka ya kuzembea kazi, amekaririwa msemaji Polly
Namaye na shirika la habari la AFP.
Msemaji huyo amesema nguruwe hao wanafanyiwa uchunguzi wa "kigaidi" kama ulivyo utaratibu.
No comments:
Post a Comment