Picha
za video zimeonesha mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez akimng'ata beki
wa Italy Giorgio Chiellini. Mwamuzi hakuona kitendo hicho lakini huenda
hatua zitachukuliwa baadaye.
Tuesday, June 24, 2014
Sunday, June 22, 2014
NGURUWE MBARONI UGANDA KWA "UGAIDI"
Polisi nchini Uganda wanawafanyia uchunguzi
nguruwe wawili kuhusiana na "ugaidi" baada ya wanyama hao kuingia katika
eneo la bunge.
Taarifa zinasema nguruwe hao watoto walikuwa wamepakwa rangi za chama tawala na kubebeshwa mabango yanayowatuhumu wabunge kwa ufisadi.
Watu wawili wanaoshukiwa kutekeleza tukio hilo wanashikiliwa na polisi wakisubiri kuburuzwa mahakamani mjini Kampala.
Askari polisi kadhaa wamesimamishwa kazi kufuatia tukio hilo na wanakabiliwa na mashtaka ya kuzembea kazi, amekaririwa msemaji Polly Namaye na shirika la habari la AFP.
Msemaji huyo amesema nguruwe hao wanafanyiwa uchunguzi wa "kigaidi" kama ulivyo utaratibu.

Alikiba: Sina bifu na Diamond lakini alinikosea na nikaumizwa na nilisha samehe
Msanii Alikiba ameamua kufungaka na kuweka waZi kili kinacho hitwa
tofauti au bifu kati yake na Msanii Diamond!Kwanza lazima tukubaliane
kuwa ALikiba ni mmoja wa Wasanii wasio penda maneno na malumbano na
wasanii wenzie ndio maana hukaa kimya. Kwanza Alikiba alisema hana bifu
na diamond na hana sababu ya kuwa na bifu nae japo yanayo ongelewa yana
muumiza sana na aliamua kuondokana na hayo yote busara ya haraka ilikuwa
kukaa kimya.
Aliendelea kusema aliumizwa sana aliposikia kuwa amefuta mistari ya
diamond kwenye wimbo wa Single boy ambao aliimba na lady jaydee na
hakuimba kabisa na diamond na hata producer aliye record wimbo huo
alithibitisha. Aliendelea kusema kuwa aliumizwa sana na uongo huo kuhusu
yeye na hakupenda kuuongelea sana kwa sababu ange onekana anatafuta
kick wakati hakuKuwa na kitu kama hicho.
Pia Alikiba aliamua kusema kuwa aliumizwa sana na kitendo cha Diamond
kufuta mistari yake kwenye wimbo wa Lala salama maana Diamond
hakumwambia kwanini kafanya hivyo na hadi leo hakuwai kumwambia. Alisema
hilo swala amechukulia kama na Kitendo cha mtu kuomba mtihani wako
aangalizie alaf baadae ana kurudishia mtihani wako na kusema sitaki
majibu yako au ana yafuta yote alaf unategemea atajisikiaje? na alisema
yeye alisha samehe lakini Diamond alimkosea na hadi leo hawakuwai
kukutana.
Ameweka wazi kuwa aliamua kuwa kimya ili watu waongee lakini hana tatizo
na Diamond. Katika hili sikuona sababu ya Diamond kutomwambia Alikiba
kuwa wimbo naufanya upya na nimetoa mistari yako maana sikuipenda na
nimeamua kuimba mwenyewe.
Saturday, June 14, 2014
Kwa Mara ya Kwanza Baada ya Muda Mrefu Jack Wolper Anaswa Live Live Ndani ya Malavidavi
Jack Wolper na Mpenzi Gee anayedaiwa wa Rafikie
KABANG! Baada ya kutoonekana katika pozi za kimahaba kwa muda mrefu, kwa
mara ya kwanza, staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe
‘Gambe’ amenaswa ‘live’ na mwanaume anayedaiwa kuwa ni mume wa mtu,
Kwa muda mrefu Wolper amekuwa makini na picha zake za kimahaba tangu
alipokuwa akitoka kimapenzi na mfanyabiashara maarufu jijini Dar,
Abdallah Mtoro ‘Dallas’.
CHANZO CHAMWAGA MTONYO
Awali, chanzo makini kilipenyeza habari kuwa kuna mawasiliano yamenaswa
‘kimafia’ ambayo yalitoka kwa Wolper kwenda kwa rafiki yake yakionesha
anabanjuka na mwanaume huyo wa mtu aliyejulikana kwa jina moja la Gee.
