Thursday, February 19, 2015

IFM wamtaka Lowassa Ikulu

Mh.Edward  Lowassa
Wanafunzi wa Chuo cha IFM jijini Dar es Salaam wametangaza azma yao ya kumuunga mkono Edward Lowassa iwapo ataamua kugombea nafasi ya Rais katika Uchaguzi Mkuu 2015
Ikulu ya Tanzinia


Jengo la chuo cha IFM

Mbunge afariki ghafla Zanzibar

Mh.Salmin Awadh wakati wa uwahi wake

Mwakilishi wa jimbo la magomeni Zanzibar Mh.Salmin Awadh amefariki ghafla akiwa kwenye kikao cha CCM zanzibar.
Sababu ya kifo chake bado haijafahamika hadi sasa na maziko yamepangwa kufanyika kesho Februari 20 katika kijiji cha Makunduchi, mkoa wa Kusini Unguja.
Marehem Salmini Awadhi licha ya kuwa mwakilishi wa jimbo hilo kwa zaidi ya miaka 9 tangu mwaka 2005, alikuwa ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM, na moja kati ya viongozi waandamizi wa CCM visiwani Zanzibar.
Alizaliwa Tarehe 26 June mwaka 1958 na amewahi kutumikia jeshi la wananchi wa Tanzania kati ya mwaka 1976 na 1986, na mpaka mauti yanamkuta akiwa na umri wa miaka 56 alikuwa ni Makamu mwenyekiti wa bodi ya gazeti la Zanzibar Leo.
Bwana ametoa,bwana ametwaa.R.I.P Salmin Awadh.

Chanjo mpya ya HIV yatoa mafanikio

Mchanganyo wa dawa ya HIV

 Mbinu mpya ya chanjo imeonekana kuwakinga nyani dhidi ya virusi vya HIV ,ripoti ya wanasayansi wa Marekani imesema.
Chanjo kwa kawaida huifundisha kinga ya mwili wa mtu kukabiliana na maambukizi.
Lakini,watafiti katika taasisi ya Scripps mjini Carlifornia wamebadilisha DNA ya nyani hao ili kuzipa seli zao uwezo wa kukabiliana na virusi vya HIV.
Kikosi hicho cha wanasayansi kimetaja hatua hiyo kama mafanikio makubwa na sasa kinataka kuanzisha mbinu hiyo miongoni mwa binaadamu.
Chanjo

Majaribio yaliofanywa miongoni mwa nyani hao katika ripoti ya jarida la asili,yalionyesha kuwa nyani walikingwa kutokana aina yoyote ya virusi vya HIV kwa kipindi cha wiki 34.
Watafiti wanaamini kuwa mpango huo huenda ukawa muhimu miongoni mwa watu ambao wana virusi vya HIV.
Mtanfiti bingwa Professa Micheal Farza ameiambia BBC :'' tunakaribia kupata tiba ,lakini bado tunakabiliwa na vikwazo hususan katika salama wa kuwapa watu wengi zaidi.
''Tunaifurahia na tunadhani kwamba mi mafanikio makubwa,lakini tuna upendeleo''.
Chanjo za HIV zimeshindwa kufanikiwa kwa kuwa virusi hivyo hujibadilisha mara kwa mara kila vinapolengwa na dawa.
Lakini Chanjo hii mpya hulenga eneo ambalo vurusi hivyo hujibadilisha.

Wednesday, February 18, 2015

Mwanafunzi awa chifu mkuu wa kabila la wahehe

Rais Jakaya Kikwete akiwa na chifu Adam Abdul kulia wakati wa kuapishwa
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Chifu mpya wa Wahehe, Chifu Adam Abdu.Rais ameshuhudia kiapo cha chifu mpya wa kabila hilo chifu Adam wa pili aliyetawazwa katika kiti hicho cha uchifu baada ya kifo cha baba yake Abdul Adam Sapi Mkwawa.
Chifu Adam wa pili ni mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Highland iliyopo manispaa ya Iringa na kwa kuwa hajafikisha umri wa miaka 20 kazi ya uchifu itashikiliwa na baba yake mdogo Hassan Mkwawa

Saturday, February 7, 2015

SERIKALI KUSHUGHULIKIA WANAOSABABISHA MIGOGORO YA ARDHI

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda
Mkutano wa 18 wa Bunge la Jamhuri ya muungano umemalizika leo kwa bunge kujadili na kupitisha maazimio ya jinsi ya kumaliza migogoro ya ardhi nchini.
Katika maazimio hayo yaliyopokelewa na serikali , serikali imeziagiza mamlaka husika kuwachukulia hatua watendaji wote waliopewa dhamana za uongozi ambao wanasababisha migogoro ya Ardhi, Wakulima na Wafugaji kuendelea na kuifanya kama miradi yao ya kujiingizia kipato katika kufanya usuluhishi.
Akipokea mapendekezo ya kamati teule iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza na kuchambua Sera mbalimbali zinazohusu masuala ya Ardhi, kilimo, Mifugo, Maji na Uwekezaji Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda amesema Serikali imepokea mapendekezo yote saba yaliyotolewa na kamati hiyo na kuahidi kuyafanyia kazi.
Pinda amesema kuwa Taarifa ya Kamati hiyo imeonesha kuwa migogoro mingi imeshindwa kumalizika kutoka na baadhi ya watendaji kuifanya kama miradi yao ya kiuchumi na kuendelewa kuyagawa makundi ya wakulima na wafugaji.
Katika mkutano huo, jumla ya maswali 122 ya msingi na 313 ya nyongeza yameulizwa na kujibiwa na jumla ya maswali 15 ya msingi na 13 ya nyongeza yaliulizwa na kujibiwa kwa utaratibu wa papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.
Mbali na maswali hayo, bunge lilipokea na kujadili taarifa mbalimbali za kisekta na zisizo za kisekta na kupitisha mapendekezo mbalimbali kwa ajili ya kutekelezwa na serikali.
Mkutano huo wa 18 wa Bunge umehitimishwa leo, na Bunge kuahirishwa hadi Tarehe 17 Machi. 2015.