YADAIWA NI MUME WA SHOSTI YAKE
Chanzo hicho kilikwenda mbali zaidi kwa kudai kwamba licha ya kuwa ni
mume wa mtu, mwanaume huyo ni bwana wa rafiki yake kutokana na
mawasiliano hayo yalivyosomeka.
“Mashabiki kila siku huwa wanamtetea Wolper na skendo zake, sasa
nakutumia picha pamoja na ‘chating’ zake alizokuwa akichati na shoga
yake kuhusiana na jamaa huyo,” kilisema chanzo hicho.
PICHA ZATUA RISASI JUMAMOSI
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wa Risasi Jumamosi
alimtafuta sosi huyo na kufanikiwa kuzitia kibindoni picha hizo kisha
kazi ya kuwasaka wahusika ikaanza.
Wa kwanza kutafutwa alikuwa ni Gee ambaye kwa mujibu wa vyazo tofauti,
ilidaiwa kuwa kwa sasa hayupo Bongo na hakuacha mawasiliano yoyote tangu
alipoondoka.
WOLPER SASA!
Baada ya jitihada za kumsaka mwanaume huyo kugonga mwamba, paparazi wetu alimtwangia simu Wolper ambaye alieleza kila kitu:
Paparazi: Mambo vipi Wolper, nasikia makelele unaweza kusogea sehemu yenye utulivu kuna ishu nataka tuongee?
Wolper: Niko msibani na sasa hivi ndiyo zoezi la kuaga mwili, ngoja niingie kwenye gari nikupigie.
Baada ya dakika 45
Wolper: Haya niambie wangu niko sehemu nzuri.
Paparazi: Ni hivi, kuna habari imetufikia ikiambatanishwa na picha na baadhi ya chating inakuhusu wewe!
Wolper: Habari gani hiyo mbona unanitisha?
Paparazi: Kuna picha zinakuonesha wewe ukiwa katika pozi la kimalavidavi
na jamaa anayedaiwa kuwa ni mume wa mtu. Ukiachana na picha hizo,
zimeambatanishwa chating zinazoonesha ulikuwa ukichati na rafiki yako
kumueleza kuwa mwanaume uliye naye ni mume wa mtu!
Wolper: Kiukweli kabisa bila ya hata kupepesa macho hizo picha ni zangu
na zimepigwa kwa kutumia simu yangu tangu mwaka juzi lakini kuhusiana na
hizo chating siyo zangu hata wewe unaweza kuwa shahidi kwani mara
nyingi huwa tunachati na unajua vizuri ‘floo’ yangu katika kuandika SMS.
Paparazi: Ok, sawa, lakini turudi katika suala la picha, huyu ndiyo bwana’ko wa sasa?
Wolper: Hapana, huyo ni mshikaji wangu tu na tulipiga picha hizo tukiwa
baa tena kipindi kile nahamia tu Mwananyamala (Dar) na sasa hivi hata
sijui huyo mshikaji yuko wapi.
Paparazi: Ina maana huna mawasiliano naye kwa muda mrefu, mtu ambaye mlipiga naye picha kimahaba namna hii?
Wolper: Kweli kabisa, sina mawasiliano naye kitambo nikimaliza tu
kuongea na wewe nitamtafuta na kumuuliza kulikoni picha hizo kuvuja.
Paparazi: Si ulisema umepiga katika simu yako wewe si ndiyo wa kujiuliza kwa nini picha zimevuja?
Wolper: Nilimzawadia simu kama rafiki yangu na picha zikiwa humohumo sikuzifuta.
Paparazi: Haya Wolper ngoja nikuache mi niendelee na majukumu.
Wolper: Poa wangu baadaye nitakucheki.
WOLPER HUYUHUYU
Hii ni mara ya pili kwa Wolper kutuhumiwa kukwapua bwana wa rafiki yake.
Hivi karibuni mshiriki wa Miss Tanzania 2012, Husna Maulid alilalamika
kuwa Wolper kamchukulia bwana’ke aliyemtaja kwa jina moja la Rajab, raia
wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Si Wolper pekee, ‘trendi’ inaonesha kuwa mastaa wengi wa kike hasa wa
filamu wamefanya ishu ya kuporana wanaume kuwa sehemu ya utamaduni
katika tasnia hiyo bila kujua wanajiondolea heshima mbele ya jamii.
Wednesday, June 11, 2014
Flora Mbasha Aelezea Kisa cha Mume wake Mbasha Kumtishia Kumuua, na Tuhuma za Kumbaka Shemeji Yake.
Muimbaji wa Injili Flora Mbasha amefunguka kuhusu kisa cha mume wake,
Emmanuel Mbasha kumtishia kumuua, pamoja na tuhuma za kumbaka shemeji
yake mwenye miaka 17, katika Exclusive Interview aliyofanyiwa.
Flora anaeleza,
“Yani alikuwa mpaka ananitukana matusi ya nguoni kama mtu ambaye hajaokoka”, amesema Flora. “Nikahisi labda kuna kitu amabcho kimemuingia, nikamwambia Mbasha au umerogwa ndugu yangu we unaongea vitu gani hivyo, akawa analalamika tu basi we ndio umerogwa sio mimi.”
Flora ameendelea kusema,
“Na kabla sijatoka ndani alisema we lazima leo nikufundishe adabu alinishika tu akaniniga yani mpaka akaniachia maalama kwenye shingo yani hivi ninavyozungumza mpaka saizi bado shingo yangu inauma yale maumivu niliyoyapata hiyo siku. Nikamwambia Mbasha Mbasha Mbasha unaniuwa hata kuongea siwezi”.
“Huo usiku sikurudi nyumbani na asubuhi Jumatatu yule binti akapiga simu hakunipigia mimi alimpigia mdogo wangu mwingine akamwambia tu mimi naondoka ilikuwa mida kama saa 12 kasoro akasema mi naondoka mi shemeji ameninyanyasa amenidhalilisha kanifanyia kitendo kibaya sana, sasa akamuuliza amekufanyia nini akawa hawezi kuongea kwenye simu akamshauri tu kwamba usiondoke subiri dada yako atakapokuja kwanza anarudi muda si mrefu…kwasababu Yule binti tulikuwa tunakaa nae nyumbani sasa ni miaka kama mitatu au mine naishi nae pale nyumbani namtunza mimi ni mdogo wangu kwahiyo nilikuwa naishi nae hapo ndani kwahiyo alikuwa kama ni mtoto wa kwangu mimi tulikuwa tunamlea pamoja na mme wangu.” Amesema Florah Mbasha.

BONGO MUVI WAGOMBEA KUMPA MKONO RAIS KIKWETE
HATIMAYE staa wa sanaa za maigizo Bongo, marehemu Said Ngamba ‘Mzee Small’ amezikwa juzi Jumatatu katika Makaburi ya Segerea jijini Dar es Salaam,
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF), Simon Mwakifwamba akisalimiana na Rais Kikwete.
Msiba huo ulihudhuriwa na mamia ya watu akiwemo Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Jakaya Kikwete na ujumbe wake kutoka
Ikulu, mastaa mbalimbali na wadau wengine wa filamu.BONGO MUVI WAJITOKEZA
Awali, ilionekana kuwepo harufu ya wasanii wa Bongo Movies Unity kutohudhuria baada ya kutoonekana msibani hapo tangu siku ya msiba na mkesha wa kuamkia siku ya mazishi.

Mzee Chillo akiteta jambo na Rais Kikwete.
Mpaka Jumapili usiku, wasanii wa filamu walioonekana nyumbani kwa
marehemu Mzee Small walikuwa ni Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’, Wastara Juma
na Simon Mwakifwamba ambaye ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania
‘TAFF’.MASTAA WAMGOMBEA JK
Rais Kikwete aliingia msibani hapo na kulakiwa na mwenyeji wake, Rais wa TAFF, Mwakifwamba kisha kusalimiana na watu waliokuwepo msibani ambapo wasanii walionekana kumgombea JK ili washikane naye mkono.
Akizungumza baada ya kushikana mkono na JK, mmoja wa wasanii wa Bongo Muvi ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini alisema: “Ni bahati ya mtende kushikana mkono na rais ndiyo maana hakuna aliyekuwa tayari kuipoteza.
WAKONGWE
Mbali na mzee Olotu, wakongwe wengine walioonekana msibani hapo ni pamoja na Mashaka, Mbembe, Mohammed Fungafunga ‘Jengua’, Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’, Hashim Kambi ‘Ramsey’ na wengine wengi.
Timu ya publicarblog inatoa pole kwa wafiwa wote, ndugu jamaa na marafiki. Mungu awape wepesi katika kipindi hiki kigumu cha mpito. Inshaalah!
Innalillah Wain illah Rajiun.
Tuesday, June 10, 2014
Subscribe to:
Posts (Atom)